Gentlemen_
JF-Expert Member
- Nov 24, 2019
- 4,431
- 13,876
1- Hakikisha vitu vyako ulivyoacha ndani ya gari:
- USB flash, Charger, hela, na vitu vingine vidogovidogo ni vyema ukavitia ktk mfuko maalumu ukashuka navyo. Huwa si rahisi kubaini kama vimeibiwa kwa haraka mpaka utakapotoka eneo la tukio.
-Mtindo wa kubadiri vitu au kuiba kabisa hasa Carpets, jana nimeenda kuosha "Mkweche" wangu, wakati anarudishia Carpets hakuweka zote maana hii gari ina Carpets mbili mbili. Yeye akaweka moja moja zingine akasema hazikuwepo, alikuta hivyo. Na mimi sikubishana nae nikasema sawa nikaondoka.
-wengi wanapewa ORDER na watu kwamba nitafutie kitu fulani ambacho kiuhalisia madukani si rahisi kukipata au ni ghali sana, mfano kuna rubber zinazozuia vumbi matope etc ktk baadhi ya sehemu hasa nyuma ya gari huwa wanazichomoa, fuse mbalimbali etc kuna jamaa yangu aliacha gari kuosha akaenda kunywa pombe, walimbadirishia Control box, kurudi gari haiwaki (Baadae kule garage ndio wakagundua Control Box imechapwa)
Spika ndogo ndogo zinazokaa nyuma ya gari ktk baadhi ya magari huwa wanazibandua, wewe huwezi jua siku hiyo hiyo.
2- Kujifanya madereva wakiona gari kali, nzuri au imekaa mkao wa kipekee:-
Hii imenikuta hivi karibuni, nimeenda kuosha gari, akataka nimuachie funguo ya kuisogeza nikamuuliza unaiweza hii gari? Akaitikia ndio naiweza naendesha malori ije inishinde hii?. Kwa confidence yake mie nikamuachia funguo nikakaa pembeni. Baada ya kuosha nikasikia gari imewasha huku imekanyagiwa mafuta (Full Throttle). Akatia gia gari ikaruka na kuzima, bahati nzuri mbele kulikuwa na Tank ambalo halina maji so lile TANK lilisogezwa kwa umbali tu. Nikaenda kumuuliza imekuwaje? akasema alitak kwenda nyuma, badala aweke Reverse yeye akaweka gia namba 5. (Hii gari ni Manual ya 6 gears, na gearbox yake imegeuka sio ordinary) yeye kwa kukariri kwake akataka aniingize hasara.
Tuwe makini na hawa WAOSHA magari hasa ktk kipengele cha kusogeza gari.
3- Kutumia Pressure ya maji katika sehemu ambayo haina haja:-
Anaweka high pressure ktk sehemu sensitive kama ktk taa hasa upande wa nyuma kwenye waya, kama gari yako rangi yake imevimba kidogo atatia pressure hapo mpk rangi inabanduka. Yaan hawaangalii pakutumia high pressure na low pressure.
4- Kuosha Engine (INJINI) bila uangalifu:-
- Kuna magari ni very sensitive ktk maji, hasa haya ya umeme. Unakuta mtu anaenda kupigilia high pressure ktk engine bila tahadhari mwisho wa siku anakuletea faults zisizo na maana. Ni heri uoshe kwa mvuke au afute tu engine-bay yote.
5- Wanasoma Documents zako:
Nilifanya research fupi tu baada ya kufuta kitambulisho changu na kukificha nyuma ya siti pia nilikiweka katikati ya Documents zingine huku nikiziunganisha ndani ya bahasha, nilifanya maksudi.
Baadae wakati nimerudi home nikacheck zile Documents nikakuta zimewekwa ndivyo sivyo na ile ID imeshikwa shikwa inaonyesha Fingerprints. Nikajisemea hawa kumbe nikiacha vitu vyangu humu wanapekua pekua instead of kufanya wanachotakiwa kufanya.
Ni hayo tu, Je wewe ulikutana na Changamoto gani kwa hawa Waosha Magari?
Rejea:- Muosha Magari apatisha ajali gari lenye thamani zaidi ya Milioni 100. Akutwa anaruka sarakasi