Ukopaji fedha na jinsi unavyoua Urafiki

Kuandikishana ndio njia nzuri, inamfanya kuwajibika, mimi Mzee wangu huwa anandikishana hata na mafundi wakianza kazi tena Serikali za mtaa, ole uzingue.
 
mkuu wanapenda kulipa ila ndo vile hali tete
Sasa kama unashindwa kulipa kwa wakati, si ni busara kumfuata aliyekukopa na kumweleza challenges zako, huku ukiomba muda zaidi? Kuchikichia kunaleta maana tofauti kabisa.

Nadhani pia wadaiwa wengi wanaassume ile pesa uliyowakopa huihitaji kiviiiile, hasa wanapopiga hesabu zao kichwani na kuconclude kwamba labda una "kipato kikubwa".
 
mkuu naomba madili ya kazi na mimi aisee. naangamia mtaani
 
Kuna mwanafunzi aliulizwa swali na mwalimu wake. 'Kamau, babako akikopa shilingi elfu saba kwa jirani kisha akope elfu tisa kwenye benki, atalipa deni la shilingi ngapi kwa ujumla?' Kamau akasema sufuri. Mwalimu akarudia tena 'elfu saba kwa jirani, elfu tisa kwenye benki. Deni la babako litakuwa la shilingi ngapi?' Kamau akasema tena, 'sufuri.' Mwalimu akajawa na hamaki akamwambia Kamau, 'we kijana hujui hesabu hata kidogo!' Kamau naye akamjibu, 'si eti sijui hesabu mwalimu, wewe ndo humjui babangu!' πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
"Tunaweza Kuwait marafiki bila kuombana pesa" ndio slogan ninayotumia hyo
 
Mtu kama hana kwa mfano hela ya kula msaidie hela ya kula ya siku tuu kwa maana ya elfu tano au ukimwonea huruma elfu kumi.
Nshaachaga muda kukopesha watu wote hata ndugu wa tumbo moja, nimeshatia hela sana na hawarudishi, mbaya zaid anakuja mtu ulishamkopesha na anaomba. Umkopeshe tena.....huwa nina roho gani sijui, siwezag kumkumbusha zaidi na kumwambia tuu sina.

Ukweli wazungu nahisi hawana tabia hii, ndo mana ukitaka kukopa anakuambia nenda bank, na anakushangaa coz hujajipanga.
Acheni kukopa tunaaibishana na kukoseana urafiki, jipange, kama huna usikope mtu, nenda bank, usifanye kitu juu ya matumiz yako ya kawaida, kula kulingana na urefu wa kamba yako.

Usikopeshe mtu, mwache aende bank.
 
Usinikumbushe sijui nna pepo la huruma. Sijui ninywe dawa gani nisitoe hela kiulaini jamani wengine nshasamehe
Ondoa hyo roho, sio dhambi usipomkopesha mtu, zipo bank na financial institution zingine, nshakopesha na kutokana na hilo nimepoteza marafiki sana aisee, ila ni Mungu naona ndo kanipa moyo mgumu wa kutokukopesha tena.
 
Mshikaji wa kwanza alinikopa hela alikuwa amekamatwa na traffic ulivyokuwa anaomba ....nirushie kiasi fulani nikifika na nskurefund, kilichotokea baada ya kufika mbn kimy dah mwanangu nipo sehemu nakula bata nikitoka nakutumia,
 
Hahaaaaa mecheka sana....ukweli yan...kuna watu hawalipi maadeni hata iweje..sasa endelea kuwakopesha.
 
Achana kukopesha watu...namna ya watu kama hawa pasua kichwa.
 
That's the mistake they make "assuming we don't need the money that's why we gave them"
Nakumbuka a few years ago nilikua nimepanga Kinondoni mpangaji mwenzangu (kijana) ambae tulitokea kuzoeana alikua anadaiwa kodi hana pesa, akaja akaniomba nimkopeshe. Kwa moyo mweupe nikamwazima 500,000 na nukamuuliza lini itarudi akasema next month. Nikaona poa tu...keeping in mind hiyo pesa niliplan kununua mahitaji ya mdogo wangu na kumpa p.money ya while akifungua.
Jirani akalipa kodi mwezi ulofuata kapiga kimya nikapotezea, mwezi mwingine tena kimya... Ikabidi nimkumbushe akanipa viswahili akaniambia nimpe muda, bila hiyana nikakubali.
Uzuri nilisha msort dogo akaenda skuli bila shida.
Ila jirani alinikwaza for taking advantage of my kindness.... Siku nkamwabia uvumilivu umenishinda hiyo pesa utatoa bila kupenda.
Nikakaa a week tena harudishi ananiona fala....Siku 1 lunch time nikatoka Mikocheni (offcn) to Victoria (office kwake) kufika reception nikaomba kumuona....
Alishtuka vibaya, but I was composed nikamwambia nnashida na HR wako nataka nimpe haka ka agreement ketu akate pesa yangu tumalizane mi na wewe.
Aliogopa akasema usifike huko naomba tuongee jioni, nikamwambia maongezi sitaki niambie unanipa lini right now... akasema kesho.
Kabla hata ya kesho akaniingizia 500,000 ,na mazoea yakaishia hapo!!!!!
Alinipa funzo kubwa sana, saiv hata aje mtu anatambaa sina helaaaaaaaaaa. Bora zikae kwenye account niziangalie ila sio kuwapa ungrateful people.
 
πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…