Ukopaji fedha na jinsi unavyoua Urafiki

Ukopaji fedha na jinsi unavyoua Urafiki

Nimekopesha na sio mashoga kuna jirani yangu nilimkopesha mpaka leo hajanipa na tunaonana na kuongea vizuri tu wala haonyeshi kulipa deni yaan me kwenye mtu kunikopa huwa hawanirudishii sasa hivi wamenifundisha roho mbaya
Kama unacho toa
 
Chukua Mkeo,watoto wako na wewe mwenyewe then bebeni na Mashuka yenu mpk kwa mdeni wenu.

Kaeni hapo sebuleni na umwambie mkewe leo hatutoki hapa na tutalala hapa kuanzia sasa mpk deni letu litakapolipwa maana nimeshindwa kuendesha familia yangu.FULL STOP
 
Mimi nimewakopesha rafiki zangu wawili Kila mmoja na wakati wake.

October 2014 Jamaa yangu nilimkopesha Milioni moja taslimu. Alikuwa amekwama ktk biashara yake ya miti ya mbao. Hajanilipa mpaka 26/01/2018 saa 13:24 na cmu yangu hapokei. Nikibadili Namba akipokea akijua Mimi anakata simu.

November 2014 nilimkopesha Jamaa yangu mwingine Milioni 2 taslimu. January 2015 alinilipa Milioni moja, ikabaki moja mpaka Leo 26/01/2018, saa 13:30 hajamalizia. Nikimfuata ananipa jibu cjapata Pesa mkuu.

NB: Wote nimeandikishana nao kwa mwanasheria wangu ambae n rafiki yangu.
Kama uliandikishana nao wanyoshe kwenye mkono wa sheria watajifunza kuheshimu makubaliano.
 
Madeni noma, nina mjomba angu nilimkopesha million moja 2016, February.. Akadai ndani ya mwez ananirudishia, nimejuta.. Hatuna mawasiliano mazuri, maana ishu imeshakua ya familia
 
wakati nasoma chuo cousin wangu (RIP ma cousin) sikuwa namuelewa vizuri lakini sasa naelewa kwa nini alikuwa anafanya vile.akija rafiki kumkopa lets say 100,000/ yeye alikuwa anampa kiasi alichokuwa ana feel au alichonacho so anaweza mpa hata 40.000/ na kumwambia hiyo 60,000/akatafute sehemu nyingine yeye amempa kama rafiki....no refund......alikuwa anaogopa kukimbiwa na marafiki......hapa maskani/kijiweni kuna mshikaji alichukua tsh.10,000/kwa muuza matunda hajapita hii njia tangia mwezi wa nne 2017
 
Madeni noma, nina mjomba angu nilimkopesha million moja 2016, February, nimejuta.. Hatuna mawasiliano mazuri, maana ishu imeshakua ya familia
Pole sana aisee. Hiyo jifanye kama umesamehe tu na angalau sasa umepunguza mtu mmoja ambaye hatoweza kuja kuomba mkopo hata siku moja
 
Kama uliandikishana nao wanyoshe kwenye mkono wa sheria watajifunza kuheshimu makubaliano.
Tatizo lipo hapa. Watu wengi huwa wanaona noma kuanza kuandikishana, hasa kama ni rafiki wa karibu sana au ndugu kabisa ila nadhani hii inaweza kusaidia.

Sijui deni lina siri gani. Hata kwa wale wanaokuja kulipa madeni yao, ni wachache nnooo wanaolipa kwa wakati. Mtu akikwambia "nikope ntakulipa sijui wiki/mwezi ujao", wewe multiply atleast mara tatu ya huo muda na toa hela yako huku mind yako imeset kwa timeframe hiyo. Wahenga waliona mbali pale walipokuja na kauli "kukopa harusi, kulipa matanga"
 
Back
Top Bottom