Ukomo wa Toyota Crown Sedan

Sasa Toyota kwenye hiyo Supra aliingia cha kike, kukubali BMW kuweka injini zake na kumsaliti JZ engine.

Wanunuzi wa mwanzo wa Supra na wadau wa magari walilalamika gari kuwa na performance ndogo. Mwaka huu BMW wametoa tangazo kuwa watatengeneza tena Supra ikija na maboresho.Fans wa Toyota Supra walijua hii itakuwa Monster sasa BMW akaweka injini za inline 4 na inline 6 cylinder na teknolojia kibao gari ikiwekwa na wakina Nissan Skyline au Gt-r inakuwa mchumba.

Hiyo Supra uwezi kuamini mtangazaji wa Top Gear amekiri wazi wazi Toyota Yaris yenye 3cylinder na 1600cc ina uwezo kumzidi Supra.
 
Ile GR Yaris ni mziki mnene! Supra ya BMW ni chamdoli kweli.
 

Kumlinganisha Toyota na Benz ni matusi , Toyota anauza sana sababu gari zake bei nafuu ila ni dharau kumlinganisha na Mercedes Benz
 
Mjerumani anaumba gari.

Toyota anaunda vyuma vyenye matairi.
 
Mjerumani anaumba gari.

Toyota anaunda vyuma vyenye matairi.
Si mkanunue za Mjerumani. German High commission Office hapa Tanzania inatumia gari za Toyota. Wakitoa misaada kwa serikali ya magari bado wanatoa gari za Toyota.
 

Hawa ni Wajerumani 100% kazi zao za field hapa kwetu wanatumia LR na LC tu, sijawahi ona hata siku moja na magari ya Kijerumani. Ila sisi wamatumbi ndio tunajua gari bora linatoka kwa mjerumani...πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Mjerumani anaumba gari.

Toyota anaunda vyuma vyenye matairi.
Mjerumani anatengeneza gari Luxury na akilenga high income earners, Toyota anatengeneza gari za luxury,usafiri na za watu wa kipato cha kawaida Kwa ufupi anamgusa kila mtu kuanzia bepari mpaka mmatumbi wa Naliendele.
 
1. Toyota anapendwa na wabongo kwasababu spare moja inaweza ikawa na bei nyingi. Mpaka used unapata kwa 5% ya bei halisi.

2. Tunapenda Toyota kwasababu hatutunzi gari zetu vizuri. Service haifanyiki kwa wakati, tunanunua cheap and unreliable spares tunarundika.

3. Mafundi wa Toyota wanaweza kuguess na gari ikatembea, ila sio Nissan wala EU cars.

Ila tukisema tuitunze Toyota vile inatakiwa kutunzwa, basi wabongo wengi watakimbilia kwenye baiskeli. Manake utauziwa shockups genuine toka toyota tena bran new kwa bei mara hata 10 kwa zile used tunazonunua ilala.
 
Zamani hapa bongo tulikuwa tunaogopa sana Subaru kisa bei ya spares ni kubwa na mafundi hakuna.

Ila sahivi zimeanza kutapakaa.

Wabongo wengi tunaishi kwa mazoea, hatujiongezi. Kitu ambacho unaweza kukipata kwenye manual au ku-google hujishughulishi kukitafuta.

Mafundi wa german cars wanachukulia uzoba wa wabongo kuwapiga. Kifaa unachoweza agiza mwenyewe kwa $200, unapigwa mpaka 900K. Kisa hatujiongezi.

German cars spares zake ni mkataba, bei ni sahihi sawa na hizi za Toyota. Shida kubwa ya german cars ni luxury features nyingi ambazo ni gharama kuzimantain.
 
Naona magari ya IT yanayopelekwa Rwanda / Congo ni visu (Hyundai / Kia/ Daewoo/ Mazda / Volvo/ Bmw/ Audi / Ford sijajua wenzetu wanawezaje kuyamudu. Najua Tanzania/ Kenya / Uganda ni Toyota tu. Sijajua huu uchaguzi unachangiwa na nini hasa.
 
Watu wa field Tz ni wangapi? 95% ya wanaonunua magari Tz ni matumizi ya mzinguko ya hapa na pale.

Hata hizo balozi wanatumia S Class, VW Touareg na 7 Series kutoka mwakwao mpaka ofisini au mizunguko ya town. (Ushahidi ninao).

Wanapotaka kwenda porini kukagua miradi yao ndo wanatumia hizo LCs.

Sasa wabongo wangapi wanaenda na spacio au ist sehemu ambazo LC zinapelekwa mara kwa mara?

Kingine LC zinatumika sana kwasababu ya uwepo wa dealership za Toyota hadi huko mikoani na sio kwamba haziharibiki. Zinapata shida ila kwakuwa authorized workshops zipo almost kila mkoa ndo maana wanazitumia ili wakipata breakdown wazikimbize zitengenezwe chap.

Na UK embassy na miradi yao yote wana recommend kutumia Discovery 3 or 4. Na wao ndo wanatumia hizo. Ila kwa matumizi ya hapa mjini hakuna ubalozi wowote wanaotumia magari ya Toyota. Hata ubalozi wa Indonesia au Iran. Wanaendeshwa kwenye S class.
 
Naona magari ya IT yanayopelekwa Rwanda / Congo ni visu (Hyundai / Kia/ Daewoo/ Mazda / Volvo/ Bmw/ Audi / Ford sijajua wenzetu wanawezaje kuyamudu. Najua Tanzania/ Kenya / Uganda ni Toyota tu. Sijajua huu uchaguzi unachangiwa na nini hasa.
Ni mentality tulionayo.

Kiuhalisia 80% ya wanaonunua magari hata used hapa bongo hawawezi kuyatunza vile inapaswa. Oil yenyewe zinatumika zile SAE 40 zilizo chini ya kiwango. Nani ataenda kununua recomended oil ya 80K wakati ya 30K inafanya kazi? Au ukanunua shockup ya 1.6M wakati ya 170K inafanya kazi?

Ila hizo brand zingine utaambiwa hakuna spare wala mafundi, ila jibu ni kwamba hakuna spare feki na mafundi wengi shule hakuna. Wanafanya kazi kwa kuunga.
 
Naona magari ya IT yanayopelekwa Rwanda / Congo ni visu (Hyundai / Kia/ Daewoo/ Mazda / Volvo/ Bmw/ Audi / Ford sijajua wenzetu wanawezaje kuyamudu. Najua Tanzania/ Kenya / Uganda ni Toyota tu. Sijajua huu uchaguzi unachangiwa na nini hasa.
Huko Congo/Zambia pesa sio ya mawazo na wapo rough kweli kwenye kutumia magari Yao. Ukienda utakuta BMW/Benz/Audi tangu iagizwe imetumika na chasis number ila haijasajiliwa na ipo juu ya mawe.
Magari ya mzungu hayana shukrani ugumu wa kutunzika sio Bongo hata uko ulaya watu wanalalamika tembelea forums zao.

Sema akipendacho mtu huwezi kumzuia asitumie Kwa sababu ndogo ndogo.
 
Mkuu, hata Supra original haina perfomance. Mpaka uisuke 2jzgte ndio upate perfomance ya ukweli. Hata hii Mpya, kuna jamaa ameitune amepata 1000hp. Fans walicholalamika sio kwamba engine katengeza BMW, bali ni 100% rebadged Z3 new model tu. Sura ya gari ni Z3, engine mwenyewe ni Z3. Yaani in short, haina Full DNA ya toyota na hivo fans hawakufurahia. Toyota walitakiwa watoe Supra fully made by toyota, lakini wamekimbia cost na kumtafuta BMW. Haya yametokea hata kwenye toyota 86. Wameazimana na Subaru, wakati toyota alikuwa na concept yake nzuri tu.
 
S
Siko biased unless it comes to reliability.

Reverse camera tu ni very basic feature kwa gari za kuanzia 2005 na kuendelea ila matumizi yake ni hafifu sana hapa nchini. Ila it doesn't make it a bad thing as long as it works.
Linapokuja suala la reliability sipingi kuwa toyota yuko vyema tena sana. Ford alitoa tangazo kutaka kuwaaminisha watu kuwa eti wao wana most reliable car, Toyota akamaindi na tangazo lao wakaliondoa.
 
HIo gari imekuwa dissapointment kwa wengi. Labda watu walitegemea Toyota watengeze Supra kama Nissan GTR. Halafu Nissan GTR nazungumzia izi mpya, zipo kwenye level za kina corvette, dodge, mustang n.k

2020 SUpra ina 335Hp
original supra 276 HP
Nissan Skyline gtr 276
2020 Yaris ina 106 hp Huyo jamaa wa Top Gear akashindanishe na IST kwanza.

Wamenuna Toyota hajawapa walichotegemea. ni 2020, 2jz wameacha kitambo sana kutengeza.
 
Mkuu Toyota Yaris GR ina performance kubwa uwezi kuiwekea IST ni matusi makubwa. Yaris anashindanishwa na Vw Golf na anamtoa kamasi vizuri.

Angalia mwezi huu Yaris alichofanya huko Nurburg Circuit Ujerumani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…