Ukomo wa Ubunge; wananchi walisema nini kwenye rasimu ya Warioba?

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Moja ya hoja zilizopendekezwa na wananchi katika rasimu ya Katiba mpya ya Tume ya Warioba ilikuwa ni kuweka ukomo wa vipindi vya mtu kuwa mbunge. Mapendekezo yalisema ukomo uwe vipindi vitatu, hata hivyo, Rais Kikwete na bunge la katiba waliikataa hoja hiyo.

Kama ilivyo duniani kote, utumishi wa umma unaukomo. Wakuu wa mashirika ya umma kama EWURA, TCRA, TANESCO n.k ukomo ni vipindi viwili, CAG ukomo ni vipindi viwili. Kwa vyombo ambavyo havina vipindi vya utendaji kama jeshi la polisi, magereza, zimamoto na TPDF, ukomo ni umri wa kustaafu. Kundi pekee nchi hii ambalo halina ukomo wa vipindi wala kustaafu ni hili wabunge. Kazi yao wao inaupekee gani?

Na kwabahati mbaya sana hata hoja ya kuwekewa ukomo au kustaafu kwa wabunge inapoibuliwa, chombo pekee chenye mamlaka ya kujadili na kuamua ni bunge lenyewe, hili hili la akina Job Ndugai, Jenista Muhagama, Wiliam Lukuvi, George Simbachawene n.k, kunaukomo hapo utawekwa? Kama hili la ukomo kwa wabunge limeshindikana, tulitoe kwa wote, waalimu, madaktari, mapolisi na wengine wote wasistaafu, maana hii neno kustaafu limeshindwa kutekelezeka kwa wabunge wetu.

Tunaposhauri ukomo uwepo, hatuwachukii viongozi wetu wala kubeza mchango wao, bali tunatoa fursa kwa watanzania wengine kuja na mawazo mapya ya kuendeleza nchi yetu. Busara iliyotumika kuweka ukomo kwa makundi mengine ya watumishi wa umma, ni busara hiyo hiyo ingetumika kuweka ukomo kwa wabunge pia. Sio busara viongozi wetu mstaafu kwa njia aliyopitishwa mzee John Malechela na kijana wake Livingstone Lusinde.
 
Moja ya hoja zilizopendekezwa na wananchi katika rasimu ya Katiba mpya ya Tume ya Warioba ilikuwa ni kuweka ukomo wa vipindi vya mtu kuwa mbunge. Mapendekezo yalesema ukomo uwe vipindi vitatu, hata hivyo, Rais Kikwete na bunge la katiba waliikataa hoja hiyo.

Well said comrade
Upande wa CCM nasikia reforms zimefanyika na ukomo ni 15 years vipindi vitatu
 
Tunaposhauri ukomo uwepo, hatuwachukii viongozi wetu wala kubeza mchango wao, bali tunatoa fursa kwa watanzania wengine kuja na mawazo mapya ya kuendeleza nchi yetu. Busara iliyotumika kuweka ukomo kwa makundi mengine ya watumishi wa umma, ni busara hiyo hiyo ingetumika kuweka ukomo kwa wabunge pia. Sio busara viongozi wetu mstaafu kwa njia aliyopitishwa mzee John Malechela na kijana wake Livingstone Lusinde.
Naunga mkono hoja
P
 
na iwe hivi
muda wake wa vipindi vitatu ukipita haruusiwi kurudia tena ata baada ya mihula kadhaa kupita yani nikama mtumishi anavyostaafu anakwenda kwenye kilimo na ufigaji na yeye pia vivyo hivyo
 
Naunga mkono hoja
Lakini uongozi ni raha sana hata wewe ndugu ungekuwa mbunge usingefanya reform kama hiyo watu wanapambania matumbo yao bhn 😂😂🚶
 
Ndio maana tunasema, **** hili la kustaafu limeshindikana kwa wabunge, tulitoe kwa wote? Kwani unadhani Rais, Jenerali-TPDF, IGP, CAG, AGP, wakurugennzi wa mashirika ya umma n.k wao ndio wanapenda kustaafu? Kustaafu ni kwa ustawi wa nchi, kunatoa fursa kwa nguvu mpya na mawazo mapya kuwa na mchango kwenye taifa letu.
 
Moja ya hoja zilizopendekezwa na wananchi katika rasimu ya Katiba mpya ya Tume ya Warioba ilikuwa ni kuweka ukomo wa vipindi vya mtu kuwa mbunge. Mapendekezo yalesema ukomo uwe vipindi vitatu, hata hivyo, Rais Kikwete na bunge la katiba waliikataa hoja hiyo.

Kama ilivyo duniani kote, utumishi wa umma unaukomo. Wakuu wa mashirika ya umma kama EWURA, TCRA, TANESCO n.k ukomo ni vipindi viwili, CAG ukomo ni vipindi viwili. Kwa vyombo ambavyo havina vipindi vya utendaji kama jeshi la polisi, magereza, zimamoto na TPDF, ukomo ni umri wa kustaafu. Kundi pekee nchi hii ambalo halina ukomo wa vipindi wala kustaafu ni hili wabunge. Kazi yao wao inaupekee gani?

Na kwabahati mbaya sana hata hoja ya kuwekewa ukomo au kustaafu kwa wabunge inapoibuliwa, chombo pekee chenye mamlaka ya kujadili na kuamua ni bunge lenyewe, hili hili la akina Job Ndugai, Jenista Muhagama, Wiliam Lukuvi, George Simbachawene n.k, kunaukomo hapo utawekwa? Kama hili la ukomo kwa wabunge limeshindikana, tulitoe kwa wote, waalimu, madaktari, mapolisi na wengine wote wasistaafu, maana hii neno kustaafu limeshindwa kutekelezeka kwa wabunge wetu.

Tunaposhauri ukomo uwepo, hatuwachukii viongozi wetu wala kubeza mchango wao, bali tunatoa fursa kwa watanzania wengine kuja na mawazo mapya ya kuendeleza nchi yetu. Busara iliyotumika kuweka ukomo kwa makundi mengine ya watumishi wa umma, ni busara hiyo hiyo ingetumika kuweka ukomo kwa wabunge pia. Sio busara viongozi wetu mstaafu kwa njia aliyopitishwa mzee John Malechela na kijana wake Livingstone Lusinde.
Kikwete alaaniwe kabisa
 
Back
Top Bottom