Uturuki hana interest ya kumpiga Assad. Baba yake Assad yule Bashar al Assad alikuwa strong sio kama mwanae huyu, yule senior aliifanya Syria iwe ya kikorofi na hivyo Uturuki au yeyote asingetia mguu pale Syria. Baada ya waasi kuisumbua serikali ya Assad akawa anapokea msaada kwa yeyote yule, wanamgambo wa Kikurdi wanaitaka sehemu fulani ya Uturuki na ya Iraq, Syria hawana claims kivile. Ikatokea ISIS ambayo ilitaka kutawala ulimwengu wa Kiislamu, makundi mengine kama Taliban hayakuwa yanaipenda pamoja na hao Kurdish fighters. Wakurdi wakawa wanapigana na ISIS Kaskazini mwa Syria, wakati ISIS haina claims kwa Uturuki. Hivyo ISIS na Uturuki wakajikuta adui yao ni Wakurdi, wakati huo Syria ikajikuta adui yake ni ISIS na waasi.
Uturuki ikalazimika ipigane na Wakurdi ambao walikuwa wanaanzisha strongholds Kaskazini mwa Syria ili wasije ungana na ndugu zao PKK na Peshmerga. Israel haikuwa claimed na ISIS hivyo sio adui yake, Iran ikawa inaisaidia Syria kupigana na ISIS ila ikapata mwanya kupitisha silaha kuzipeleka Lebanon kwa Hezbollah, Israel ikaja Syria kupigana na influence ya Iran.
Fact ni kwamba Israel inampenda Assad kwa kuwa ni mnyonge, hana muda wa kujenga uchumi wa Syria na anaifanya iwe busy na uadui wa ndani. Israel haitamani Syria itulie iwe na maendeleo watajenga uchumi na jeshi kisha waitishie maana ina eneo lao la Golan heights. Israel huwa inashambulia silaha za Iran zilizopo Syria ili zisiende Lebanon, haishambulii jeshi la Syria likiwa lenyewe.
Then Wakurdi sio Waarabu, ni jamii inayobaguliwa na Waarabu pamoja na Waturuki. Kuna makosa yalifanyika kuigawa Middle East pale baina ya Syria, Turkey na Iraq kulitakiwa kuwe na nchi ndogo ya Wakurdi. Huwa ni wakorofi na warriors, pia huonekana ni barbarians kwa majirani hivyo wanaishi kwa kupigana, wakiweka silaha chini wanafanyiwa extermination.
Kwenye mkanganyiko huo Saudi Arabia anaingia akiwa hana shida na Israel wala Uturuki bali Iran.