Hayo matumizi ya lita 10,900,000 kwa siku umeipata wapi kwani hata kwenye hizo takwimu za Makamba ulizozinukuu hazimo!
Makamba anazungumzia lita za mafuta zinazoshushwa bandarini na kuhifadhiwa kwenye maghala. Tunajua kuwa baadhi ya mafuta hayo yataelekea nchi zingine jirani (yako transit). Hatupi mchanganuo wake ili kutuchanganya.
Kuna mahali anasema tuna lita 118,594,024 zitakazotusheleza kwa mwezi mmoja. Ukikokotoa hii unapata lita 3,933,000 kwa siku. Wewe unasema lita 10,900,000 kwa siku.
Kuna mahala pengine anasema kutakuwa na lita 202,742,704 ambazo zitatosha siku 33. Ukikokotoa hii maana yake ni lita 6,143,718 kwa siku. Sasa hii tofauti kubwa inatoka wapi? Yaani mwezi uliopita matumizi kwa siku yalikuwa lita 3,933,300 lakini mwezi ujao yatakuwa lita 6,143,718 kwa siku. Haya ndiyo mahesabu ya Makamba uliyotuletea hapa. Halafu na wewe ukayaongeza hadi kuwa lita 10,900,000 kwa siku.
Takwimu zilizoko Google ni sahihi kwamba matumizi yetu kwa siku ni barrels 15,000 (= lita 2,285,000) hadi barrels 20,000 (= lita 3,180,000). Wastani ni barrels 18,000 kwa siku sawa na lita 2,862,000 nilizozitumia kufanya ukokotoaji. Hata ukitumia hiyo ya Makamba ya lita 3,933,300 kwa siku bei ya lita moja haitazidi Sh 1,600 kwenye retailers.