Uko tayari? Dar es Salaam mpya inakuja. Serikali kutwaa eneo la mita za mraba 233,000. Maeneo ya Sinza, jirani na Mlimani City, Boko, SIMU2000 kuguswa

Uko tayari? Dar es Salaam mpya inakuja. Serikali kutwaa eneo la mita za mraba 233,000. Maeneo ya Sinza, jirani na Mlimani City, Boko, SIMU2000 kuguswa

Dar inapangwa upya, Sinza inasukwa upya, maeneo jirani na Mlimani City yanasukwa upya. Serikali inaenda kutwaa eneo la ukubwa wa mita za mraba 233,000 na kulipanga upya.

Maeneo kama Sinza yana viwanja vya 20/20, na maeneo hayo kwa sasa ndio ujenzi mkubwa wa maghorofa unakuja. Ni vyema serikali imeyatwaa maeneo hayo ili iyamiliki, ifute ramani ya eneo hilo, ifidie, kisha ilipange upya, na kugawa viwanja vikubwa kwa uwekezaji mkubwa.

Kama ujenzi ungeendelea kwa hali ilivyo, maeneo hayo yangekuwa hayana mvuto, na yenye msongamano.

Hii iende mpaka Tandale kwa awamu, tuipate Dar tunayoitaka.

View attachment 3171283

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI:

View attachment 3171960
Kazi nzuri ya Rais Samia hiyo ,lazima aweke alama ambayo inaweza isifikiwe na yeyote baadae.
 
Ayo maeneo serikali inataka kuweka karakana ya mwendokasi pale mbuyuni na mji mpya wa mashimoni, na pale boko basihaya wanaweka stendi kuu ya mwendokasi
Hata namshangaa huyo anaeleza utadhani serikali imesema inaubadilisha makazi ya Dar, wakati lengo ni kujenga vituo vya BRT tu.
 
MWENDOKASI - DART KUTWAA MAENEO YA KAWE MBUYUNI KWA AJILI YA KARAKANA

Bosi wa Mwendokasi DART afika eneo la Mecco Kawe Dar es Salaam kuangalia maeneo

View: https://m.youtube.com/watch?v=29SjgPwnpPw

Viongozi wakiwemo Mkuu wa wilaya DC, mbunge askofu Dkt. Josephat Gwajima na kigogo wa DART Dkt. Athumani Kihamia wafika eneo la mradi wa DART Kawe mtaa wa Mbuyuni kwa Amani...

Wananchi wastuka wapinga michoro ..inaingia maeneo yaliyo nje ya ramani..
 
Back
Top Bottom