dola laki tano ni pesa ndogo sana kusafirisha. watu wanasafirisha bilions. kama upo na bank nzuri hapa bongo, mfano ni CRDB au stanbic, fanya tu transfer toka bank ya ulaya kuja ya bongo. ila kuwa na vielelezo vya usafi (biashara au chochote etc). ikifika hapa, pesa zako hazitakuwa frozen hadi uwe kwenye tuhuma inayopelelezwa na polisi au ukiwa umefunguliwa mashtaka. ukiwa kwenye tuhuma, labda nchi ya nje imeleta tuhuma kwamba umefanya kosa kule ndio unahamishia/unasafishia pesa huku, IGP ana siku chache sana za kufreeze akaunti yako bila amri ya mahakama (7 to 14 days), baada ya hapo bank wanatakiwa kuachia pesa zako manake polisi watakuwa wameshindwa kuleta tuhuma yeyote. kama bank wataendelea kuzuia, unaweza kuwafungulia kesi wakulipe fidia. pia, kama umefunguliwa shauri mahakamani, mahakama inaweza kutoa order baada ya maombi. sasa wewe kama pesa zako ni safi, serikali ya tanzania itakufunguliwa mashitaka ya nini hadi pesa yako iwe frozen? au polisi watafanay uchunguzi wa nini bila kuwepo tuhuma au mlalamikaji? nilishawahi kuwa na account HSBC bank, nilisafirisha pesa zilipofika tu, nilipigiwa simu wakauliza, nikawapa majibu, mambo yaliishia hapo.