Ukiwasikiliza hawa watu kila mtu ana hoja ya msingi sana, shida huwa hatukubali kukubaliana katika kutofautiana

Ukiwasikiliza hawa watu kila mtu ana hoja ya msingi sana, shida huwa hatukubali kukubaliana katika kutofautiana

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Binadamu anapozaliwa huwa kakusudiwa aishi miaka mingi hata buku lakini harakati zake za maisha ndiyo huanza kuipunguza hiyo miaka taratibu au kwa mpigo!

Anyway! Tuachane na hilo turudi kwenye hoja ya hawa watu!

1. Wanandoa: Ukiwasikiliza wanandoa kwa makini vile wanazungumza umhimu wa ndoa, faida ya ndoa kiafya na kijamii hakika unaweza kutangaza ndoa siku hiyohiyo! Wanasimulia Mambo mengi ni mazuri mtupu; hakika wanahoja nyingi za msingi

2. Ukiwasikiliza wanawake: Ukaamua kutega sikio kuwasikiliza wanawake wanacholalamikia juu ya wanaume unaweza kuona kabisa wana hoja za msingi, ukisikiliza wanavyowasema wanaume kwa umalaya na uchepukaji unaona kabisa wanayo hoja kwa upande wao kama wanawake! Wako sahihi kabisa maana hawajui chochote juu ya kiwewe cha nyege za kiume!

3. Ukiwasikiliza wanaume: utazidi kuchanganyikiwa zaidi watakapokwambia mwanaume anawaza ngono mara nyingi zaidi kuliko mwanamke.

Hivyo ili alizike ni lazima awe na uhakika wa kusikilizwa na mwanamke muda wowote akihitaji!

Kutokana na kutafta uhakika huo, hutafta michepuko kama njia ya kujihakikishia ngono na msawazo wa akili; Mwanaume anayetulia na mwanamke mmoja huwa siyo asili yake kama siyo kulogwa basi atakuwa mcha Mungu sana!

Pia wanasema siku za kusubiri period ya mke zinatesa sana hisia ya Mme, siku za kusubiri baada ya kujifungua zinatesa pia! Marumbano ya ndani ya nyumba yanatesa pia! Kiufupi hawa Malaya ukiwasikiliza wanazo hoja nyingi sana kwa upande wao.

4. Ukiwasikiliza single mother: Hawa ukiwapa nafasi ya ukiwasikiliza utagundua wanatema hoja nyingi mhimu sana!

5. Ukiwasikiliza watoza kodi na watumia kodi: Hakika ukiwasikiliza wakusanya kodi na wala kodi wanavyomtaka mlipa kodi alipe utaona kama jambo ni jepesi sana.

6. Ukiwasikiliza walipa kodi wakilalamika kuhusu kodi unaweza ukaifuta siku hiyohiyo kama una mamlaka maana utaona wanavyoteseka.

7. Ukiwasikiliza wanaotetea mkataba wa bandari unaona wanayo hoja kwa upande wao ili mambo yasikwame kama yalivyopangwa.

8. Ukiwasikiliza wanaopinga mkataba wa bandari utaona kabisa wanaoukubali huo mkataba wana roho mbaya sana za kuuza nchi kwa faida ya matumbo yao!

HAKIKA MIJADALA MiNGI INAYOTUGOMBANISHA HUTEGEMEA SANA KILICHOPO KARIBU YETU!

Tujifunze kujua ni kwanini ili tuelewane.

1*whHK7suWlw-jWyuMoNKHwA.gif
 
Back
Top Bottom