Ukizuia upinzani wa kidemokrasia unakaribisha upinzani wa kiharamia

Ukizuia upinzani wa kidemokrasia unakaribisha upinzani wa kiharamia

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2020
Posts
5,146
Reaction score
15,927
Katika miaka karibu 24 ambayo Mwalimu Nyerere alikua kiongozi wa Tanganyika na baadaye Tanzania, kulikua na majaribio matatu ya kupindua serikali.

Wakati huo hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuiondoa serikali madarakani, kwakuwa nchi ilikua na chama kimoja tu kilichojipa uhalali wa kuongoza nchi, na yeye Nyerere ndiye aliyekua kiongozi wa chama hicho na kiongozi wa serikali yake.

Moja ya faida za demokrasia ni kuwapa njia halali na ya amani wale wote wanaopingana na sera za serikali iliyopo madarakani kujaribu kuiondoa serikali hiyo madarakani kupitia kura za wananchi.

Madhara ya kuminya demokrasia na uhuru wa watu ni kuwajengea hisia wapinzani wote wa serikali kuwa njia hizi za kidemokrasia na amani haziwezi kufanya kazi kwenye nchi yao, na hivyo basi polepole, hatua kwa hatua unaishia kutengeneza makundi hatari yatakayo amua kutumia njia mbadala kuiondoa serikali madarakani.

Mambo haya huwa yanatokea taratibu sana, na watu wengi kwa upumbavu wao na uroho wa madaraka huwa wanapuuzia mpaka pale hali inapokuwa mbaya.

Mlio karibu na watawala washaurini, hii njia waliyoanza kupita tangu 2015 siyo sahihi. Baada ya JPM kufariki wengi tulitegemea sasa serikali itarudi kwenye mstari, lakini naona kuna kila dalili za upuuzi uleule kuendelea.
 
Back
Top Bottom