Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wana JF wenzang
Baada ya tumbua tumbua iliyofanyika jana, na kupelekea vijana wawili (maadui wa taifa) kutumbuliwa na mwenye nchi yake, inasemekana na kuonekana kabisa kuwa watumbuliwaji wameunda genge lao na kutuma vijana huku mitandaoni kwa lengo la kumpiga mkwara boss wao aliewatupa nje ya kazi zao.
Tumeshaona waliotumwa wamekuja na mikwara ya kwamba inawezekana vijana hao wakamkwamisha mwenye nchi huyo na namba 1 wa chama ktk kinyang'anyiro cha kumpitisha mgombea wa chama chao, pamoja na kile cha uraisi 😂😂😂
Ukweli ni kwamba hizo ni ndoto za alinacha kwa nchi ambayo mkuu wa nchi ndio mwenyekiti wa chama. Nikiwa na maana kwamba yeye ndio alifa na umega kuanzia kwenye chama na nchi, hivyo kumuangusha au kumuengua mtu wa aina hii ili asigombee uraisi kwa kujifanya eti wao ndio waliokulia kwenye chama ni kujidanganya wenyewe.
Nafikiri wote tunakumbuka Jinsi raisi na mwenyekiti wa chama aliepita hayati Dr John P. Magufuli alivyowapeleka puta vijana hao hadi kupelekea wengine kutambaa kutoka kwao hadi ikulu kuomba msamaha. Sasa itakuwa kwa huyu ambae ana baraka kubwa kutoka kwa baba wa chama (Kikwete) na support kubwa kutoka uraiani baada ya wananchi wengi kufurahia kutumbuliwa kwao!!
Narudia tena, Makamba na Nape hawana ujanja wala nguvu ya kupindua meza iliyopo ikulu iwe kiushawishi au kifedha. Wao watulie tu na kuwa waangaliaji wa mechi kama wengine walivyokuwa waangaliaji pindi wao walipokuwa bado wachezaji wa team ya mama.
Thanks kwa kunisoma.