Habarini wapendwa, Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada, je gari ukiwa unaweka full tank na sio ya mafuta ya buku kumi kumi inapunguza ulaji wa mafuta?
Yaani kuna mtu kanishauri gari yangu niwe naweka full tank siku ikikaribia kuisha najaza tena eti nisiwe naweka ya buku kumikumi inakuwa inakunywa sana, je ni kweli?
Kwa wenye uelewa nielewesheni plz.
Namimi niweke mchango wangu kidogo hapa kwa maelezo rahisi kueleweka hasa kwa matu ambaye hajapita kwenye saiyansi
1. Mafuta kwenye chombo cha moto huhesabiwa kama mzigo hivyo ukiweka full tank maana yake umeweka mziko mkubwa
Hivyo wanapendekeza kama upo mjini uweke wastani wa nusu tank hivi li upate maleage nzuri ila kama upo nje ya mji ambapo vituo vya mafuta viko mbali weka tu full tank kwa kuwa tofauti ni ndogo sana
2. Ukitaka kupata maileage nzuri ( kutumia mafuta kidogo)
a. Usibebe mizigo au kuendesha huku umebeba vitu vizito ndani ya gari
b. Jaza tairi ziwe na upepo stahiki
c. Fanyia gari service kwa wakati
d. Usitumie Aircondition kama sio muhimu sana. ; unaweza kuvaa nguo nyepesi badala yake
e. Wakati unaendesha tumia gia sahihi; kwenda polepole sana mafuta huenda mengi ( mwendo mzuri ni km 60 hivi na 90)
f. mwisho epuka kukimbiza na kutumia tumia break mara kwa mara kwani huongeza ulaji wa mafuta badala yale, achia mafuta gari ipunguze mwendo yenyewe
Kwa kufanya hayo unapatapa matokeo mazuri na ikikupendeza unipe mrejesho