Ukiwa na tabia hizi, jiandae kuwa middle class na kuteseka ki uchumi!

Ukiwa na tabia hizi, jiandae kuwa middle class na kuteseka ki uchumi!

Hapana mkuu nyumba ni asset, asset is anything with economic value to the owner and that can be converted to cash however cash itself is an asset. Hata kama nyumba unaishi mwenyewe still is an asset coz it has value and can be converted to cash at future. Hata ukinunua kiwanja ukakiacha usifanyie shughul yoyote ile ni asset, coz land has economic value and you can expect cash flow at future, soma hapa: http://m.investorwords.com/273/asset.html

(i stand to be corrected)
 
Akili yangu ipo wazi sana lakini kuna watu wanataka kutuambia kuwa kujenga ni kuzika pesa kama walivyokaambiwa na Robert kiyosaki ni hapo tu ndipo napopinga,usafiri binafsi pia ni muhimu ktk kukuwezesha kufuatilia biz zako

mkuu saba7 nadhani hujamuelewa mleta mada haujakatazwa kujenga nyumba wala kununua gari ila inatakiwa ujue position yko kiuchumi kwa wakat huo huo km Una mil 12 hlf zote unatka ujengee nyumba hpo ndyo cyo sawa! kwanini hzo mil 12 usifungue mirad km mitatu tofauti uizungushe hyo hela ndani ya mwaka ifike mil 40 then baada ya hpo ndyo unaanza kujenga nyumba yko very comfortable...kwa mfano mini km nilivyokupa mfano hpo juu ningesema hyo mil 1.5 ni ndogo nikanunua pikipiki kwa ajili ya luxury leo hii ningekuwa WP???
 
Ndugu maisha hayana formula maalumu.Gali na nyumba vina u muhimu wake,lita tano za mafuta zinaweza kunipeleka mbali.Sio muda wote hutahitaji daladala,zipo dharura za haraka zita hitaji taxii,kama taxii ningelipa Tsh.10,000 mafuta nitaweka ya sh.5,000 tu,kama uta nunua gari nzima basi gharama za lazima ni ku service gali yako,bima na Load licence hivi viwili kwa mwaka,service kila Km. 3,000 na kuendelea na pia inategemea aina ya oil uliyo nunua sababu ya BP inaenda hadi Km.5,000.Pia huokoa muda wazungu husema "Time is money".

Nyumba ukijenga unatulia na ina dhamana hata kwa mikopo,tena mikopo mingine haihitaji hati bora mali isiyo hamishika hasa kwa baadhi ya benki binafsi.Wapo matajiri walio kopa waka endelea na wapo waliokopa wakafirisika au kufirisiwa no formula hata biashara zilizo fanyiwa resarch kabla ya kuanza huweza kufirisika mfano word adams na hata viwanda vingi wanaendesha wenye mitaji.Biashara hiyo hiyo ukishindwa mwenzio anaweza kuianzisha eneo hilo hilo na ikawepo.Hakuna formula.Maisha kila mtu ana tengeneza Formula yake hakuna kuigana,hata ukiiga baadae uliye muiga anaweza kubadilisha je utamuiga tena?
 
Ndugu maisha hayana formula maalumu.Gali na nyumba vina u muhimu wake,lita tano za mafuta zinaweza kunipeleka mbali.Sio muda wote hutahitaji daladala,zipo dharura za haraka zita hitaji taxii,kama taxii ningelipa Tsh.10,000 mafuta nitaweka ya sh.5,000 tu,kama uta nunua gari nzima basi gharama za lazima ni ku service gali yako,bima na Load licence hivi viwili kwa mwaka,service kila Km. 3,000 na kuendelea na pia inategemea aina ya oil uliyo nunua sababu ya BP inaenda hadi Km.5,000.Pia huokoa muda wazungu husema "Time is money".

Nyumba ukijenga unatulia na ina dhamana hata kwa mikopo,tena mikopo mingine haihitaji hati bora mali isiyo hamishika hasa kwa baadhi ya benki binafsi.Wapo matajiri walio kopa waka endelea na wapo waliokopa wakafirisika au kufirisiwa no formula hata biashara zilizo fanyiwa resarch kabla ya kuanza huweza kufirisika mfano word adams na hata viwanda vingi wanaendesha wenye mitaji.Biashara hiyo hiyo ukishindwa mwenzio anaweza kuianzisha eneo hilo hilo na ikawepo.Hakuna formula.Maisha kila mtu ana tengeneza Formula yake hakuna kuigana,hata ukiiga baadae uliye muiga anaweza kubadilisha je utamuiga tena?

Wonderful comment...key word MAISHA HAYANA FORMULA..nimekubali naunga mkono hoja...Nyumba wawezaitumia kwa mkopo au dhamana mahakamani nk
 
Wakuu nimewasoma wote vizuri sana basi hebu na mie nitupia machache tuu...maisha ni malengo!!!mtu unatakiwa uwe na malengo yako ili mradi uje uishi vizuri wewe na familia yako...kwa sababu sio wote wamezaliwa wawe wafanyabiashara au waajiriwa.Mie nilivyomaliza college nilifanya kazi kidogo hapo Dar lakini malengo niliojiwekea ili nitoke kimaisha ilikua ni lazima niondoke bongo,kwa hio nilikichanga, pesa ilipotosha nikalipa chuo nikakimbilia kwa Obama...nikafika nikala shule nikasave nikashusha mijengo miwili bongo na nikaoa mmbongo na nina familia maisha yanaenda ingawa nw niko kwa pele bado nakichanga na familia iko kwa obama poa... na kila mwaka lazima nije vacation na familia bongo.kwa hio basi maisha ni malengo tu na sio biashara tu ndio inayoweza kukutoa.,tuige mataifa mengine, kama hizo za kusafiri kwenda ughaibuni kusaka life wakenya na waganda wanafanya sana na wengi wao shule ziko vizuri na wana mafanikio sana...kingine lazima tuweke moyo wa kutokata tamaa pindi hali inapokua sivyo kwasababu "winners never quit", na unaweza kuanza na gari au nyumba ukawin kuliko hata huyo aliwekeza kwa biashara...malengo ni muhimu sana.
nawakilisha.
 
True kabisa tena umenyuka suite yako ya kazi na heels unakimbilia daladala usiombe mvua inyeshe weweee ,kamata vitz kula kiyoyozi saafii

chamsingi unapoamua kufanya kitu chochote fanya kikiwa kweli kina umuhimu wa kukifanya kwa wakati huo na sio ilimradi unafanya kama kuionyesha jamii, kama wabongo wengi wanavyofanya
 
acha wabishe tu ila watakukbali siku moja.
Maana sio kila mtu lazima akubali ushauri huu ila kinachokubaliwa na wengi ndio chenye tija,maana kuna watu hata mungu hawamkubali itakuwa mada hii.

Mie ni shuhuda wa hili na ninakubaliana sana na jamaa juu ya mada hii.


niliajiriwa mwanzo nikafanikiwa kujenga nyumba,haikuisha ikaishia kwenye hatua za mwisho za kuezeka,then nikaacha kazi baada ya mshahara kuwa wa mwezi 86,baada ya hapo hali ikawa ngum kuliko maelezo.
Nikawa na nyumba ambayo haijaisha huku hata pesa ya kula sina na nauli sina,naenda town kwa mguu huku thamani ya nyumba ni kama 16m kulingana na hatua iliyofika na kiwanja,maana nilinunua eneo kubwa ili niweke vitu vya kuchezea wanangu.na pia ilikuwa semi vip area of our class.
Na mbaya zaidi kama unavyosema mie nilifikira ku invest kwenye bisahara iwe mwisho.

Akatokea jamaa mmoja akaniambia sasa mkuu hapo ulipo una nyumba ambayo haijaisha na haikaliki na unapiga mizinga ya buku,mara mia tanona stresses kibao,unaweza kufa kwa mawazo huku mtaji unao.na ukizingatia umepanga chumba

sasa akanishauri niuze,nilikuwa mbishi ile mbaya,maana aliniambia kijuu juu sana,sasa kwa vile mungu alikuwa amenipangia nitoke,baada ya wiki yule jamaa aliniita sehem na kunipa darasa la maana kama jamaa hapo juu,nikamuelewa.
Basi nikaitia ile unfinished house sokoni,haikuchukua muda ikapata mteja kwa 25m kwa thamani ya wakati huo.
Yaani siku nalipwa nililia sana kwa kuona nauza nyumba yangu of my dream hata kama haijaisha,nililia kwa kuza nyumba maana suala la kupata pesa ya mauzo nilijua nitapata tu kwa eneo lile lazima ningepata mtu.

Sasa,akanishauri kwamba pesa iweke bank kwa muda wa miezi miwili huku ukifiria ufanye nini na usikurupuke.


ndio nikalipa pesa kwenda sido dodoma kusomea usindikaji wa vyakula.
Baada ya kumaliza nikaja kuanzisha bisahara ya viungo,maana kule nilikutana na wajasiriamali wengi na upeo tofauti kwahiyo nilijifunza mengi sana na nilipata moyo sana.
na nilienda dodoma kwa kutegema kwamba nitakutana pia na wajasiriamali wa bisahara ya asali ambayo ilikuwa ni ndoto yangu ya pili kwa baadae.
baada ya mwaka mmoja nikaanza kufanyabiashara ya viungo baada ya kusajili kampuni,na hili suala ndugu zangu la kusajili kampuni ni rahisi sana na bei chee kabisaa,ila mtu akisikia kampuni anaogopa.
Hii ikanifanya niwe sugu na mkavu kweli,maana ukiwa mjasirimali weka aibu pembeni na ujitoe muhanga kwa lolote na popote.
Baadaya kusajili kampuni na kununua kimtambo kidogo cha kusaga viungo na mambo mengine,nikakodi nyumba ya kupanga,yaani nyumba nzima kodi ya 250,000,yaani makazi na ofisi humohumo.
Nikapita sehem kibao kunadi bidhaa hiyo,kisha nikaenda kwenye mahoteli makubwa,huko unakumbana na changamoto kibao,ila kwenye 20 ukipata moja basi ni hatua kubwa sana.
Basi nikafanikiwa ku supply kwenye hotel mbili na pia nikafungua duka dogo mjini.na kule sido nilipata rafiki zangu na wao wakaniambia wazo lako zuri ukiwa tayari utuambie na sie kama tunawaeza kuwa agents kwa commission,so nikaweza pia kupenya soko la baadhi ya mikoa,licha ya kwamba ni kwa kiwango kidogo sana maana viungo vingi hutumika sana ukanda wa pwani.na ndio maana nilikweda pia mombasa kuangalia hali ipoje ila sherida kidogo za kule zikanibana,lica ya kwamba njia za magendo zipo nyingi lakini risk sana.
Naangalia namna ya kufanikisha taratbu za vibali kwa baadae.

Sasa baada ya hapo na kufanya biashara kwa muda nikaweza kununua bodaboda kama tano hivi ila nilianza na tatu,then nikaongeza mbili,kisha carry tatu,moja ni ya biashara zangu.
Ndio nikasema kwamba bodaboda zote ni kwa kujenga nyumba na carry moja ni kusomesha my two children international school na matumizi binafsi.
Yaani nimejenga kwa urahisi sana,maana kila mwezi nilikuwa naenda na mafundi kwa ajili ya ujenzi wa kidogo kidogo mpaka nikamaliza kwa huku,then ndio nikahamia chanika dar na pia nikajenga kwa style ile ile.
Maana bodaboda moja naletewa hesabu ni tsh:50,000 kwa wiki,kwa hiyo inakuwa (tsh:50,000 x 5 bd x 4wk = jumla tsh:1,000,000 kwa mwezi

sasa mie nakubaliana sana na jamaa,kujenga ni rahisi sana kama ukiwa na mradi na ku-locate baadhi ya pesa kwenye ujenzi.maana siku hizi mafundi tupo nao mitaani,yaani hata ukipata laki mbili basi unakwenda nae over wekend,mnapiga mzigo kisha mnasepa,ukipata tena unafanya the same,basi utamaliza nyumba bila hata kuamini.

Nahisi kama kuna kipindi vijana tuna limit uwezo wetu wa kufikiri na kuamua na kuona kwamba mimi biashara hii siiwezi hata kama inalipa vipi.hembu jifunze uone.hakuna kitu chepesi namna hiyo nakuna biashara inaoingiza pesa nyingi kwa haraka kwa muda mfupi,inatakiwa uvumilivu wa hali ya juu na nidhamu ya pesa na muda.
Mara nyingi vijana huiga nani kafanya nini na kwanini kafanikiwa kwa muda mfupi,unasahau kwamba unaesema kafanikiwa kwa muda mfupi sio kweli,nikwamba muhangaikaji ndio anajua muda na miaka mingapi ameteseka katika kutafuta pesa,ila sie tunaemtizama ndio tunaona kama pesa kapata juzi tu,na kama kawaida ya vijana wengi tuna ugonjwa kukatishana tamaa sie kwa sie.
Ndio maana tunashauriwa kusoma sana vitabu vya ujasiriamali na pia kujifunza kwa waliopiga hatua walizopita katika hali ngum mpaka kufanikiwa.maisha sio rahis kabisa kama hutoishughulisha akili yako kufikiri na kufanya maamuzi magum.

mfano mdogo wa mlio dar,hivi mnafaham kwamba mamalishe wengi wa dar wana viwanja vyao na wengine wananyumba zao na wanasomesha watoto wao kwenye shule nzuri tu?na unajua kwamba mtaji wao hata laki moja haufiki kwa baadhi yao,na ndio wanaoongoza kuhudhuria semina za ujasiriamali napia ndio wenye nidhamu kubwa sana ya pesa na pia baadhi yao wameweza hadi kuwa na miradi mingine zaidi ya hiyo.hawa ndio role model wangu na nimejifunza mengi kupitia mifano yao.

salute
 
Jaman investment ni perception on how will you generate income. Nyumba sio lazima uijenge kisha ukakuishi .Inaweza kupangishwa kwa waindi kama wanavyofanya Arusha, then na ww umepanga uswahilini real estate business guys msichanganyikiwe just think every thing can be invested.good night
 
Kaka ulishaanza biashara bila kujua kwamba umeanza biashara.Hiyo nyumba ndio mtaji wako. usingejenga bro ukaingia kwenye business wakati ukiwa kazini ungepoteza sana hasa kwenye nchi ambayo waaminifu wanahesabika? lakini iliweka store fedha yako kwa thamani ya nyumba. you can do it again and you will gate more than 25mill
 
Hapana mkuu nyumba ni asset, asset is anything with economic value to the owner and that can be converted to cash however cash itself is an asset. Hata kama nyumba unaishi mwenyewe still is an asset coz it has value and can be converted to cash at future. Hata ukinunua kiwanja ukakiacha usifanyie shughul yoyote ile ni asset, coz land has economic value and you can expect cash flow at future, soma hapa: http://m.investorwords.com/273/asset.html

(i stand to be corrected)

you are very right mkuu...
 
Nyumba ni Mtaji...kama una hati zako za umiliki ukifika Benki pale wanakuona km Mungu..ila kwenye suala la kununua gari nakuunga mkono mtoa mada..
 
Nyumba ni Mtaji...kama una hati zako za umiliki ukifika Benki pale wanakuona km Mungu..ila kwenye suala la kununua gari nakuunga mkono mtoa mada..

I wish hiyo hati ingekuwa inapatikana kwa urahisi unaosema, binafsi nilishakata tamaa na hati, anayefahamu jinsi ya kuipata anaweza kutoa maelezo, or else inaweza ikachukua miaka.
 
Inawezekana ni kweli mkuu..mimi naweza kuwa mhanga wa kuwekeza ktk vitu visivyozalisha.mwisho wa siku vyote nimeshindwa kuvikamilisha..
Pole mkuu hata mie ni mhanga kwa mbaliiiii ila wakati mwingine family background na makosa waliyoyafanya wazee wetu plus kodi ya nyumba pia ni ya kunyanyasana kiasi kwamba mtu anaamua kufanya maamuzi ya namna hii, hoja za jamaa zina msingi sana ila kwa mtu ambae ni muajiriwa na muda mwingi yupo kazini huo muda wa ku-invest ataupata wapi wakati amekubali ku-invest elimu yake kuwatajirisha wengine na ndio maana kuna ambao wanaamua kuanza na mjengo kwa kuwa investment yoyote unahitaji kuwa nayo karibu na ukisema umwachie mtu on your behalf unaweza ukapata kichaa maana hela anazitafuna na nyumba unakuta huna. By the way ushauri wake ni mzuri sana ila tunaangalia mazingira na aina ya kazi tunazofanya unless kama mtu amebahatika kuwa mfanya biashara moja kwa moja bila kuajiriwa sehemu though mtu anaweza kuanza na nyumba kwa lengo la kuitumia kama dhamana pindi anapoona mambo ya ajira hayaendi na kuamua kujikita kwenye biashara
 
I wish hiyo hati ingekuwa inapatikana kwa urahisi unaosema, binafsi nilishakata tamaa na hati, anayefahamu jinsi ya kuipata anaweza kutoa maelezo, or else inaweza ikachukua miaka.
Hati inapatikana bila zengwe kama utaamua kuifuatilia pia inategemea na upo eneo gani, kwa uzoefu kwa Dar kidogo inakuwa shida hasa kwa wale ambao wanakaa maeneo ambayo hayajapimwa though huwa wanapewa leseni ya makazi ambayo pia unaweza kuombea mkopo. Kwa mikoa mingine including Rock City hati inapatikana hata kama unaishi eneo ambalo halijapimwa kikubwa eneo uliopo uwe umejenga nyumba pia liwe kwenye master plan ya mji kama eneo la makazi na si viwanda au lilitengwa kwa shughuli zingine
 
Kwa Arusha sawa ila siyo Dar, kodi za nyuma zimepanda sana, mfano mfanyakazi, upate pesa yako ya kujikimu, ufungue biashara, kisha uanze kulipa kodi mbili, pakuishi na biashara, at the same time unakatwa deni la mkopo, utaendelea kukopa ili ulipe nyumba tu, faida haitatosha ulipe pango la biashara, mfanyakazi na nyumba ya kuishi maana mshahara utakaobaki sana sana utaendeshea maisha yako, kujenga nyumba unaweza kujenga pole pole na si nyumba nzima, baada ya hapo badala ya kulipa kodi ndiyo unafungua investment.
Wazo la jamaa ni bomba mno ila pia kuna limitation ambayo ni hiyo uliyoielezea maana huwezi kuwatumikia mabwana wawali yaani huku mwajiriwa na huku mfanya biashara mwisho wa siku hela ikikata na nyumba huna na kazi huna itakuaje hapa? maana mie naona nyumba inaweza baadae ikatumika kama dhamana na kuitumia kupata mkopo then unaanza kufanya biashara

Kwa point yake Nkobe inatupa changamoto kwamba kama unapata hela ya kutosha na ajira yako inakupa muda wa kutosha wa kufanya mambo mengine ni vizuri badala ya kukomaa na nyumba unaweza kufikiria ku-invest ili ujiweke vizuri kiuchumi then unaendelea na masuala ya ujenzi, kwa case yako kama ulivyochangia wakati mwingine ndio changamoto zinazowafanya watu wakomae na mjengo kwanza pia bado hakijaharibika kitu maana unaweza kuitumia nyumba kama dhamana ya mkopo.
 
Last edited by a moderator:
Wadau, hasa vijana wenzangu,

Ushauri kwa vijana wenzangu. Ukiona wewe kwanza ndiyo umepata kazi, ukaanza kwa kununua gari la kutembelea, baada ya hapo ukanunua kiwanja na ukaanza kujenga ujue wewe utaishia kuwa middle class na kuteseka ki uchumi katika maisha yako yote. Ninaposema kuteseka ki uchumi namaanisha kila ikihitajika laki moja wewe kuitoa mpaka ukope au ukitoa unaishiwa. Vijana wengi wanapenda kuishi maisha ya luxury wakati hawana sifa ya kuwa na luxury, unakuta ndani kwake kajaza vifaa expensive wakati hana rasilimali ya kumpa kipato, wengi wanafanya hivyo ili waonekane wako na maisha safi kwa jamii, kumbe wanajichimbia kaburi

Asilimia kubwa ya middle class walieanza kwa ku invest kwenye mambo yasiyozalisha, mfano nyumba ya kuishi mwenyewe au gari, ukianza, ukianza kwa kujenga nyumba ya kuishi wewe ndio mbaya kabisa. Watu tunaowaita matajiri, walianza kwa ku invest kwenye kitu kinachozalisha pesa then gari la kutembelea, nyumba vikaja baadae. Huo ni ushauri wangu kwa vijana wenzangu

BAADA YA KUONA SIELEWEKI, NIMEONA NIWAPE MFANO HUU.

Hapa Tanzania, Wahindi wamekuwa waoga kujenga Tanzania kwa hofu kuwa labda hapa si kwao. Wahindi wanaishi National Housing kwa kupanga, ni mabillionaire, wameshika uchumi wa nchi hii, hawatishwi na kodi za nyumba, mfano kwa Arusha wanalipa kodi hadi 1.5m kwa mwezi kwa nyumba ambazo si national housing huko Arusha.
Sasa vipi wewe Mtanzania ungeanza na biashara then Nyumba?


Usipotoshe watu,sio lazima kuanza kama walivo anza wahindi.
Naweza nunua gari ya 10m,lakini siwezi jenga nyumba (yoyote ile)ya 10m.

Kama uwezo wangu ni 10m kwa sasa,na nahitaji gari kwanini nisinunue gari huku nikijipanga na mengine hayo?

Hivi ndivo nilivo anza,na i promise you sita struggle kama unavo taka watu waamini.

1.Nikiwa chuo nikanunua shamba ekari8 kwa 1.3m mkuranga.
2. Nika graduate 2012 na nikanunua gari 2013, (hili lilinisaidia kutembelea shamba kirahisi zaidi,point: Fanya kile unacho weza kufanya kwa wakati huo,don't stretch beyond your limit kwa kukimbilia kujenga afu unaacha nyumba ikiwa kwenye msingi kwa 10 years)

3. Etc etc etc,najua ujenzi jinsi ulivo na gharama zake,ukibebesha mtu mawazo ya JENGA KWANZA kabla ya chochote,tena unasema JENGA NYUMBA YA BIASHARA. Nadhani hauwi realistic,au haujui unacho kiongea in terms ya gharama halisi na maisha halisi ya mwajiriwa wa kitanzania.

Good day.
 
Nimependa sana ushauri wako, ni kweli kabisa, Kuanza kwa kujenga nyumba ya kuishi ni sawa na kuzika pesa, ila watu wengi hili hawalijui kabisa na kuna baadhi ya nchi kisheria huruhusiwi kujenga nyumba kwa pesa yako mwenyewe kwa sababu wanafahamu madhara yake.

nIMEPENDAS

Hivi ukiwa na 50m,ni nyumba gani ya biashara utakayo jenga? Guest house au?
Kila mtu akijenga hiyo mitaa itakuaje? Acheni kupotosha watu.
 
sidhani kama kuna ukweli, maisha ni kujipanga na kupanga ni kuchagua. nyumba na gari nayo ni mahitaji ya msingi sana tu ya kuanza nayo kama hukuwa navyo na haijalishi ununue vya kwanza au vya mwisho, jitihada binafsi ndio muhimu zaidi

Wewe unayajua maisha,sio hawa wanao andika mambo walio jifunza darasani
 
For your information! The richest investor in the world Warren Buffet alianza kujenga nyumba yake before hajaanza biashara alikuwa ameajiliwa wakati huo.
Nawashauri vijana in their 20's to build their career rather than entering into debts.

That is realistic
 
Huo ni ukweli mtupu, mfano wewe unatumia milioni 60 kujenga nyumba ndani ya miaka 4, ukimaliza hiyo nyumba haizalishi chichote, unaishi mwenyewe, vipi kama hiyo 60 kama ungewekeza mfano kwenye ufugaji wa kuku, kama uko serious hao kuku wangekupa hata milioni 4 kwa mwezi na ukajenga kirahisi

Tuna tofautiana vipaumbele,lakini yote maisha na lazima kutoka.
 
Back
Top Bottom