Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ambaye Wachambuzi wanamueleza kama ndiye bingwa wa siasa za Kisasa kwenye Ukanda wa eneo la Maziwa Makuu, Anashangaza sana!
Pamoja na kushambuliwa, Kudhalilishwa na kutukanwa hata Matusi ya nguoni, tena wakati mwingine anatukanwa na watu ambao amewakuza na kuwalea kisiasa na kimaisha, Lakini hakuwahi kuwajibu, Kulipa kisasi wala hata kupambana nao, mara zote amekuwa kama Kaka Mkubwa au kama Mzazi, ambaye anaamini kwamba Mtoto akinyea mkono basi usiukate, chukua maji na sabuni uoshe utatakata tu .
Nikiwa kama Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa kimataifa na Mbobevu wa siasa za Tanzania nimempigia simu Mwamba huyu na kumuuliza kwanini asiitishe Press ili kufafanua Tuhuma na matusi dhidi yake kutoka kona mbalimbali, ambayo inaonekana kama yanamchafua?
Kwanza alinijibu kwa ufupi kwamba NO COMMENT, hapa alilenga kunikatisha niishie hapo na nisiendelee tena kumuuliza chochote kuhusu hilo, lakini nilipombana sana Mwamba huyo alisema kwamba hatojibu hoja ambazo zinahusu, kashfa, Matusi kwake binafsi, na kwa kadri ya kumbukumbu zake matusi na kashfa dhidi yake ni nyingi mno na isingekuwa rahisi kuzijibu na wala hazina tija yoyote, Na kwamba yuko tayari kujibu maswala yote yanayohusu Chadema na mipango yake.
Sasa kwa vile hoja zangu zilihusu Mashambulizi anayoyapata yeye binafsi, na wala haikuwa masuala ya Chadema kama Chama ikabidi niishie hapo .
Swali langu ni hili, Mtu huyu ana Moyo wa aina gani kiasi cha kuvumilia mambo haya?
Pia soma: