Ukoloni mamboleo unaitafuna Kenya

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wakoloni hawajawahi kuondoka Kenya hata baada ya kupata Uhuru.

Wakoloni waliacha watu wao na mali zao Kenya kitu ambacho kinailazimisha Kenya kuvilinda kwa gharama yoyote wakati wote kwakutumia jeshi, sera, sheria na utamaduni.

Hii inawafanya viongozi wa Kenya wasiweze kukifanya kile wanachokifanya viongozi wengine Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Ndio maana Kenya lazima wasiende mbali sana na utawala wa sheria na demokrasia kwa lazima hata kama hawataki. Vyombo vya usalama vya Kenya, sera, sheria na tamaduni zao lazima zilinde Ardhi, mashamba, makazi, viwanda, biashara, taratibu na desturi za wakoloni na wawekezaji wazungu. Hali inayoifanya Kenya iishi kwa kutarajia kupewa misaada na uwekezaji kutoka kwa wazungu. Roho ya Kenya iko kwenye misaada kutoka ng'ambo.

Kwa juujuu na harakaharaka watu wanaweza kuona kana kwamba Kenya kuna utawala wa sheria na demokrasia kuliko mataifa mengine, lakini wanafanya hivyo bila kupenda. Ndiyo maana ni rahisi sana kusikia migomo mingi ya wafanyakazi, wabunge na wanafunzi Kenya wakiidai nchi yao vitu na mishahara ambayo nchi haiwezi kugharamia lakini wanalazimika kuwatimizia ili Kenya isikike vizuri kwenye masikio ya wazungu . Ni rahisi pia kusikia uchaguzi Kenya eti umefutwa na mahakama kitu ambacho hakiwezekani kwenye mataifa mengine ya Afrika Mashariki. Hebu madaktari, wabunge au wanafunzi wa tanzania, uganda, rwanda, burundi, ethiopia wagome waone cha mtema kuni. Huwezi kumkamua ng'ombe asiye na maziwa.

Kama Kenya ikinyimwa msaada kutoka kwa wazungu au wachina haiwezi kusimama hata kwa mwaka mmoja. Hii vicious cycle ni mpaka lini? Nini atakaja kusema wewe mzungu rudisha ardhi kidogo ili tuwape wakenya nao walime mahindi na mananasi kidogo? Ni nani atakuja kusema wakikuyu hivyo mlivyofanya havikubaliki?

Kenya ni taifa ambalo linahitaji ukombozi upya dhidi ya wazungu.
 
Magufulistan people. The same song since 1964 " kenya kuna ukoloni mambo leo" .. ujamaa commie low iq nonsense.
Fumba macho yako kisha fikiria ni ardhi kiasi gani iko bado mikononi mwa wazungu wachache in terms of plantations, ranches, settlements, religious, hotels, garages, yards, recreations, business.
 
Magufulistan people. The same song since 1964 " kenya kuna ukoloni mambo leo" .. ujamaa commie low iq nonsense.
Kuna mada zingine ukimaliza kuzisoma huwa unahisi ni kama IQ yako imeshuka ghafla hadi kwenye level ya Burukenge. Mtu anasema na confidence kwamba demokrasia na matokeo ya uchaguzi kufutwa nchini Kenya ni kwasababu ya ukoloni mamboleo. Nyerere aliwasex kiakili kweli kweli hawa majirani na ule mfumo wake uliofeli wa ujamaa. Jiwe naye amekuja kamalizia 'kazi nzuri' ya Mwalimu.
 
Magufulistan people. The same song since 1964 " kenya kuna ukoloni mambo leo" .. ujamaa commie low iq nonsense.

The high IQ people who failed to solve trivial issues like police brutality, nepotism and tribalism. Mnahangaika na bbq or sorry bbi.
Akili kubwa ambao, their people's hearts bleed because of prevalent of historical Injustice.
 
Kenya viongozi walipelekwa the Hegue kwasababu gani? Mbona Tanzania, Uganda, Sudani kusini, Somalia, Ethiopia, DRC, Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, nk kuna mauaji lakini viongozi wa nchi hawajapelekwa huko?

Hivi nchi kama Kenya ina pesa ya kurudia uchaguzi wakati watu hawana chakula wala vifaatiba hospitalini? Kwetu Kenya bhana mhimili wa mahakama una nguvu kwasababu ya kulinda maslahi ya wakoloni wetu. Kama watu wakipigana itaharibu mali nyingi za walowezi na wageni.
 
The high IQ people who failed to solve trivial issues like police brutality, nepotism and tribalism. Mnahangaika na bbq or sorry bbi.
Akili kubwa ambao, their people's hearts bleed because of prevalent of historical Injustice.
Their high IQ makes them speak English with their own mothers. The colonial language.
 
The high IQ people who failed to solve trivial issues like police brutality, nepotism and tribalism. Mnahangaika na bbq or sorry bbi.
Akili kubwa ambao, their people's hearts bleed because of prevalent of historical Injustice.
BBI; whose idea is this? BBI is all about fear of not protecting investors' properties and missing Aids.
 
Ile ngazi waliyoitumia wazungu kupandia juu waliko kiuchumi wameiondoa na kuificha na pengine wameichoma moto kabisa.

Kiuchumi wazungu walifika pale walipo kwa kufunja haki za binadamu na kwa kukanyaga sheria na demokrasia. Walikusanya mitaji ya uwekezaji kwa kutumia njia zisizokubalika kama vile kupora makoloni, kufanyakazi kwa masaa mengi bila kujali umri kwa ujira mdogo, walitumia watumwa bure na kukanyaga demokrasia na usalama pahala pa kazi. Hawakuwa na malipo ya ajali kazini au pension.

Walipohakikisha kuwa wao tayari wana uhakika wa mitaji na masoko duniani wakatulazimisha sisi wadogo kabisa tujali haki za binadamu, demokrasia, usalama kazini, malipo ya ajali kazini, uhuru wa kuabudu, mifuko ya kijamii ya pension, kulipia huduma za kijamii kama shule, hospitali, maji, nk.

Nchi zetu hizi changa haziwezi kupiga hatua kimaendeleo kama zitakumbatia uhuru wa sheria, democrasia, usalama kazini, utunzaji wa mazingira, haki za binadamu, uhuru wa kuandamana, vyama vingi, uchaguzi kila miaka 5, nk. Tutatumia muda na rasilimali nyingi sana Afrika kuhangaikia mambo hayo.

Nchi kama za China, N Korea, Asia ya kati, Asia ya mbali, Rwanda, nk zinapiga hatua kiuchumi kwa kuachana na mambo ya haki za binadamu, utawala wa sheria, democrasia, nk. China ina watu zaidi ya 1 bn, kama wakiruhusu demokrasia haitatawalika na watashindwa kuwalisha.

Kenya ni taifa dogo sana, demokrasia, sheria, haki za binadamu, malipo halali kwa wafanyakazi, nk ni ghali sana to undertake kwenye ulimwengu ambao masoko yote yanadhibitiwa na wazungu. Utapata wapi fedha za kuendeshea mfumo wa vyama vingi, sheria, bunge, na serikali?

Jaji anasema uchaguzi ufutwe maana yake taifa litumie hela na muda tena kurudia uchaguzi huku wananchi hawana maji, umeme, madawati shuleni, chakula, madawa, barabara, madawati. Hatuwezi kuendelea milele, na hii sio kwa bahati mbaya bali tulitegeshewa na wakoloni ili tusiende mbele.
 
Mla mirungi anadhani ana high iq
 
The most stupid commentary I have read this year, ujinga mtupu, hizi ni stories za abunwasi😂😂
 
Just shut up uar not making sense 😵
 
Kenya is far better from Tanzania in terms of development and other fields that's why they are not proud of small things like interchange or flyovers while they got them more than 10 years ago
Kenyan president hawezi kwenda kupinga picha kwenye flyover au kuacha shughuli Zake kwenda kupokea ndege
Twende Nairobi halafu angalia Dodoma utapata majibu
 
heri ukae kimya.hakuna unachojua.
 
Mkuu mimi najua Nairobi vizuri
Wazungu mkiwaita Tanzania mnawaita wawekezaji lakini wakiwekeza Kenya mnawaita wakaloni
Hao hao wakileta msaada mnawaita wahisani
Wakiuliza msaada wao umetumika vipi mnawaita mabeberu
Ndumilakuwili
tushikane hapo kwenye uhuru kutozindua barabara na majengo.au umeshtuka[emoji23][emoji23][emoji23].

kwani hata umesahau pesa ni moja ila ina majina kibao kutokana na mahali inapotolewa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…