kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Wakoloni hawajawahi kuondoka Kenya hata baada ya kupata Uhuru.
Wakoloni waliacha watu wao na mali zao Kenya kitu ambacho kinailazimisha Kenya kuvilinda kwa gharama yoyote wakati wote kwakutumia jeshi, sera, sheria na utamaduni.
Hii inawafanya viongozi wa Kenya wasiweze kukifanya kile wanachokifanya viongozi wengine Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Ndio maana Kenya lazima wasiende mbali sana na utawala wa sheria na demokrasia kwa lazima hata kama hawataki. Vyombo vya usalama vya Kenya, sera, sheria na tamaduni zao lazima zilinde Ardhi, mashamba, makazi, viwanda, biashara, taratibu na desturi za wakoloni na wawekezaji wazungu. Hali inayoifanya Kenya iishi kwa kutarajia kupewa misaada na uwekezaji kutoka kwa wazungu. Roho ya Kenya iko kwenye misaada kutoka ng'ambo.
Kwa juujuu na harakaharaka watu wanaweza kuona kana kwamba Kenya kuna utawala wa sheria na demokrasia kuliko mataifa mengine, lakini wanafanya hivyo bila kupenda. Ndiyo maana ni rahisi sana kusikia migomo mingi ya wafanyakazi, wabunge na wanafunzi Kenya wakiidai nchi yao vitu na mishahara ambayo nchi haiwezi kugharamia lakini wanalazimika kuwatimizia ili Kenya isikike vizuri kwenye masikio ya wazungu . Ni rahisi pia kusikia uchaguzi Kenya eti umefutwa na mahakama kitu ambacho hakiwezekani kwenye mataifa mengine ya Afrika Mashariki. Hebu madaktari, wabunge au wanafunzi wa tanzania, uganda, rwanda, burundi, ethiopia wagome waone cha mtema kuni. Huwezi kumkamua ng'ombe asiye na maziwa.
Kama Kenya ikinyimwa msaada kutoka kwa wazungu au wachina haiwezi kusimama hata kwa mwaka mmoja. Hii vicious cycle ni mpaka lini? Nini atakaja kusema wewe mzungu rudisha ardhi kidogo ili tuwape wakenya nao walime mahindi na mananasi kidogo? Ni nani atakuja kusema wakikuyu hivyo mlivyofanya havikubaliki?
Kenya ni taifa ambalo linahitaji ukombozi upya dhidi ya wazungu.