Ukiwa umebeba pesa nyingi fanya kila uwezalo Polisi wasijue

Ukiwa umebeba pesa nyingi fanya kila uwezalo Polisi wasijue

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Umeuza mazao yako, madini yako nyumba yako etc.

Fanya uwezalo hawa jamaa wasijue, usiniulize sababu.

Uzi tayari

32E41115-F33B-413B-BEC4-9AEFD386BE2E.jpeg
 
Hawa Jamaa ni zaidi ya majambazi..kuna mshikaji wangu anafanya biashara za minadani..Huwa wanasafiri pamoja na kama unavyojua wakirejea Toka masokoni Huwa na vibunda vya kutosha .anasema Huwa wakikutana na askari usiku hudanganya wanatoka msibani ,la sivyo mnageuzwa kitega uchumi
 
Umeuza mazao yako, madini yako nyumba yako etc.

Fanya uwezalo hawa jamaa wasijue, usiniulize sababu.

Uzi tayari

View attachment 2559375
Tanzania ukiwa na fedha nyingi chunga sana haya makundi 2 yasijue. 1. Majambazi 2. Polisi. Uko sahihi kabisa. Polisi kujua umebeba fedha nyingi ni hatari kwa maisha yako.
 
Tatizo wana pua za kunusa pesa kama paka na mnofu wa nyama.

Ni bora mara elfu ukutane na jambazi ukiwa na pesa maana anaweza zichukua akuachie uhai wako kuliko kukutana na jambazi polisi.

Polisi kwanza wanachukua pesa yako halafu wanakutia ndani kwa kesi ya kizushi kama vile haitoshi huwa wanaamini nyumbani utakuwa na pesa zaidi, hivyo wataenda kupekua kwako na kuadhibu waliowakuta.

Wakimaliza yote hayo wanakutundika kwenye dari ya mahabusu na huo ndio mwisho wako.

Ukiwa na pesa na kuona polisi ni bora hata ukimbilie mdomoni mwa mamba anaweza asikudhuru.
 
Hawa Jamaa ni zaidi ya majambazi..kuna mshikaji wangu anafanya biashara za minadani..Huwa wanasafiri pamoja na kama unavyojua wakirejea Toka masokoni Huwa na vibunda vya kutosha .anasema Huwa wakikutana na askari usiku hudanganya wanatoka msibani ,la sivyo mnageuzwa kitega uchumi
Uko sahihi. Tanzania tuna baadhi ya polisi vibaka na majambazi.
 
Back
Top Bottom