Kwa maswali yako haya inabidi kwanza nikupeleke VETA, maana umeuliza maswali ambayo kwa kweli uko mbali sana na ufahamu wa magari. Lakini ngoja nijaribu kukujibu;
1. Fuel consumption kwa gari husika huwa inakadiria gari ikiwa na mzigo wote inayopaswa kubeba?
Nimekuelewa. Good question. Sidhani, labda kwa gari za mizigo. Gari ya tani 7, wakisema fuel consumption ni 15l/100km ina make sense kwamba hiyo ndio consumption rate gari ikiwa na mzigo wa tani saba katika normal driving. Kwa gari ndogo za abiria mara nyingi consumption ni ukiwa dereva peke yako bila mzigo, kwa hiyo kwa kiasi fulani watakuwa wanadanganya.
2. Fuel consumption huwa inapigwa kwa kuzingatia hali zote za barabara wakati gari ikiwa na mzigo inayostahili kubeba?
Swali halieleweki
Lakini kama una maana fuel consumption inapimwaje, ni kwamba zile zinazoonyeshwa kwenye gari huwa unapewa wastani kwa driving ambayo hauko kwenye rough road na ya lami (normal driving). Kumbuka, kiwango kizuri cha kujua wastani wa fuel fuel consumption yako ni wakati uko spidi kati ya 80-100km/hr. Ukiendesha mwendo taratibu sana unakuwa unatumia gia kubwa na gari inakula mafuta zaidi. Ukiendesha kwa kasi sana, unapotita spidi ya 110km/hr injini inafanya kazi zaidi kwa hiyo inahitaji mafuta zaidi.
3. Ukiwa na tank la lita 10,000 katika umbali wa mita 3 toka ardhini, ukalijaza full, ukianza kutumia maji kutoka kwenye tank hilo, pressure ya maji wakati tank liko full na wakati liko nusu au robo ya mwisho kuisha inakuwa sawa?
Pressure inakuwa kubwa wakati tenki limejaa. Lakini hapa unaogolea flow ya maji kwa kutumia gravity. Gari hazipeleki mafuta kwenye injini kwa kutumia gravity, zinatumia fuel pump. Kwa hiyo hii theory yako hai-apply kwenye gari
4. Ukiwa na closed circuit tuseme ya maji ambayo iko pressurized kwa 3bar, ukaamua kutoa maji kwa kufungua point moja tu ya kutolea maji, maji yote yatatoka?
Hapa unaongelea juu ya flow effect ya atmospheric pressure na pressure head kwenye container. Ukiweka maji kwenye kopo ukatoboa tundu moja juu moja chini, maji yatatoka ikiwa matundu yote yako wazi. Ukiziba tundu la juu hayatatoka. Pressure head ikiwa sawa na atmospheric pressure kwenye tundu la chini asi maji hayatatoka. Sababu mojawapo ni kwamba unakuwa ume create vaccum juu ya maji ndani ya kopo. Ukiondoa kidole tundu la juu unaua effect ya vacuum, na pressure ya chini ya kopo ni atmospheric pressure + pressure head ya container, na maji yanaanza kutoka tena tundu la chini. Mfumo wa mafuta ya gari umetengenezwa kwa kutoruhusu kutengeneza vacuum mafuta yanapopungua.
5. Ni wakati gani pump ya mafuta ina effect kubwa zaidi kwenye uvutaji wa mafuta, full tank au half or one fourth of tank?
Effect ya pump ya mafuta iko vilevile, uwe na full tak au half tank. Iko calibrated kunyonya kiasi kile kile cha mafuta, na kama ikiathirika na mafuta kuwa nusu au full tank imeharibika, peleka gari gereji