David M Mrope
Senior Member
- Jul 13, 2021
- 115
- 74
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambayo ukishafikisha miaka 60 basi unatakiwa uachane na ajira serikalini. Mfumo huu umeendeshwa kwa muda mrefu tu. Ni kweli ulikiwa mfumo mzuri katika kipindi kile ambacho bado wasomi walikuwa wachache sana katika jamii zetu.
Lakini kwa sasa serikali ni vyema kama ikapunguza miaka ya kustaafu na kufikia 50. Zipo faida mbalimbali endapo wafanyakazi watastaafu wakiwa na miaka 50. Basi tuangalie baadhi ya faida hizo;
(i) ITAPUNGUZA TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA.
Tatizo la ajira kwa vijana katika nchi yetu ni kubwa sana. Vijana wengi wanamawazo ya kimapinduzi. Wanandoto na maono ya kisasa. Wananguvu katika ufanisi na watu makini zaidi katika kazi. Lakini katika nchi yetu vijana hawa hawana ajira,na maarifa yao ya kimapinduzi ya kisasa yanakwenda na maji.
Hivyo kama serikali itaruhusu kufanya kazi miaka 50 tu kisha unaachia ngazi,hii itaruhusu kijana aliyeko mtaani kushika ngazi kwa kasi mpya na kusonga mbele.
(ii) ITAONGEZA UFANISI KATIKA KAZI.
Mfanyakazi akishajua akishatimiza miaka 50 tu anaondoka,basi hakutokuwa na mtu anachezea ovyo ovyo mshahara. Leo ukikutana na mzee ofisini hata hawezi kuona maandishi yani na ashajichokea mwenyewe ila hang'atuki. Tena wazee wengine hawana la kufaya mpaka wanageuka walevi tu,na kupunguza ufanisi kazini.
(iii) ITASAIDIA MATUMIZI BORA YA PESA ZA KUSTAAFU.
Tatizo la matumizi mabaya ya pesa za kustaafu ni kutokana na uzee. Kwa sasa serikali inatoa milioni mia moja kwa mzee wa miaka 60 inategemea huyu mzee kweli ataweza kuitumia kwa usahihi hii pesa?. Unakuta wazee washajishukuru tu kimaisha basi wanaponda mali kufa kwaja.
(iv) ITASAIDIA UTENDAJI KAZI KUENDANA NA MABADILIKO YA KITEKNOLOJIA.
Hii itasaidi sana kukuza uchumi wa nchi yetu. Mfano saizi unaweza ukaenda ofisini ukakuta mzee hata kompyuta hawezi kutumia. Sasa katika teknolojia ya sasa mambo yamebadilika sana,huyu mzee anatakiwa apishe vijana waliosomea mambo mapya.
(v) ITAKUZA SEKTA YA KILIMO NA UFUGAJI.
Wakati wa sasa serikali inasubiri mzee afikishe miaka 60 kisha astaafu,mzee huyu anakuwa ashachoshwa sana na anakosa hata nguvu ya kufanya shughuli zingine za kiuchumi. Ni vizuri serikali ikapunguza umri wa kustaafu mpaka miaka 50 ili kutengeneza wastaafu wenye nguvu za kuendeleza sekta zingine mfano kilimo na ufugaji.
(v) ITASAIDIA KURUDISHA MIKOPO YA ELIMU YA JUU KWA KIWANGO KIKUBWA.
Kwa sasa serikali inapata hasara kubwa sana kwa kusomesha vijana wengi wa elimu ya juu na mwishowe wanakaa mtaani bila ajira.
Sasa ili serikali irudishe pesa zote kwa wakati, na ili zile pesa zitumike kusomeshea wengine, basi kwa njia hii ya kupunguza umri wa kustaafu ni bora zaidi kwani utasaidia kuajiri vijana hawa ambao walikopeshwa na serikali.
NB.
Sheria hii iwe kote katika taasisi binafsi na taasisi za kiserikali. Itasaidia sana kupunguza tatizo la ajira.
DAVID M MROPE
SUA.

Upvote
7