Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,053
- 6,304
Kuna UBAYA gani kuwa MIDDLE CLASS?
Kuna UBAYA gani kuwa MIDDLE CLASS?
Nafikiri watu wanalinganisha maisha ya Ulaya na huku kwetu. Ulaya public transport ni reliable na pia unaweza kupanga kwenye appartment na maisha yakendelea bila shida.
Huku kwetu ni tofauti kabisa, kwa wale wanaoishi Dsm adha ya usafiri ni kubwa kupita maelezo, ndiyo maana vijana wengi wanaona ni bora kujilipua na gari ili kurahihisha mobility zao. Hata ukiwa na biashara ukiwa na gari inakusaidia sana pia.
Kwenye nyumba pia Ma landlord wa Bongo hawaeleweki, na hakuna sheria inayodhibiti upangishaji wa nyumba, ndiyo maana wenye nyumba wanapanga kodi jinsi wanavyojisikia bila hata kujali ubora wa nyumba zenyewe, mwenye nyumba pia anaweza kukufukuza kwenye nyumba wakati wowote tena bila kosa lolote la maana.Ukiwa mkorofi ndiyo kabisa utakuwa ni mtu wa kutafuta nyumba kila mwezi.
Kwa mazingira hayo ndiyo maana Bongo nyumba ni security kubwa sana. Ukiweza kujenga nyumba na ukawa na usafiri wako then your very free to take risk of investment.
Kwahiyo mimi naona ni bora ukakamilisha kwanza nyumba na gari then ukaanza kutake risk za biashara, you will be very secured.
Ame graduate at 25 akaajiriwa na kupanga nyumba ya 150,000
At 30 ana familia na amejaliwa watoto wa 2 aendelee kupanga nyumba ya 300,000?asijenge!
Unafananisha us/uk kwenye 'nhc' nyingi na zile apartment binafsi hamna manyanyaso
Mtoa mada anaweza akawa yupo sawa tatizo ni kwamba hajawapoint vizuri wale watu wanaohusika, I mean graduates, ambao wengi wao wanaanza na mshahara wa laki 5,
Hawa watu wengi wao baada ya miaka 2 wanachukua mikopo na kununua magari bila ya kufungua hata kigenge au sehem ya kuchomea chips,
Lakni kwa mtu ambae anauwezo wa kujenga nyumba inamaanisha kipato chake ni kizuri coz huwez jenga nyumba km huna hata uwezo wa kupata milion 2 kwa mwezi nje na bajet yako.
Nyumba ni part ya investments otherwise umejenga sehem ambayo hata hati huwez kupata na ni sehemu isiyo na soko hata benk ukienda utapewa milion 10
Wadau, hasa vijana wenzangu,
Ushauri kwa vijana wenzangu. Ukiona wewe kwanza ndiyo umepata kazi, ukaanza kwa kununua gari la kutembelea, baada ya hapo ukanunua kiwanja na ukaanza kujenga ujue wewe utaishia kuwa middle class na kuteseka ki uchumi katika maisha yako yote. Ninaposema kuteseka ki uchumi namaanisha kila ikihitajika laki moja wewe kuitoa mpaka ukope au ukitoa unaishiwa. Vijana wengi wanapenda kuishi maisha ya luxury wakati hawana sifa ya kuwa na luxury, unakuta ndani kwake kajaza vifaa expensive wakati hana rasilimali ya kumpa kipato, wengi wanafanya hivyo ili waonekane wako na maisha safi kwa jamii, kumbe wanajichimbia kaburi
Asilimia kubwa ya middle class walieanza kwa ku invest kwenye mambo yasiyozalisha, mfano nyumba ya kuishi mwenyewe au gari, ukianza, ukianza kwa kujenga nyumba ya kuishi wewe ndio mbaya kabisa. Watu tunaowaita matajiri, walianza kwa ku invest kwenye kitu kinachozalisha pesa then gari la kutembelea, nyumba vikaja baadae. Huo ni ushauri wangu kwa vijana wenzangu
BAADA YA KUONA SIELEWEKI, NIMEONA NIWAPE MFANO HUU.
Hapa Tanzania, Wahindi wamekuwa waoga kujenga Tanzania kwa hofu kuwa labda hapa si kwao. Wahindi wanaishi National Housing kwa kupanga, ni mabillionaire, wameshika uchumi wa nchi hii, hawatishwi na kodi za nyumba, mfano kwa Arusha wanalipa kodi hadi 1.5m kwa mwezi.
Sasa vipi wewe Mtanzania ungeanza na biashara then Nyumba?
lakini hiyo pesa uliyojengea nyumba,ungeinvest pengine badala ya kujenga nyumba baada ya miaka mitano,ungeweza kununua nyumba na ukabaki na investment zako.nashangaa huyu anataka kutisha watu. hebu waangalie na kodi wanazolipa wenye nyumba sahv ndio waone kama kujenga nyumba mapema inalipa au lah.
lakini hiyo pesa uliyojengea nyumba,ungeinvest pengine badala ya kujenga nyumba baada ya miaka mitano,ungeweza kununua nyumba na ukabaki na investment zako.
unataka.wote wawe first.class ndugu? au ukisema middle class unamaanisha nini naweza sema kwa Tanzania asilimia 5% ndo first class...wakiwemo wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa sana kama kina mengi na bakhera mfano..na watu wengine wachache ambao wanauwezo wa kuearn mil angalao 10 kwa mwez..
hao middle.class unaowakataa ndo wapo kina sisi wengi kiasi kama 45% na kama 55% ni lower class hii ni kwa mujibu wa world bank (2012).
sasa ndugu mtu kuanza na kununua gari ama kujenga nyumba ama kuspend ni maisha yake..kuna wanaopenda maendelei na wapo wanaopenda pia luxury life na yote haya hufanya kwa mipango yake.mtu anaweza kufikiria kujenga nyumba ni mil 50 na hapo amepanga..bado anapigania daladala..sasa kama mshahara wake unaruhusu kununua vitz ya mil.5 kwanini asinunue wakati hiyo mil 5 haitoshi kujenga ama kuanzisha biashara? kila mtu ana malengo yake hata biashara si kila mtu anaweza kuwa interested na biashara fulani..mfano..nina mpangaji wangu ana mke na watoto 2 amepanga rum 2 self analipa laki 250,000/-.kwa mwezi..na ana harrier anapack hapo nje..sasa mtu kama huyu ana malengo yake ameamua kupanga na kununua gar kwanza kama sehem ya malengo yake aliyojiwekea then ndo ajenge..huwezsema awekeze kwenye kuzalisha kumbe hayuko interested na biashara wala nini..mwingine anaona kero kupanga anaamua kujenga kwanza..so kwa suala kama hili jamani linatofaut miongoni mwa watu kulingana na vipaumbele vyao..tena mtu anaeanza kazi na kujenga namheshim coz kujenga sio mchezo..
ila kusema watu watabaki middle clasa umenishtua ndugu..hongera kwakua upo first class na sijui kama tutafika huko ukizingatia gape linazidi kuwa kubwa baina ya wenye nacho.na wasiokua nacho na wanaokitafuta..
ndo hapo ndugu lakini si kila mtu yupo interested na ujasiriamali ndugu..
Ni investment gani ipo certain kiasi hicho? Yaani in 5 years uwe umerudisha mtaji wako na una ziada ya kununua nyumba! Hembu toa mifano halisi ueleweke vizuri. Tena kwa wale ambao wanaotaka kufanya biashara huku wakiendelea na kazi zao ofisini ndiyo ngumu kabisa kufanikiwa, biashara inahitaji usimamizi. Ukipata hela yako ni bora ujenge nyumba, nunua gari, acha maisha yaendelee.
Vijana mmekuwa too global mpaka mnasahau mnaishi Mabibo na mivinjenilakini hiyo pesa uliyojengea nyumba,ungeinvest pengine badala ya kujenga nyumba baada ya miaka mitano,ungeweza kununua nyumba na ukabaki na investment zako.