Ukoloni unavyozidi kuwaangamiza Waafrika kwenye nchi zao

Ukoloni unavyozidi kuwaangamiza Waafrika kwenye nchi zao

MWANAHARAKATI MWEMA

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2022
Posts
216
Reaction score
313
Kwanza Namshukuru' mwenyezi Mungu mwingi Rekhma kunifikisha siku ya Leo, pia nawaombea wote wanaochukia uzembe, wizi, ubabaishaji na unyumbu.

Moja ya maswali ninayojiuliza kila siku ni kwamba kama miaka ya 1500 wazungu waliizunguka dunia kutafuta fursa, sisi ngozi nyeusi hasa watanzania mhitimu WA digree anaamini Kwa elimu yake hastahiki kuteseka kusafiri Kwa basi kurudi kijijini kwao au Kijiji Jirani kutafuta shamba kuifanyia Kazi elimu yake Karne hii ya 21.

Wazungu ambao Kwa wakati huo walisafiri katika mazingira magumu sana lakini walipambana Kwa kuwa waliongozwa na Nia na uzalendo WA nchi zao,lakini mtanzania huyu ambaye msomi Leo anapata digree ya maghumashi anakalia kiti cha ofisi,ndiye anayekubali kumsaidia mzungu kubeba rasilimali za nchi yake na kusindikiza Kwa mtutu WA bunduki.

Mzungu amemfanya mwafrika kama Choo,mwafrika anamfanya mzungu kama mungu,ndio wametutawala lakini Kwanini hatuukatai utumwa Kwa matendo Kwa kuamua kwamba kitu chetu kitatengenezwa na Sisi wenyewe hata kama kitaonekana hakina ufanisi lakini ndio itakufanya uje na aina ya ujuzi mzuri Zaidi ya uliopita Hili nalo linaonekana Shida tumelogwa na Nani?

Viongozi WA kiafrika wanadhani kukopa na kutengeneza miundombinu Ni Vibaya! 'Hapana' Shida inakuja kuwa endapo TU, technology iliyotumika kwenye Kazi husika haitotoa "WAHITIMU" lengo mama.

Wazungu ndio wanunuzi wakubwa low material nyingi kutoka africa, Ila waafrika ndio dampo na soko kuu la by product za viwanda vya ulaya tuamke tujifunze kufanya Kazi na kujituma, ukishapata mtu anaekulemaza Kwa kukufanya uwe teketeke na kupenda vya bule na kuomba mkatae na ukipata baba anaekukomaza na kukufunza kujitegemea na kupambania chako mshukuru' mungu.

Waafrika tushtuke wazungu,wachina,wajapani,wahindi nk: hawawezi kukupa fulsa katika nchi zao uwe kama wao nchini mwetu,nyie hamjiulizi tajili Namba moja Hadi Kumi wote ni¥¢€£¢€¥π√× nyie Ni wasindikizaji Kwa Sababu ya kuamini WAGENI kuwapuuza wazawa.


Kwaherini jumatatu njema.
 
Black race inaogopeka ulimwenguni kote kwakuwa ithibati za kisayansi zinathibitisha ndio chanzo cha uhai ukuu ustaarabu nk.. Zinafanyika juhudi nyingi kukizima hiki kizazi lakini bado hawajafanikiwa
 
Black race inaogopeka ulimwenguni kote kwakuwa ithibati za kisayansi zinathibitisha ndio chanzo cha uhai ukuu ustaarabu nk.. Zinafanyika juhudi nyingi kukizima hiki kizazi lakini bado hawajafanikiwa
Mna jizima wenyewe kutokana na ubinafsi,chuki, na ujinga ulio kithiri.
 
Back
Top Bottom