Sizinga
Platinum Member
- Oct 30, 2007
- 9,374
- 6,857
Habari kutoka mtandao wa chunichi.co.jp unaeleza kuwa gari za Sedan Toyota Crown zimefikia ukomo wa utengenezaji wake baada ya kutoa updated version ya mwaka 2021.
Sababu kubwa ya kufikia ukomo wa magari haya pendwa na yenye 'high perfomance and comfortability' ni mauzo madogo katika soko la kimataifa. (Just remember kuna kipindi Toyota Crown sedan hazikuuzwa kabisa katika soko la US). Utakumbuka Toyota Crown zilianza uzalishaji mwaka 1955 na zinafikia ukomo wake mwaka 2021.
Mtandao huo unaendelea kuhabarisha kuwa Mbadala wa sedan hizo itakuwa ni Toyota Crown SUV gari ambazo bado zitaendelea kutumia jina la 'CROWN' zitakuwa na platform ya 'Toyota Highlander'. Toyota Crown SUV hizo zitakazoanza uzalishwaji wake mwaka 2022 zitajikita zaidi katika soko la Kimataifa la Marekani pamoja na Uchina. Gari hizo zitakuwa na mifumo mingi ya kiusalama hasa zikikaribiana na kitu chochote (pre-crash safety, pedestrian detection, cyclic detection nk).
Maoni ya wanamtandao wengi wamestushwa na habari hizo kwani gari hizo zimeonekana kupendwa sana hasa na vijana kutokana na muundo wake pamoja na perfomance yake, na wameenda mbali zaidi kwa kudai kuwa gari za juu aina ya SUV zipo nyingi sana kwanini TOYOTA wamekuwa na akili mgando za kuachana na utengenezaji wa gari hizo.
Haya wale wamiliki wa ndege za chini habari ndo hiyo, itabidi muanze kutafuta mbadala wa sedan hizo labda mnaweza kuhamia kwenye Toyota Avalon kwa sasa.