Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Chochote unachokifanya huwa kina matokeo; matokeo yanaweza kuwa mazuri au mabaya. Itategemea na namna ulivyokipangilia. Pia kuna kitu nimejifunza, ukiwatendea watu wema ipo siku ule wema wako ulioutenda utakulipa.
Hasa, ukiwasaidia hawa watu:-
Hasa, ukiwasaidia hawa watu:-
- Watoto wasiokuwa na wazazi na wakapoteza tumaini la kuishi Labda walifiwa na wazazi au walitelekezwa; ukiwekeza rasilimali zako kwa hawa na wakafanikiwa, maisha yako yatakuwa mazuri na yenye baraka. Pale utakapokutana na changamoto, hawa watakuinua.
- Wale wasiokuwa na makazi, wanalala vichakani au mitaroni .
Pia kama utafanikiwa kuwainua na kuwabadilisha, na baadaye wakafanikiwa; utakuwa umeweka hazina ambayo ipo siku zitakurudia kwa kile ulichokiwekeza.
- Kuwasaidia wale wenye umasikini uliotukuka, kwa kuwaendeleza watoto wao kwa elimu au vipaji walivyonavyo.
Hawa watoto wakifanikiwa huwa wanarudi kushukuru, itategemea watakuwa kwenye nafasi ipi.