Acha wabishe tu ila watakukbali siku moja.
Maana sio kila mtu lazima akubali ushauri huu ila kinachokubaliwa na wengi ndio chenye tija,maana kuna watu hata Mungu hawamkubali itakuwa mada hii.
Mie ni shuhuda wa hili na ninakubaliana sana na jamaa juu ya mada hii.
Niliajiriwa mwanzo nikafanikiwa kujenga nyumba,haikuisha ikaishia kwenye hatua za mwisho za kuezeka,then nikaacha kazi baada ya mshahara kuwa wa mwezi 86,baada ya hapo hali ikawa ngum kuliko maelezo.
Nikawa na nyumba ambayo haijaisha huku hata pesa ya kula sina na nauli sina,naenda town kwa mguu huku thamani ya nyumba ni kama 16m kulingana na hatua iliyofika na Kiwanja,maana nilinunua eneo kubwa ili niweke vitu vya kuchezea wanangu.Na pia ilikuwa Semi VIP area of our class.
Na mbaya zaidi kama unavyosema mie nilifikira ku invest kwenye bisahara iwe mwisho.
Akatokea Jamaa mmoja akaniambia sasa mkuu hapo ulipo una nyumba ambayo haijaisha na haikaliki na unapiga mizinga ya buku,mara mia tanona stresses kibao,unaweza kufa kwa mawazo huku mtaji unao.Na ukizingatia umepanga Chumba
Sasa akanishauri niuze,nilikuwa mbishi ile mbaya,maana aliniambia kijuu juu sana,sasa kwa vile mungu alikuwa amenipangia nitoke,baada ya wiki yule jamaa aliniita sehem na kunipa Darasa la maana kama jamaa hapo juu,nikamuelewa.
Basi nikaitia ile unfinished house sokoni,haikuchukua muda ikapata mteja kwa 25m kwa thamani ya wakati huo.
Yaani siku nalipwa nililia sana kwa kuona nauza nyumba yangu of my Dream hata kama haijaisha,nililia kwa kuza nyumba maana suala la kupata pesa ya mauzo nilijua nitapata tu kwa eneo lile lazima ningepata Mtu.
Sasa,akanishauri kwamba pesa iweke Bank kwa muda wa miezi miwili huku ukifiria ufanye nini na usikurupuke.
Ndio nikalipa pesa kwenda SIDO dodoma kusomea usindikaji wa vyakula.
Baada ya kumaliza nikaja kuanzisha Bisahara ya Viungo,maana kule nilikutana na Wajasiriamali wengi na upeo tofauti kwahiyo nilijifunza mengi sana na nilipata moyo sana.
Na nilienda Dodoma kwa kutegema kwamba nitakutana pia na wajasiriamali wa bisahara ya Asali ambayo ilikuwa ni ndoto yangu ya pili kwa baadae.
Baada ya mwaka mmoja nikaanza kufanyabiashara ya Viungo baada ya kusajili Kampuni,na hili suala ndugu zangu la kusajili kampuni ni rahisi sana na bei chee kabisaa,ila mtu akisikia Kampuni anaogopa.
Hii ikanifanya niwe sugu na mkavu kweli,maana ukiwa mjasirimali weka aibu pembeni na ujitoe muhanga kwa lolote na popote.
Baadaya kusajili kampuni na kununua kimtambo kidogo cha kusaga viungo na mambo mengine,nikakodi nyumba ya kupanga,yaani nyumba nzima kodi ya 250,000,yaani makazi na ofisi humohumo.
Nikapita sehem kibao kunadi bidhaa hiyo,kisha nikaenda kwenye mahoteli makubwa,huko unakumbana na changamoto kibao,ila kwenye 20 ukipata moja basi ni hatua kubwa sana.
Basi nikafanikiwa ku supply kwenye hotel mbili na pia nikafungua duka dogo mjini.Na kule SIDO nilipata rafiki zangu na wao wakaniambia wazo lako zuri ukiwa tayari utuambie na sie kama tunawaeza kuwa Agents kwa Commission,so nikaweza pia kupenya soko la baadhi ya mikoa,licha ya kwamba ni kwa kiwango kidogo sana Maana Viungo vingi hutumika sana ukanda wa Pwani.Na ndio maana nilikweda pia Mombasa kuangalia hali ipoje ila sherida kidogo za kule zikanibana,lica ya kwamba njia za magendo zipo nyingi lakini risk sana.
Naangalia namna ya kufanikisha taratbu za vibali kwa baadae.
Sasa baada ya hapo na kufanya biashara kwa muda nikaweza kununua Bodaboda kama Tano hivi ila nilianza na tatu,then nikaongeza mbili,kisha Carry tatu,moja ni ya Biashara zangu.
Ndio nikasema kwamba Bodaboda zote ni kwa kujenga nyumba na Carry moja ni kusomesha my two children International School na matumizi binafsi.
Yaani nimejenga kwa urahisi sana,maana kila mwezi nilikuwa naenda na mafundi kwa ajili ya ujenzi wa kidogo kidogo mpaka nikamaliza kwa huku,then ndio nikahamia Chanika Dar na pia nikajenga kwa style ile ile.
Maana Bodaboda moja naletewa hesabu ni Tsh:50,000 kwa wiki,kwa hiyo inakuwa (Tsh:50,000 x 5 Bd x 30 = Jumla Tsh:1,050,000 kwa mwezi
Sasa Mie nakubaliana sana na jamaa,kujenga ni rahisi sana kama ukiwa na mradi na ku-locate baadhi ya pesa kwenye Ujenzi.Maana siku hizi mafundi tupo nao mitaani,yaani hata ukipata laki mbili basi unakwenda nae over wekend,mnapiga mzigo kisha mnasepa,ukipata tena unafanya the same,basi utamaliza nyumba bila hata kuamini.
Nahisi kama kuna kipindi vijana tuna limit uwezo wetu wa kufikiri na kuamua na kuona kwamba mimi biashara hii siiwezi hata kama inalipa vipi.Hembu jifunze uone.Hakuna kitu chepesi namna hiyo nakuna biashara inaoingiza pesa nyingi kwa haraka kwa muda mfupi,inatakiwa uvumilivu wa hali ya juu na nidhamu ya pesa na muda.
Mara nyingi vijana huiga nani kafanya nini na kwanini kafanikiwa kwa muda mfupi,unasahau kwamba unaesema kafanikiwa kwa muda mfupi sio kweli,nikwamba muhangaikaji ndio anajua muda na miaka mingapi ameteseka katika kutafuta pesa,ila sie tunaemtizama ndio tunaona kama pesa kapata juzi tu,na kama kawaida ya vijana wengi tuna ugonjwa kukatishana tamaa sie kwa sie.
Ndio maana tunashauriwa kusoma sana vitabu vya ujasiriamali na pia kujifunza kwa waliopiga hatua walizopita katika hali ngum mpaka kufanikiwa.Maisha sio rahis kabisa kama hutoishughulisha akili yako kufikiri na kufanya maamuzi magum.
Mfano mdogo wa mlio Dar,hivi mnafaham kwamba Mamalishe wengi wa Dar wana viwanja vyao na wengine wananyumba zao na wanasomesha watoto wao kwenye shule nzuri tu?Na unajua kwamba mtaji wao hata laki moja haufiki kwa baadhi yao,na ndio wanaoongoza kuhudhuria semina za ujasiriamali napia ndio wenye nidhamu kubwa sana ya pesa na pia baadhi yao wameweza hadi kuwa na miradi mingine zaidi ya hiyo.Hawa ndio Role Model wangu na nimejifunza mengi kupitia mifano yao.