Ukiwa nyumbani halafu huna kazi

Ukiwa nyumbani halafu huna kazi

Wengi mnaochangia hapa naona ni wale wa mjini...ukiwa kijijini kuna mikazi kibao hata hiyo nafasi ya kukaa ndani bila kazi unatoa wapi? Matokeo yake mzazi anaanza kukuonea huruma utasikia leo pumzika upike mboga ya kula tukirudi

Half kinachoniboa ni kuwa Kijana ukishafanikiwa kipesa, ndugu wanaanza kukupigia simu wakijifanya wanakujulia hali, kumbe ni unafiki mtupu, wakati kabla ya hapo walikuwa wanakulia buyu Khantwe
 
Hi
haya ni baadhi ya mambo yanayopelekea mtu kujikuta yupo nyumbani na hana kazi
1. kukosa mtaji wa kuanzisha biashara au huduma fulani
2. kukosa uwezo wa kufanya kazi za nguvu
3. kukosa ujuzi, mfikirie fom 6 liver ambae kakosa chuo
4. kukosa connection za kupachikana, kama zile za benki tela, loan ofisa au customer care
5. watu wenye stress huwa hawapendi kufanya kazi kwakuwa muda mwingi huwa ni watu wenye hasira hasira, mtu wa namna hii anapaswa kufanya biashara inayomwacha peke yake, kama vile kuuza duka na sio kumpa kipindi akafundishe darasani, atapiga mtu hadi aue.

so zipo sababu. cha muhimu ni watu wanaomzunguka mtu huyo kumshauri cha kufanya na kumpa sapoti ya kifedha ikibidi.
Hii namba tano mbona kama vile haileweki
 
Unajua mimi huwa napata wakati mgumu sana kumuelewa mtu pale anaposema eti amekaa nyumbani na hana kazi....!!??
Hii huwa inanipa wakati mgumu zaidi kutafakari kwamba, yaani huyu mtu anae kaa nyumbani kwanini hawezi kujishughulisha na chochote ambacho ni halal...??

Wewe wasema
 
Usiombe tena ukawa sio mtoto wa kuzaliwa kwenye hiyo familia unaambiwa mnanenepeana tu hapa mnakula maharage ya buree.Fance ya michongoma inakuhusu(Yamenikuta Haya) [emoji23] [emoji23]
 
Una amshwa wewe ufungulie mlevi mlango, unampa chakula, unampelekea maji ya kuoga, mke kalala tu wanasema jirani ni KKB (kula kulala bure} kumbe ni wewe.
 
Kama unaitwa Michael wanaanza kukuita Jamaa,

We jamaa
Uyu jamaa bado amelala
Uyu jamaa yupo wapi akanunue sukari
Uyu jamaa yupo wapi akajaze gas

Battery zikiisha kwenye remote utasikia huyu jamaa ameshaharibu remote
We jamaa
 
Mkuu, ikiwa wazazi wako walikupeleka shule na leo upo mtaani eti unalalamika kwamba hauna mtaji, basi jiweke kwenye kundi la vijana waliowatia hasara wazazi wao.
Naomba nijibu hoja zako kama ifuatavyo:-
1. Kukosa mtaji ni uzembe mkubwa na kimsingi hakuna mtu ambaye anaweza kupata mtaji kwa urahisi kama mnavyo dhania ndugu (nendeni mkabebe haya zege ama kuchimba mitaro ili mtaji upatikane)
2. Hakuna mtu mwenye anapenda kufanya kazi ngumu, na hasa vijana wengi wa kiTanzania ni wavivu wa kupindikua (vijana wa leo hawapendi kazi za mikono na wana madeko sana)
3. Sio wote wanao fanikiwa walipata ujuzi wa kazi za mikono. Na kukosa nafasi ya kujiunga ama kuchagukiwa chuo kikuu, hiyo haimaanishi kwamba basi ushindwe kuuza hata matunda mitaani ama kubrashi hata viatu.
4. Hakuna connection ambayo utaweza kuipata kama hauna mwenye atakushika mkono(hii isiwe kigezo kwa vijana na hasa ndipo hasa mnapaswa muanze kujipanga mapemza ikiwa unajua kwamba hauna connection).
5. Stress sio kitu kinacho kuja ghafla ndugu, kila jambo linahitaji utulivu na umakini ili kujikinga na mikwamo isiyo ya lazima kama kuwapa stress na desperation.
Noted!
 
Kuna siku nikasema town mpaka niwe na ramani maalum ndo naenda. Duh maza si akainasa hio, kila siku unasikia tu kuna wengine et town mpka wawe na ramani. Yan ikawa kama fimbo akisema m natulia kama maji mtungini.
 
Likija tangazo kwenye t.v. unaambiwa umebadili chaneli
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]daaah
 
unamwagiwa maji ya ukoko wa wali+utumbo wa samaki kwa maksudi

#arafu alie kumwagia anakwambia bahati mbaya ..lakini jitahidi upate kazi maana ungekuwa na kazi nisingekumwagia...[emoji849][emoji849][emoji849]
 
Back
Top Bottom