Ukombozi wa nchi unahitaji watu waliodhamiria

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mchakato wa kuitoa nchi katika hatua moja duni kwenda katika hatua nyingine bora zaidi kwa jina la ukombozi, unahitaji watu waliodhamiria kweli kweli.

Jukumu hili haliwezi kuwa la kila mtu. Nyuso za watu hawa, maneno, (nyuzi, posts) na matendo yao hujionyesha.

Inawezekana namna gani kuwasikia Nyerere, Museveni, Kagame, Sokoine, Putin, Mandela, Lissu, Mbowe, Mangula, Mtikila, Seif, Malema, Garang, Saddam, Milosevic, Thatcher, Gadaffi, XI, Mengistu, Mugabe, Rawlings, Gandhi, Castro, Obama, Kim na wa namna hiyo wakiwa carried kwenye mizaha au hadithi za mbususu, simba na yanga, man city na man u, vumbi la congo na ya namna hiyo?

Pana haja ya kukatumia ka litmus haka ka kupima kudhamiria, kuwaengua wengine kwenye harakati hizi ili kutosumbuka na kupoteza muda na watu wasiojitambua.

IMG_20221001_234759_452.jpg

Kuikataa mikono yenye damu hakuwezi kuwa nusu nusu.

"Mtu hawezi kuwa mguu mmoja ndani na mwingine nje."

Ukombozi hauhitaji watu wengi. Wasanii na waachwe kuendelea na usanii wao kwa raha zao.

Ukombozi hawezi kuachiwa Mungu kutuletea bila ya sisi kuchukua hatua za makusudi.

IMG_20220927_190940_421.jpg

Ni heri kuwa na watu wachache waliodhamiria kuliko kuwa na lundo la waoga, wajinga, wapumbavu au wasaka fursa.

Ni vyema kujipima mwenyewe kutambua wewe ni asset au ni liability tukapeana nafasi kiroho safi.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Jamii inamchanganyiko wa hayo makundi yote uliyoyataja hapo juu, wajinga, wapumbavu, wasaka fursa, nk..

Kwenye mapambano, ni vyema kuanzisha ukiwa na dhamira yako ya dhati, wengine watajiunga nawe mbele ya safari wakija kuuona umuhimu wake.

Kuna wakati akili zetu huwa zinalala mpaka zije kuamshwa na tukio fulani ndio tuone umuhimu wa jambo lililoanzishwa na wale tuliokuwa hatuwaelewi mwanzo.
 
Kwa hakika.

Cuba yote walikuwapo 82 tu waliokuwa tayari.

Zimbabwe walikuwapo kina Muzorewa, Sithole na wenzao wakizipinga harakati zote za ukombozi.

Hata huku kama huko pia kina Muzorewa wapo.

"Wapenda ngono na wachawi siyo kwenu tu, hata kwetu wapo." --SAM.
 
Mchakato wa kuitoa nchi katika hatua moja duni kwenda katika hatua nyingine bora zaidi kwa jina la ukombozi, unahitaji watu waliodhamiria kweli kweli.

Jukumu hili haliwezi kuwa la kila mtu. Nyuso za watu hawa, maneno, (nyuzi, posts) na matendo yao hujionyesha.

Inawezekana namna gani kuwasikia Nyerere, Museveni, Kagame, Sokoine, Putin, Mandela, Lissu, Mbowe, Mangula, Garang, Saddam, Milosevic, Thatcher, Gadaffi, XI, Mengistu, Mugabe, Castro, Obama, Kim na wa namna hiyo wakiwa carried kwenye mizaha au hadithi za mbususu, simba na yanga, man city na man u, vumbi la congo na ya namna hiyo?

Pana haja ya kukatumia ka litmus haka ka kupima kudhamiria, kuwaengua wengine kwenye harakati hizi ili kutosumbuka na kupoteza muda na watu wasiojitambua.

View attachment 2374229

Kuikataa mikono yenye damu hakuwezi kuwa nusu nusu.

"Mtu hawezi kuwa mguu mmoja ndani na mwingine nje."

Ukombozi hauhitaji watu wengi. Wasanii na waachwe kuendelea na usanii wao kwa raha zao.

Ukombozi hauwezi kuachiwa Mungu kutuletea bila ya sisi kuchukua hatua za makusudi.

View attachment 2374234

Ni heri kuwa na watu wachache waliodhamiria kuliko kuwa na lundo la waoga, wajinga, wapumbavu au wasaka fursa.

Ni vyema kujipima mwenyewe kutambua wewe ni asset au ni liability tukapeana nafasi kiroho safi.

Au nasema uongo ndugu zangu?
fact tupu mzee wang... ili ukombozi uje watu wanaitaj kiongoz wenye nia na kiongoz anaitaj watu wenye nia na uthubut ... kati ya hvy viwil kimoja kikiwa opposite n kingjne hakun ukumboz utaokuj hata siku mmoja
 
Umesema ukweli kabisa. Dhamira inaweza kuleta mabadiliko makubwa yanayowashinda wengi. Hata vijana wadogo kama Thomas Sankara, Jerry Rawlings nk waliondoa tawala kongwe zilizojaa ubadhilifu wakati wakubwa wao wa kijeshi majenerali nk wakishindwa kufanya.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Dhamira maana yake ni kuwa na nia na uthubutu. Huwezi kuwa na dhamira ukose kimojawapo au ukose vyote viwili.

Wenye dhamira wana nia na uthubutu.

Panapo dhamira panahitaji mkakati thabiti. Hapo ndipo uongozi mahiri unapohitajika.

Kwenye list Ile Pana Nyerere - Kim.
 
Umesema ukweli kabisa. Dhamira inaweza kuleta mabadiliko makubwa yanayowashinda wengi. Hata vijana wadogo kama Thomas Sankara, Jerry Rawlings nk waliondoa tawala kongwe zilizojaa ubadhilifu wakati wakubwa wao wa kijeshi majenerali nk wakishindwa kufanya.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app

Ni nia yetu kuendesha harakati hizi kwa amani na kwa mujibu wa katiba hadi ushindi kamili .

Inawezekana, kwani penye nia Pana njia.

Shime waungwana.
 
Tuishi kulingana na hulka, mitazamo na tamaduni za watu wetu na kwa kuzingatia hizo tuandae mikakati sahihi ya ukombozi. ,Nafahamu hali ya kisiasa tuliyo nayo inaumiza na inakera. Lkn siyo sahihi kuchukua njia za akina Putin, Mandela ama Kim na kuzitumia kwa jamii kama ya watanzania. Utabaki peke yako na utafeli asubuhi sana.

Ndiyo maana hata Nyerere aliliona hilo akaamua kutumia njia ya ushawishi (lobbying) badala ya mtutu ili kuupata Uhuru wa Tanganyika. Alifanya lobbying ktk kipindi ambacho wimbi/fasheni ya kuutafuta Uhuru kwa mtutu ilikuwa juu Sana.

Lkn Nyerere akawasoma watanganyika akaona hatatomboa akitumia mtutu.

Kizazi hiki tumekwama wapi hadi tunakosa ubunifu tunalazimisha kukopa mambo ya miaka 1960s??
 
Watanzania siyo watu wa mikiki mikiki. Nikupe mfano mwingine. Kule Uganda kuwaamata wanasiasa maarufu kama Kiza Besigye ama Boby Wine inakuwa balaa kweli kweli na polisi wengi hufariki. Maandamano huendeshwa nchi nzima kuilazimisha serikali kuwaachia huru.

Hapa kwetu Tanzania wanasiasa maarufu mfano Mbowe, hukamatwa kama Panya-road tu nchi inatulia kana kwamba hakuna Jambo kubwa lililotokea. Hao ndiyo watanzania.

Viongozi wetu wanaboronga, tena wanaboronga kweli kweli lkn watanzania wanagugumia na kusemea vifuani mwao tu.

Hebu tukae chini tubuni mbinu itakayowaamsha watanzania wapiganie haki zao na kuifanya serikali iwe inawaogopa wananchi. Tusiige ya nchi za watu yasiweza kufanya kazi hapa nchini.
 
Ni nia yetu kuendesha harakati hizi kwa amani na kwa mujibu wa katiba hadi ushindi kamili .

Inawezekana kwani penye nia Pana njia.

Shime waungwana.
Kwa huu mfumo uliopo na watawala ni hawa hawa CCM harakati za namna hii binafsi hutakuja kushuhudia wewe wala wanao katika maisha yenu yote. CCM ni genge la kimafia hivyo unayo yaona kila uchaguzi yatajirudia na kila anaye wekwa nao madarakani anabadili chupa ila mvinyo ni uleule. Kama wenyewe hawaheshimu katiba kwa nini walindwe na hiyo katiba?
Alichofanya Jerry Rawlings kule Ghana ndicho kilikuja kuigeuza nchi ile kuwa yenye demokrasia ya mfano kwa Africa nzima leo hii
 
Tuishi kulingana na hulka, mitazamo na tamaduni za watu wetu na kwa kuzingatia hizo tuandae mikakati sahihi ya ukombozi. ,Nafahamu hali ya kisiasa tuliyo nayo inaumiza na inakera. Lkn siyo sahihi kuchukua njia za akina Putin, Mandela ama Kim na kuzitumia kwa jamii kama ya watanzania. Utabaki peke yako na utafeli asubuhi sana.

Ndiyo maana hata Nyerere aliliona hilo akaamua kutumia njia ya ushawishi (lobbying) badala ya mtutu ili kuupata Uhuru wa Tanganyika. Alifanya lobbying ktk kipindi ambacho wimbi/fasheni ya kuutafuta Uhuru kwa mtutu ilikuwa juu Sana.

Lkn Nyerere akawasoma watanganyika akaona hatatomboa akitumia mtutu.

Kizazi hiki tumekwama wapi hadi tunakosa ubunifu tunalazimisha kukopa mambo ya miaka 1960s??

Utakuwa hautusomi vyema tu mkuu. Hakuna sehemu tunayongelea mtutu. Wala hakuna tunapoongelea kukopa lolote lisilofaa la 1960s.

Hata hivyo yapo yenye kufanana katika struggles zote. Struggles zote lazima kuwa na dhamira na kuwa na mikakati. Dhamira inaweza kuwa Ile ile japo mikakati inaweza kuwa tofauti.

Kwani hata tuna ya kuficha?

Tunayo dhamira ya dhati ya kudai mabadiliko kama ilivyokuwa kwenye 1990s. Tofauti yetu ipo kwenye njia.

"Tunadai mabadiliko kwa njia za amani na kwa mujibu wa katiba."

Kwamba hadi sasa hilo haulifahamu mkuu na unaongelea mitutu, unapaswa kuona ni kwa nini ni muda sasa wa kuwatambua walio assets na liabilities.

Tutaendelea kuongea yale yale hadi lini? Si yatakuwa yale ya Museveni, wakaramojong na suruali zao?
 
Mkuu mapinduzi ya namna gani unayo yazungumzia kwa hapa taifani :- i, Civil revolution au
ii, Millitary revolution
 
Kwa huu mfumo uliopo na watawala ni hawa hawa CCM harakati za namna hii binafsi hutakuja kushuhudia wewe wala wanao katika maisha yenu yote. CCM ni genge la kimafia hivyo unayo yaona kila uchaguzi yatajirudia na kila anaye wekwa nao madarakani anabadili chupa ila mvinyo ni uleule. Kama wenyewe hawaheshimu katiba kwa nini walindwe na hiyo katiba?
Alichofanya Jerry Rawlings kule Ghana ndicho kilikuja kuigeuza nchi ile kuwa yenye demokrasia ya mfano kwa Africa nzima leo hii

Hapana mkuu la muhimu ni kuchagua mbinu, yaani mikakati.

Ya msingi ni kuwa inajulikana kunahitajika watu wenye dhamira yaani nia na uthubutu kamili.

Dhamira ni ya kuleta mabadiliko kwa mujibu wa katiba. Atakaye chagua violence siyo sisi. Lakini hatuta surrender kwa mujibu wa katiba.

Tunapaswa kuelewana hapa, Ili kuweza kupanga mikakati ya ushindi kama binadamu wenye kuwajibika kusajili matokeo.

Inawezekana kwani penye nia pana njia.

Alisema J.J. Rawlings (RIP):

"Ni lazima ifikie pale ambapo hata kama shweitani atakuwa ndiye mtawala (rais), itakuwa ni lazima afanye kile ambacho Waghana (wananchi) wanataka na wala siyo kile ambacho yeye shweitani na genge lake wanataka."
 
Viongozi waliopo sasa wanaakisi jamii kubwa ya wanaowaongoza
 
Back
Top Bottom