PostGE2025 Ukiwauliza CHAUMMA na ACT - Wazalendo wanataka kuridhiana nini na CCM hawawezi kukwambia

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
"Unaita vyama vya brifcase unasema tunaweza kuendelea bila CHADEMA. Hivyo vyama si vilikuwa kwenye uchaguzi, Si vilisema uchaguzi ulikuwa huru na haki sasa vinaenda kuridhiana nao nini wakati wao walikubali kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki?"

M/Kiti CHADEMA
@HecheJohn
 
Swali ni lile lile kua CHADEMA wanataka maridhiano na CCM ya nini wakati awakushiriki uchaguzi na serikali awaitambui ingawa wanaitii.
Kumbe haujui hata maana ya maridhiano ingawa kuna mchangiaji mmoja ameweka vizuri japo kwa kiingereza.

Kutomtambua Rais ni kigezo tosha cha mgogoro kama sifa ya kuwa na maridhiano.

Lakini pia ukirejea ripoti ya Chande inaonyesha wazi kuwa miongoni mwa kauli zilizochochea mauaji ya Oktoba 29 ni kauli za hakuna nywinywinywi, Oktoba tunatiki dhidi ya no reform no election na Oktoba tunatoka ambazo zilinasibishwa na vyama vya CCM na CDM.

Kwa mantiki hiyo ni dhahiri pasi na shaka kuwa Maridhiano hayo ni ya pande mbili zenye wafuasi wengi ambapo hapa ndipo kundi kubwa la wananchi wanapoingilia.

Ama kudai kuwa maridhiano eti ni ya wananchi kwa kukwepa ukweli huu ni kujilisha upepo.

Ingawa wapo wanànchi wasio na vyama bado ni ukweli usiopingika kuwa pande hizi zinawakilisha maslahi ya wananchi wote kulingana na mahitaji yao ama ya kisiasa au kijamii hii ni kwa sababu maendeleo yoyote ya kijamii hutegemea siasa safi na uongozi bora ktk ardhi safi tuliyonayo na watu (nguvukazi kubwa vijana tulionao)
 
Vikao vya maridhiano vina pesa!
Hivyo tu!
 
Kwamba CHADEMA awamtambui Rais anaye iongoza nchi? Ilo lina madhara gani kwa wale walio tayari kumtambua na kumtii?
Unataka kusema kua kauli ya hakuna nywinywi ndiyo msingi wa uharifu ila unasahau KAULI ya kuvuruga uchaguzi,hamna kutiki,tutafanya uasi nk. Kwanini mnashindwa kusema ukweli ndugu?
 
Wewe unataka maridhiano ya nini wakati ukushiriki uchaguzi? Yaani mechi ya A na B refa aliipendelea timu B nawe ukaona isiwe tabu uchezi hiyo mechi ila leo unakuja na kusema kua ebu tujadiri na kuangalia mechi ya A na B ata kama sisi atukua kwenye mashindano...AAAh CHADEMA bhana.
 
Kama chawa hawakuelewa post hii. Basi kuna namna kichwani hakuko sawa.
 
Mwenye agenda ya maridhiano ndiye ajuaye wanachoridhiana, mwalikwa anatakiwa kusubiri maelekezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…