Ukoma wa Dodoma unavyoliathiri Taifa

Ukoma wa Dodoma unavyoliathiri Taifa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Yaani mji mzima umejaa wakoma na upofu, halafu haya ndio makao makuu ya nchi.

Hii taswira inafikirisha sana, sijui kwanini walichagua mahali penye laana ya ukoma na upofu ndio pawe makao makuu ya nchi?

Matokeo yake uchumi wetu una ukoma, soka letu lina ukoma, maendeleo yetu yana ukoma, miradi yetu tuliuoiita miradi mikubwa ya kimkakati imejaa ukoma, sio wa treni ya mwendokasi, wala sio bwawa la kuzalisha umeme kule Rufiji tulikokata zaidi ya miti milioni mbili, kote kumejaa ukoma.

Sasa tunafikiria kwamba tozo zinaweza kutuponya na ukoma, huku ni kujidanganya.
 
Ukoma wa nchi hii si kwa sababu ya Dodoma, umoka wa nchi hii unatokana na upofu wa kifikira wa watawala tangu enzi ya Mwalimu.

Tukifanikiwa kubadili jamii yetu kutoka kwenye upofu wa fikra ni dhahiri tunakuwa tumekomboa taifa hili kutoka kwenye ukoma kiuchumi!!
 
Ardhi ya Dodoma inahitaji tiba
Malisa njoo uiponye nchi
Screenshot_20220905-141527_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom