Jumanne Mwita
JF-Expert Member
- Nov 18, 2014
- 530
- 1,446
Changamoto inayowakumba wazazi wengi wanaotafuta elimu bora kwa watoto wao licha ya vipato vidogo.
Ndugu wanajamii, mimi ni mzazi naomba msaada wenu kupata shule bora na yenye gharama nafuu kwa mtoto wangu mwenye umri wa miaka 7 anayetarajia kuingia darasa la 4 mwakani lakini ninampango wa kumrudisha darasa la 3.
Maendeleo ya kitaaluma si ya kuridhisha. Nimegundua kwamba mwalimu mara nyingi hawana muda wa kumfundisha mtoto kwenye shule hizi za serikali, na mtoto akiona hivi kwamba ufuatiliaji shuleni si mzuri na wao wanaendekeza michezo sana matokeo yake mtoto anakuwa mjinga mjinga tu. Natamani kumpa mazingira bora ya elimu ili kufungua milango ya maarifa kwake, lakini kipato changu ni cha kawaida sana.
Naomba msaada katika mambo yafuatayo:
1. Shule gani bora na yenye gharama nafuu unayoijua naomba unisaidie kama unaijua kwa ambae uko hapa Katoro.
2. Kwa mtazamo wako, unachagua shule ya msingi kwa mtoto wako kwa kuzingatia mambo gani, zaidi ya performance ya kitaaluma?
3. Kwa hali kama yangu, unashauri nifanye nini ili kumsaidia mtoto wangu kupenda na kuelewa masomo zaidi?
Nimejaribu kuwasiliana na mwalimu wake mara kadhaa, lakini majibu huwa ni kwamba "tunaenda naye taratibu." Hata hivyo, najua mtoto ana uwezo, lakini mazingira anayosomea yanamkwamisha.
Naamini kwa pamoja tunaweza kusaidiana ili kujenga kizazi bora.
Maoni kutoka kwa wazazi wengine waliopitia changamoto kama zangu.