1. Uislamu ulipoingia ilibidi upambane na dini za asili.
2. Huenda walioeneza Uislamu walikuja Afrika Mashariki kwa malengo mengine kama biashara na si lengo mahsusi la kueneza dini.
3. Uislamu unafundishwa kwa Kiarabu na hicho kinaweza kuwa kikwazo ktk kueneza imani hiyo.
4. Walioeneza Uislamu hawakuwa na support au ufadhili wa serikali au dola za nchi walikotoka, hivyo uwezo wao kifedha ulikuwa mdogo.
5. Ukristo ulienezwa Afrika Mashariki na Wamisionari. Hawa walikuja kwa lengo mahsusi la kueneza dini.
6. Wamisionari walikuwa na msaada na ufadhili wa serikali na dola za nchi walikotokea. Kwa msingi huo walikuwa na ukwasi wa kiwango fulani.
7. Wamisionari walijifunza lugha za wenyeji wa eneo walilolenga kueneza Ukristo. Kwa hiyo Ukristo ulifundishwa na kuenezwa hata kwa lugha za wenyeji.
8. Juhudi kubwa zilifanyika kutafsiri Biblia, vitabu vya sala, na nyimbo za wakati wa ibada, kwa lugha za wenyeji. Zipo Biblia na vitabu vya sala za Kisukuma, Kichaga, etc.
9. Ukristo ulikuwa ndio dini ya MTAWALA hapa Afrika Mashariki hivyo kurahisisha kusambaa kwake.
Cc
Mohamed Said
JK,
Unataka tujadili hili la wingi au uchache wa Waislam na Wakristo Tanganyika.
Lakini tokea mwanzo nimetahadharisha kuwa somo hili litasababisha ubishi mkali.
Uhakika wa kutaka kujua ukweli ni kufanya sensa na kuweka kipengele cha dini.
Kwa zaidi ya miaka 40 kipengele hiki kimeondolewa Tanzania.
Walioondoa wana sababu zao.
Ila nitaeleza suala hili kama nilivyokabiliananalo katika mhadhara niliotoa Chuo Kikuu cha Iowa Marekani mwaka wa 2011.
Katika maswali na majibu niliambiwa na Mmarekani mmoja kuwa Waislam hawana nafasi nyingi katika serikali, vyama vya siasa, nafasi za elimu nk. nk. ukilinganisha na Wakristo kwa kuwa Tanzania Waislam ni "minority," yaani wachache.
Huyu bwana alitoa ushahidi wa takwimu za CIA.
Jibu langu lilikuwa kuwa zipo takwimu za miaka mingi ambazo ni tofauti na takwimu za CIA zinazotoa hesabu tofauti.
Mimi nikasisitiza kuwa tuachane na takwimu zote hizo za CIA na zinginezo tuangalie "political history ya Tanganyika," kama moja ya "variable."
Nikajibu swali kwa kuuliza swali.
Hapa nilikuwa katika mhadhara wa wataalamu wa African History.
Nikawaomba wanipe mfano wa nchi moja duniani iliyokuwa chini ya ukoloni na waumini wa dini iliyokuwa "minority," ndiyo walionyanyua silaha kupambana na mvamizi mkoloni.
Nikawapa mfano wa Vita Vya Maji Maji (1905 - 1907) na majemadari Waislam 67 walionyongwa na Wajerumani na kuzikwa katika kaburi la halaiki Songea.
Nikawauliza iweje baada ya Waafrika kushindwa katika Maji Maji katika "nationalist politics" na madai ya kupigania uhuru wa Tanganyika hao hao "minority," wakaongoza mapambano dhidi ya ukoloni wa Muingereza.
Hawa niliowauliza maswali haya ni maprofesa wa historia katika vyuo mbalimbali Marekani.
Nikawaomba kwa dakika moja waitazame India wakati inapigania uhuru wake na iwe walioongoza mapambano hayo ni Waislam ambao ni wachache wakiongozwa na Mohamed Ali Jinah badala ya Nehru ambae ni Mhindu na ndiyo wengi nchini wakawa katika duru ya nje.
Ukumbi ulikuwa kimya na baridi.
Sikupewa jibu.
Badala yake Mkuu wa Idara ya African History Northwestern University, Evanston Chicago, Jonathon Glassman aliniomba nikafanye mhadhara kama huu chuoni kwake na nilikwenda.
Kiasi muuliza swali alijihisi mdogo.