maoni yangu ni kwamba,
yawezekana vigezo, sifa , uwezo na nyota yako apo kazini vinangara zaidi ya ulowakuta hapo ofisini na hivyo unatishia na kuwapa kimuhemuhe kwamba wakikuacha apo ulipo, haita chukua muda utachukua nafasi zao ....
Kwahiyo unahatarisha nafasi za watu mkuu nenda pole pole kujipambanua.....
Jambo la pili ni kwamba,
huenda wew umekua ni kikwazo cha wao kuendelea kupiga pesa ndefu na kwamba wew ni mtu wa utaratibu na misimamo sana, hupendi konakona hata kwa wakubwa zako ofisini pako...
Jambo la Tatu,
huenda kuna uchawi na ushirikina ndani yake, na hivyo vinawapa ujasiri wa kukuhamisha na kukushusha mshahara na cheo bila wew kuripoti wala kulalamika panapohusika. Wamekufunga mdomo na misuli ya uchumi wako kichawi ukae kimya uone ni jambo la kawaida tu...
Jambo la nne,
Ukiwa kazini, ukitaka kufurahia maisha na kudumu katika status ya juu daima au kwa muda mrefu, na kwa uhakika basi pata kazi kwa haki, fanya kazi kwa bidii na upate kipato halali na sahihi kwa kazi na nafasi ulonayo...
Lakini kupata kwa uchawi na ushirikina na kujipatia kipato kisicho halali huwez enjoy maisha wala kua na uhakika wa kudumu apo kazini, daima utakua mtumwa wa hirizi. Huwez kua na Amani....
hayo ni kwa uchache sana. Endelea kumtegemea Mungu, jishushe kwa kwa wakati huu unaponyanyasika bila sababu, na kwa wakati muafaka Mungu mwenyezi atakupandisha juu, kwani ndipo unapostahili π