Ukokotoaji wa bei ya petroli kwa mwezi June baada ya ruzuku ya Sh 100 billion huu hapa: Bei inapaswa kupungua kwa zaidi ya asilimia 60%

Hivi pale bungeni, kuna mbunge ambaye hua anajishughulisha na kutumia calculator kweli?
 
Hiyo billion 100 ni kwa mwezi June tu. Kasikilize vizuri maamuzi ya mama yaliyosomwa na Makamba bungeni wiki 2 zilizopita. Kuanzia Julai bunge la bajeti litaweka utaratibu wa kuendelea wa kudhibiti bei ya bidhaa hii ya mafuta.
 
Waweza kunitafsiria kwa kiswahili tafadhali? Mie wakati nasoma Hizi Feza boys na St. Mtakatifu schools zilikuwa hazijaanza.
Kwani na wewe ni mbunge?
 
Hivi kwenye hili bunge la sasa kuna hata mmoja anayeweza kuelewa hayo mahesabu yako?!!!
 
Huijui serikali
 
Hizi makitu ni kama zile makitu wanafanya motivation/Inspiration speakers....

Mtu anamiliki 5 star Hotel akiwa kaanza na mtaji wa punje mbili za mchele....
😁😅🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Solution ya kudumu? Ila watu mna Imani sana na serikali zetu hizi
Kwenye biashara ya mafuta huko ndio wafadhili na viongozi wa serikali walipojaa. Alafu tena haohao waje na solution ya kudumu ya kupunguza bei?
Kwenye mafuta ndio sehemu wanapopatia pesa maana ndio kwenye mzunguko mkubwa wa pesa. Kwa mwezi tu mafuta yanauzwa hapa nchini ni zaidi ya tril 1.2
 
Hiyo billion 100 ni kwa mwezi June tu. Kasikilize vizuri maamuzi ya mama yaliyosomwa na Makamba bungeni wiki 2 zilizopita. Kuanzia Julai bunge la bajeti litaweka utaratibu wa kuendelea wa kudhibiti bei ya bidhaa hii ya mafuta.
Ubavu wa kudhibiti bei hana, ili uongoze vizuri ni lazima uwakubalie wale jamaa wafaidike.
 
Hivi kwenye hili bunge la sasa kuna hata mmoja anayeweza kuelewa hayo mahesabu yako?!!!
Wapo wengi tu kwani hizi ni hesabu nyepesi tu ambazo hata Dr Msukuma kule bungeni anaweza kuzielewa vizuri.
 
Una uhakika hizo hesabu ulizosoma na Dr Mwigulu alisoma kama hizo?
 
imekokotoa Vizuri mahesabu yako , je matumizi ya mapipa 18,000 Kwa siku umefanyia utafiti au kuna takwimu rasmi?
 
Wametoa ruzuku sio wamepunguza makato
 
imekokotoa Vizuri mahesabu yako , je matumizi ya mapipa 18,000 Kwa siku umefanyia utafiti au kuna takwimu rasmi?
Hata kwenye Google zinapatikana. Tanzania National Statistics Beural wanapaswa kuwa nazo. Hata pale TPA (bandarini) na TEKOHAMA kwa Waziri Nape. Kwenye wizara ya Makamba wanazijua vizuri etc etc.

Tatizo huwa zinafichwa fichwa. Sijui ni kwa sababu ya masilahi ya nani. Wabunge wetu wanapaswa kushinikiza serikali iwapatie takwimu hizo na wazihakiki kwani wanaweza kutoa za uwongo.

Google wanaonesha kwamba matumizi yetu kwa siku yana range kuanzia barrels 15,000 hadi 20,000 na wastani ni huo wa barrels 18,000 kwa siku.
 
Bila aibu kuna wabunge walishauri serikali iachane na uagizaji wa mafuta wa pamoja chini ya TPDC wakidai eti italeta unafuu huku wakiwa wanatumiwa kama mawakala na wafanyabiashara ili wapige pesa!
 
Hiyo takwimu ya Sh 1.2 trillion kwa mwezi umeipata wapi? Ni mapipa mangapi kwa mwezi? Isije ikawa ni takwimu kutoka kwa wapigaji wetu kwa masilahi ya matumbo yao. Kwani takwimu hiyo inatupa bei ya lita moja kuwa mara sita ya bei ya sasa, tukikokotoa kwa kutumia takwimu hiyo!
 
Tatizo ni kwamba wajanja wataichakachua hiyo bilioni 100!! Watakuja na hadithi za ajabu ajabu!! Huyo pre-february haaminiki hata kidogo!!
 
Wametoa ruzuku sio wamepunguza makato
Hiyo ni ruzuku kama ile ya mbolea aliyoiomba waziri Bashe. Tatizo ruzuku hiyo itapewa mawakala (middle men) binafsi wanaotuagizia bidhaa hiyo kutoka nje badala ya kuiagiza wenyewe kwa kutumia TPDC yetu ambayo ndiyo ingalipatiwa hiyo ruzuku.
 
Weka summary in short how much will it be in retail then kwa Dsm na Moro
 
Una uhakika hizo hesabu ulizosoma na Dr Mwigulu alisoma kama hizo?
Sijui huyo Dr Mwigulu na Makamba walisoma hisabati au walikimbia hisabati walipokuwa shule. Hata kama hesabu hizi nyepesi za ukokotoaji watazielewa wakizisoma hapa, bado wanaweza kuzipotosha kwa sababu zao binafsi. Ndiyo maana nimewatadharisha wabunge wetu wasije wakadanganywa na tukakosa hiyo nafuu kubwa ya bei ya mafuta ambayo rais wetu katupatia ruzuku ya TSh 100 billion kwa mwezi June pekee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…