Sasa kama unashindwa kulipa kwa wakati, si ni busara kumfuata aliyekukopa na kumweleza challenges zako, huku ukiomba muda zaidi? Kuchikichia kunaleta maana tofauti kabisa.
Nadhani pia wadaiwa wengi wanaassume ile pesa uliyowakopa huihitaji kiviiiile, hasa wanapopiga hesabu zao kichwani na kuconclude kwamba labda una "kipato kikubwa".
That's the mistake they make "assuming we don't need the money that's why we gave them"
Nakumbuka a few years ago nilikua nimepanga Kinondoni mpangaji mwenzangu (kijana) ambae tulitokea kuzoeana alikua anadaiwa kodi hana pesa, akaja akaniomba nimkopeshe. Kwa moyo mweupe nikamwazima 500,000 na nukamuuliza lini itarudi akasema next month. Nikaona poa tu...keeping in mind hiyo pesa niliplan kununua mahitaji ya mdogo wangu na kumpa p.money ya while akifungua.
Jirani akalipa kodi mwezi ulofuata kapiga kimya nikapotezea, mwezi mwingine tena kimya... Ikabidi nimkumbushe akanipa viswahili akaniambia nimpe muda, bila hiyana nikakubali.
Uzuri nilisha msort dogo akaenda skuli bila shida.
Ila jirani alinikwaza for taking advantage of my kindness.... Siku nkamwabia uvumilivu umenishinda hiyo pesa utatoa bila kupenda.
Nikakaa a week tena harudishi ananiona fala....Siku 1 lunch time nikatoka Mikocheni (offcn) to Victoria (office kwake) kufika reception nikaomba kumuona....
Alishtuka vibaya, but I was composed nikamwambia nnashida na HR wako nataka nimpe haka ka agreement ketu akate pesa yangu tumalizane mi na wewe.
Aliogopa akasema usifike huko naomba tuongee jioni, nikamwambia maongezi sitaki niambie unanipa lini right now... akasema kesho.
Kabla hata ya kesho akaniingizia 500,000 ,na mazoea yakaishia hapo!!!!!
Alinipa funzo kubwa sana, saiv hata aje mtu anatambaa sina helaaaaaaaaaa. Bora zikae kwenye account niziangalie ila sio kuwapa ungrateful people.