Kama hujaoa na unayemwomba hutaki kumwoa usimg'ang'anie na kumfuata unamuomba yeye tu kila siku maana atakuumiza kisaikolojia. Kimsingi hii ni kama business, mteja huyu akigoma ukikaa naye muda mrefu atakupotezea muda na nguvu zako pia. Jaribu kufikiri kama ingetokea mmachinga akikung'ang'ania siku nzima wewe akuuzie suruali hata ikija kutokea umenunua kwani unanunua nguo zake zote?, utanunua suruali ama shati moja basi, atakuwa amepoteza muda mrefu kwa faida ndogo kupita kiasi. Kwahiyo ukimwomba mara mbili tatu hataki songa mbele uokoe muda wako na nguvu kidogo ulizonazo, vinginevyo una muda na nguvu za kuchezea. Unaomba miezi sita kitu ya kutumia nusu saa au lisaa? Unaomba miezi sita wakati ukipewa unayepoteza nguvu ni wewe? Unaomba miezi sita wakati hujui unachokiomba kikoje? Wakati wote huo wa miezi sita unapoomba umasikini unaongezeka maana unatumia hela kuomba na hufanyi kazi vizuri maana akili imeshikwa, ukija kupewa ndio unatakiwa ugharamie zaidi??????? Huo ni upunguani... nikupe mbinu rahisi. 1 - Oa, 2 - omba muda mfupi, hujapewa songa mbele atayekupa huenda hata akaipa akili yako nguvu ya kufikiri kwa haraka zaidi.