Ukiwa umeenda kuosha gari zingatia haya

Baada ya wiki. Na hao ndio niliwapa waoshe na ndani. Siku hizi naweka kwenye glove box,nafunga siwapi funguo
Ndio inavyokuwa, ukiibiwa huwezi gundua hapo hapo.. pole aisee.
 
Muda mwingine Wateja mnatukwaza sana
Kuna Jamaa alileta Gari kuosha
Jamaa alikuwa na Milion 5 ndani ya Gari na aliziweka nyuma ya Seat alivyodai
Gari ilikuwa ni Hilux Pick up zile znazosambaza sigara,Dogo aliyeosha alitoa vitu vyote alivyovikuta kwenye Gari na kuosha Gari kisha kuvirudisha na kumkabidhi Gari
Jamaa aliondoka baada ya masaa 2 Jamaa alirudi Car Wash akiwa na Polisi anamuulizia Dogo aliyeosha Gari lake Dogo alikuwa katoka kaenda Shop nilimuuliza kuna Shida?
Jamaa alifoka sana akilalamika kuwa Dogo ameiba milion 5 zake mara Dogo akarudi kabla ya kuulizwa yule Polisi akamkunja Dogo Shati na kumwambia arudishe pesa alizochukua kwenye Gari
Dogo aliwaambia kuwa yy alitoa vitu vyote kwenye Gari na kuvirudisha Kama vp waende wakaangalie Kwenye gari walienda na waluikuta huo mfuko wenye Pesa ila Dogo aliuweka upande wa kushoto na mwenye Gari anadai yy aliuweka upande wa kulia kabla yakuja Car wash
Jamaa alianza kumsifia Dogo kuwa ni Mwaminifu na kutaka kuondoka
Mimi nilimshauri Azihesabu Pesa zake kabla ajaondoka kwel alizehesabu na kusema zmetimia pia
Nlimwambia siku nyngne awe makini na vitu vyake anapokwenda Car Wash.
 
Na kwa usumbufu aliowaletea je.. mlichukua hatua gani? Pia huyo police akili yake sio nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…