Ukiwa na Uelewa na Ufahamu mpana na wa kutosha wa masuala mbalimbali, ukinyimwa, kukataliwa au kusubirishwa ulichoomba hutojiskia vibaya

Ukiwa na Uelewa na Ufahamu mpana na wa kutosha wa masuala mbalimbali, ukinyimwa, kukataliwa au kusubirishwa ulichoomba hutojiskia vibaya

maoni yangu ni kwamba,
yawezekana vigezo, sifa , uwezo na nyota yako apo kazini vinangara zaidi ya ulowakuta hapo ofisini na hivyo unatishia na kuwapa kimuhemuhe kwamba wakikuacha apo ulipo, haita chukua muda utachukua nafasi zao ....
Kwahiyo unahatarisha nafasi za watu mkuu nenda pole pole kujipambanua.....

Jambo la pili ni kwamba,
huenda wew umekua ni kikwazo cha wao kuendelea kupiga pesa ndefu na kwamba wew ni mtu wa utaratibu na misimamo sana, hupendi konakona hata kwa wakubwa zako ofisini pako...

Jambo la Tatu,
huenda kuna uchawi na ushirikina ndani yake, na hivyo vinawapa ujasiri wa kukuhamisha na kukushusha mshahara na cheo bila wew kuripoti wala kulalamika panapohusika. Wamekufunga mdomo na misuli ya uchumi wako kichawi ukae kimya uone ni jambo la kawaida tu...

Jambo la nne,
Ukiwa kazini, ukitaka kufurahia maisha na kudumu katika status ya juu daima au kwa muda mrefu, na kwa uhakika basi pata kazi kwa haki, fanya kazi kwa bidii na upate kipato halali na sahihi kwa kazi na nafasi ulonayo...

Lakini kupata kwa uchawi na ushirikina na kujipatia kipato kisicho halali huwez enjoy maisha wala kua na uhakika wa kudumu apo kazini, daima utakua mtumwa wa hirizi. Huwez kua na Amani....

hayo ni kwa uchache sana. Endelea kumtegemea Mungu, jishushe kwa kwa wakati huu unaponyanyasika bila sababu, na kwa wakati muafaka Mungu mwenyezi atakupandisha juu, kwani ndipo unapostahili 🐒
Lakini jambo hilo kwa mfano halijatokea kwa mistake yaani limetokea hata wenzio nyote mmeondolewa kama kwenda kuanzisha sehemu nyingine ..Mfano ni mtaalamu basi umetolewa bila ya chuki ila umepelekwa halmashauri ya kijijini huko hamna tena posho kama mjini na wenzio ili kusaidia katika kazi halmashauri hiyo
 
Lakini jambo hilo kwa mfano halijatokea kwa mistake yaani limetokea hata wenzio nyote mmeondolewa kama kwenda kuanzisha sehemu nyingine ..Mfano ni mtaalamu basi umetolewa bila ya chuki ila umepelekwa halmashauri ya kijijini huko hamna tena posho kama mjini na wenzio ili kusaidia katika kazi halmashauri hiyo
kwa miaka 10 ilopita nikiwa katika siasa huko vijijini watumishi walopelekwa huko mathalani mahakimu, madaktari, walimu, maafisa organi, watendaji kata na vijiji wamebadidika mno huko na kwakweli wamebadilisha hali ya muonekano hadi uchumi wa vijijini....
For sure, wametumia fursa kule vijijini ipasavyo...

Fursa nyingi walizonazo zimewafanya hivi sasa wao ndio wana majumba mazuri huko, magari mazuri, wao ndio wana mabar, guest house na malodge ya kisasa, mastationary na maduka ya fedha, wao ndio wana mashamba makubwa hivi sasa, wao ndio wafanyabiashara wakubwa mazao na ndio wanaokopesha wanakijiji kwa riba au kwa mfano anakupa elfu60 leo kipindi kilimo halafu, kipindi cha mavuno anakuja kuchukua gunia 3 za alizeti au mahindi...

zaidi sana kutokana na uhaba wa watumishi huko halmashauri mtumishi anakaimishwa majukumu zaidi ya moja na kwahivyo suala la posho linakua la uhakika zaidi kuliko mijini....

Mathalani maDMO wengi hukaimishwa ukurugenzi wa halmashauri, unataka posho gani tena daktari ndrugu yangu 🐒

Nenda ukatengeneza fursa ndugu, posho huko halmashauri za vijijini ni uhakika sana coz fedha ni nyingi zimetengwa watumiaji ni wachache...
 
Ujumbe mzuri sana mkuu, naunga mkono mada 99% hiyo 1% sijaelewa huyo nyani wanini?
 
Back
Top Bottom