Ukombozi wa Palestine utafanywa na Urusi sio Marekani wala Waarabu

Ukombozi wa Palestine utafanywa na Urusi sio Marekani wala Waarabu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Iko siku Palestine itakombolewa na Urusi kutoka kwenye tabu ya nchi za Magharibi na Israel. Waendelee kunywa mtori nyama watazikuta chini.

Mungu sio mjinga kiasi cha kuwaacha wapalestine wateseke milele. Mungu atafanya hivyo kama alivyofanya kwa wa Israel pia. Mungu atafanya hivyo hata kwa bara la Afrika. Siku sio nyingi wazungu watakuwa maskini sana, wakimbizi na hata watumwa, wetu kama wataendelea na kile wanachokifanya sasa.
 
Myahudi yupo hadi kremlin

Tafuta klip yoyte ya putin akiisema vibaya israel km utaipata

Kwenye hii vita ya ukraine,raia wa ukraine na urusi wanapewa hifadhi nchini israel

Hata modernization ya jeshi la China, Myahudi kawauzia sana Wachina tekinolojia ya Kijeshi.

Hata siku moja hutamsikia Mchina akitoa neno juu ya madhila ya Wapalestina
 
Urusi hii hii ya Putin?...
 
Sera ya kuikomboa Palestina ni ya fundamental muslims na extremists, wale Waislamu wagumu wagumu. Moderate Muslims na secularists kama Assad wa Syria ndio dawa ya fundamentals. Sio Russia tu, hata nchi nyingine zenye mgogoro na waislamu kama Israel na Marekani zinapenda moderate na secularists na ndio wanashika mamlaka. Hawa waasisi wa ISIS, Hezbollah na Hamas hawatopata taifa la kuwaunga mkono. Hizo ndoto ziliishia kwa Anwar Sadat na Hafez al Assad.

Angalia Saudi Arabia inaishambulia Yemen miaka kama kumi sasa na hakuna taifa linanyoosha kidole sio majirani Waarabu wala wazungu. Yemen pale kuna Houthi wanasaidiwa na Iran ambaye vilevile anasaidia Hezbollah na Hamas ila wakati huohuo Sunni muslims kama Qatar na Saudi Arabia hawataki kabisa kusikia influence ya Iran. Hili suala linaisumbua Iraq ambayo ina balance idadi ya haya makundi mawili.

Ukiachana na Iran, hakuna nchi dunia hii ina interest na Palestina kwenye sera zake. Russia hawezi acha uhusiano wake na Israel eti ampiganie Palestina. Soviet Union ilijaribu kipindi ina nguvu, Israel ni ya kawaida na Waarabu wana nguvu na umoja ikashindwa sembuse leo Russia na mambo yake mengi iteseke wakati Israel imekuwa powerful na Waarabu wanapungua umoja. Serikali za kiarabu zinataka survivability ambayo inahatarishwa na sera za hivyo
 
Myahudi yupo hadi kremlin

Tafuta klip yoyte ya putin akiisema vibaya israel km utaipata

Kwenye hii vita ya ukraine,raia wa ukraine na urusi wanapewa hifadhi nchini israel
Hakuna rafiki au adui wa kudumu duniani. Urusi Sasa ni rafiki wa Iran, Syria, uturuki rna nchi kadhaa za kiarabu ikiwemo Egypt ambazo ni adui wa Magharibi na Israel. Urusi inatafuta washirika wapya ambao itawaimalisha kijeshi na kuwalinda pia. Nyuma ya Urusi wapo China, NKorea, India , Venezuela, Belarus, Serbia, Brazil, na nchi nyingi za Amerika kusini. Muungano wa Ulaya utaasambaratika kabisa.
 
Tofautisha urusi na putin
.haya ya sasa ni mihemuko ya putin na hana muda mrefu ataondoka
Hakuna rafiki au adui wa kudumu duniani. Urusi Sasa ni rafiki wa Iran, Syria, uturuki rna nchi kadhaa za kiarabu ikiwemo Egypt ambazo ni adui wa Magharibi na Israel. Urusi inatafuta washirika wapya ambao itawaimalisha kijeshi na kuwalinda pia. Nyuma ya Urusi wapo China, NKorea, India , Venezuela, Belarus, Serbia, Brazil, na nchi nyingi za Amerika kusini. Muungano wa Ulaya utaasambaratika kabisa.
 
Kaaazi kweli kweli!

Kwanza tu aliyeutangazia umma kwamba kuwepo na mataifa yanayotambulika kuwa ni mataifa ya Kiisilsmu, tayari alifanya kosa kubwa mno ambalo Kwa nje nje ni kama hakuna kosa,

Ni ubaguzi Mkubwa juu ya mataifa mengine, na ndiyo maana migogoro mingi inayoyakumba mataifa yanayoitwa ya Kiisilamu, mataifa mengine yasiyo na mlengo huo, hayaingiliii saana hiyo migogoro Kwa maana ya huo ubaguzi yakiwa na ile dhana ya kusema, watakoma,!

Na ukiona taifa la Kiisilamu migogoro yake imepewa sapoti ya kiutatuzi na mataifa yenye nguvu, ujue hapo kuna maslahi ya mataifa hayo na si vinginevyo!

Ni vema tu mataifa hayo ya Kiisilamu yakaungana na yaache kushambuliana menyewe Kwa menyewe,

Na ijulikane, Dunia ya Magharibi na ulaya iko mbasli saana kuliko dunia ya Asia, Africa n.k

Wakati nchi za Kiislamu zikijivunia kuitwa hivyo, nchi za Dunia ya kwanza zinaona dhana hiyo ni uundwaji wa mashambulizi dhidi yake

Kwa hiyo, mataifa hayo ya Ulaya na America, yametengeneza fitna ambayo waarabu hawatatoboa hizo fitina, wataendelea kumalizana wao Kwa wao Kwa Mashaka kuwa, wakiachwa, mwisho wa siku hayo mataifa, ni kwenda kupigana na mataifa hayo ya dunia ya kwanza

Ni mhimu kujitahidi mno Kwa mataifa ambayo yako nyuma ya wakati, kuusogelea wakati na kufahamu jinsi Dunia inavyochezeshwa na mataifa ysliyo mbaali
 
Palestine ni Mwenyezi Mungu ndiye atakayewaokoa.

Mungu ana njia nyingi za kunusuru watu wake wanaoonewa.

Vita kati ya Uajemi na Babylon ilipelekea kukomesha utumwa wa Wana Wa Israel.

America civil war ilipelekea kukomesha utumwa ndani ya America.

Vita ya kwanza ya dunia na ya pili ilipelekea kukomesha utumwa wa wachina dhidi ya ya wajapan, kusaidia Wayahudi kupata sehemu salama ya kuishi huko Israel na kuzipa nchi nyingi sana za Afrika uhuru.

Usije ukastaajabu ikatokea vita nyingine kubwa sana nyingine itakayopelekea wapalestina nao wanusurike.

Kwenye Qur'an Mwenyezi Mungu anasema huwa anawatumua watu kuondoa dhulma katika ardhi.
 
Moderate Muslims na secularists kama Assad wa Syria ndio dawa ya fundamentals.
Mbona Sasa waarabu walishirikiana na Uturuki kusaidia waasi ambao ni extremist ili kumpinga Assad?
 
Iko siku Palestine itakombolewa na Urusi kutoka kwenye tabu ya nchi za Magharibi na Israel. Waendelee kunywa mtori nyama watazikuta chini.

Mungu sio mjinga kiasi cha kuwaacha wapalestine wateseke milele. Mungu atafanya hivyo kama alivyofanya kwa wa Israel pia. Mungu atafanya hivyo hata kwa bara la Afrika. Siku sio nyingi wazungu watakuwa maskini sana, wakimbizi na hata watumwa, wetu kama wataendelea na kile wanachokifanya sasa.
Tokea lini mwarabu akawa na akili? Yule atabaki kuwa zwazwa tu miaka yote!
 
Mbona Sasa waarabu walishirikiana na Uturuki kusaidia waasi ambao ni extremist ili kumpinga Assad?
Uturuki hana interest ya kumpiga Assad. Baba yake Assad yule Bashar al Assad alikuwa strong sio kama mwanae huyu, yule senior aliifanya Syria iwe ya kikorofi na hivyo Uturuki au yeyote asingetia mguu pale Syria. Baada ya waasi kuisumbua serikali ya Assad akawa anapokea msaada kwa yeyote yule, wanamgambo wa Kikurdi wanaitaka sehemu fulani ya Uturuki na ya Iraq, Syria hawana claims kivile. Ikatokea ISIS ambayo ilitaka kutawala ulimwengu wa Kiislamu, makundi mengine kama Taliban hayakuwa yanaipenda pamoja na hao Kurdish fighters. Wakurdi wakawa wanapigana na ISIS Kaskazini mwa Syria, wakati ISIS haina claims kwa Uturuki. Hivyo ISIS na Uturuki wakajikuta adui yao ni Wakurdi, wakati huo Syria ikajikuta adui yake ni ISIS na waasi.

Uturuki ikalazimika ipigane na Wakurdi ambao walikuwa wanaanzisha strongholds Kaskazini mwa Syria ili wasije ungana na ndugu zao PKK na Peshmerga. Israel haikuwa claimed na ISIS hivyo sio adui yake, Iran ikawa inaisaidia Syria kupigana na ISIS ila ikapata mwanya kupitisha silaha kuzipeleka Lebanon kwa Hezbollah, Israel ikaja Syria kupigana na influence ya Iran.

Fact ni kwamba Israel inampenda Assad kwa kuwa ni mnyonge, hana muda wa kujenga uchumi wa Syria na anaifanya iwe busy na uadui wa ndani. Israel haitamani Syria itulie iwe na maendeleo watajenga uchumi na jeshi kisha waitishie maana ina eneo lao la Golan heights. Israel huwa inashambulia silaha za Iran zilizopo Syria ili zisiende Lebanon, haishambulii jeshi la Syria likiwa lenyewe.

Then Wakurdi sio Waarabu, ni jamii inayobaguliwa na Waarabu pamoja na Waturuki. Kuna makosa yalifanyika kuigawa Middle East pale baina ya Syria, Turkey na Iraq kulitakiwa kuwe na nchi ndogo ya Wakurdi. Huwa ni wakorofi na warriors, pia huonekana ni barbarians kwa majirani hivyo wanaishi kwa kupigana, wakiweka silaha chini wanafanyiwa extermination.

Kwenye mkanganyiko huo Saudi Arabia anaingia akiwa hana shida na Israel wala Uturuki bali Iran.
 
Mbona Sasa waarabu walishirikiana na Uturuki kusaidia waasi ambao ni extremist ili kumpinga Assad?
Shida ya uturuki ni wale Wakurdi Abdalah Ochlan wa Chama cha PKK ambao wanapatikana Syria, Denmark na kule kwingine ambako Uturuki inawakatalia kujiunga na NATO.
 
HAPANA SIYO HI YA PUT

IN, LABDA YA PUT OUT
Kwa taarifa yako kule Urusi wako watu ambao ni wakali kuliko Putin. Huyu Putin snap uwezo wa kuzima satellite zote za mawasiliano ya adui anga za juu . Anasubbiri vita kule Ukraine ivuke mstari mwekundu waone vita kamili ya kigiditali
 
Iko siku Palestine itakombolewa na Urusi kutoka kwenye tabu ya nchi za Magharibi na Israel. Waendelee kunywa mtori nyama watazikuta chini.

Mungu sio mjinga kiasi cha kuwaacha wapalestine wateseke milele. Mungu atafanya hivyo kama alivyofanya kwa wa Israel pia. Mungu atafanya hivyo hata kwa bara la Afrika. Siku sio nyingi wazungu watakuwa maskini sana, wakimbizi na hata watumwa, wetu kama wataendelea na kile wanachokifanya sasa.
madhala ya tozo haya
 
Kwa nini Palestine ikombolewe na Russia na sio kujikomboa yenyewe ?

# Survival of the fittest, that's how nature works.
 
Hata modernization ya jeshi la China, Myahudi kawauzia sana Wachina tekinolojia ya Kijeshi.

Hata siku moja hutamsikia Mchina akitoa neno juu ya madhila ya Wapalestina
Kwamba China imejengwa kiteknolojia ya kijeshi na Israel ?
deng-s-four-modernizations-l.jpg
 
Back
Top Bottom