Ukopaji fedha na jinsi unavyoua Urafiki

Ukopaji fedha na jinsi unavyoua Urafiki

Dawa ya Deni ni Kulipa tu,
ila Bank zipo wazi kwa kazi ya kukopesha watu sasa kwa nini watu hawaendi kukupa bank?
 
That's the mistake they make "assuming we don't need the money that's why we gave them"
Nakumbuka a few years ago nilikua nimepanga Kinondoni mpangaji mwenzangu (kijana) ambae tulitokea kuzoeana alikua anadaiwa kodi hana pesa, akaja akaniomba nimkopeshe. Kwa moyo mweupe nikamwazima 500,000 na nukamuuliza lini itarudi akasema next month. Nikaona poa tu...keeping in mind hiyo pesa niliplan kununua mahitaji ya mdogo wangu na kumpa p.money ya while akifungua.
Jirani akalipa kodi mwezi ulofuata kapiga kimya nikapotezea, mwezi mwingine tena kimya... Ikabidi nimkumbushe akanipa viswahili akaniambia nimpe muda, bila hiyana nikakubali.
Uzuri nilisha msort dogo akaenda skuli bila shida.
Ila jirani alinikwaza for taking advantage of my kindness.... Siku nkamwabia uvumilivu umenishinda hiyo pesa utatoa bila kupenda.
Nikakaa a week tena harudishi ananiona fala....Siku 1 lunch time nikatoka Mikocheni (offcn) to Victoria (office kwake) kufika reception nikaomba kumuona....
Alishtuka vibaya, but I was composed nikamwambia nnashida na HR wako nataka nimpe haka ka agreement ketu akate pesa yangu tumalizane mi na wewe.
Aliogopa akasema usifike huko naomba tuongee jioni, nikamwambia maongezi sitaki niambie unanipa lini right now... akasema kesho.
Kabla hata ya kesho akaniingizia 500,000 ,na mazoea yakaishia hapo!!!!!
Alinipa funzo kubwa sana, saiv hata aje mtu anatambaa sina helaaaaaaaaaa. Bora zikae kwenye account niziangalie ila sio kuwapa ungrateful people.
Duuuh hatakusahau
 
Rafiki yangu mmoja nilimkopa Laki Sita May 2017. Alikuwa nje ya mji na mkewe akapata emergency, akihitaji hiyo pesa. Kwa kuthamini urafiki wetu, nilimtumia fasta, na elfu kumi juu ya ''kutolea''. Huyu hajalipa mpaka leo. Mwingine alikuwa staff member na akaomba nimkope Laki Nane kwa kuwa alikuwa na shida ya kutoa kagari kake kapya bandarini. Ilikuwa June mwaka jana. Hajalipa mpaka leo.

Jambo la ajabu sasa, naona kama urafiki wetu umetetereka pakubwa sana kwa wote wawili. Sio kwamba nawasumbua kwa kuwadai, la hasha. Naona mmoja yeye hata nikichat nae, ule ukaribu wetu wa zamani haupo tena. Sasa hivi simuoni kabisa WhatsApp na nimeambiwa kabadilisha namba. Huyu wa Laki nane zaidi ya mara mbili amepokea simu zangu na kusema ''nipo busy/meeting mkuu, ntakucheki baadae buddaaa...''. Hakunicheki mpaka kesho kutwa. Last time nilitaka kumpa mchongo wa kazi moja hivi lakini alivyoyeyusha, deal nimempa mwingine.

Anyway, kopa mtu fedha at your own risk. Kwa kuwa ninathamimi sana urafiki, mwaka huu sintomkopa fedha mtu au rafiki yangu yeyote. Kama ni fedha kidogo na nimesukumwa na shida ya mtu, nitatoa msaada bure na halitakuwa deni. As for the two gentlemen, nimeshawasamehe moyoni ila sitawaambia na itakaa iwatese tu.
Well said brother.
Ila umewakopesha pesa nyingi sana. Ndio maana wanashindwa kurudisha.
Na je uliandikishana nao?
 
Kuna mwanafunzi aliulizwa swali na mwalimu wake. 'Kamau, babako akikopa shilingi elfu saba kwa jirani kisha akope elfu tisa kwenye benki, atalipa deni la shilingi ngapi kwa ujumla?' Kamau akasema sufuri. Mwalimu akarudia tena 'elfu saba kwa jirani, elfu tisa kwenye benki. Deni la babako litakuwa la shilingi ngapi?' Kamau akasema tena, 'sufuri.' Mwalimu akajawa na hamaki akamwambia Kamau, 'we kijana hujui hesabu hata kidogo!' Kamau naye akamjibu, 'si eti sijui hesabu mwalimu, wewe ndo humjui babangu!' 😀😀😀

Haha[emoji1]
 
Kuna ndugu yangu alikua na roho ngumu sana, yeye hataki kusikia neno NIKOPESHE. Ukimuomba laki anakupa elfu10 halafu anakwambia nimekupa tu sitokudai. Unajua kwenye maisha unatakiwa bandidu sometimes.
Nimejifunza hiyo falsafa kitambo na nimeitumia kwa mafanikio mpaka mwaka jana nilijisahau nikamkopesha mtu 2m....ilikuwa alipe in 3 months...nimeambulia 0.5 after 10 months....
Nime write off 1.5m....

Over my dead body kukopesha tena....
 
.. je uliandikishana nao?
No, ni msg tu za simu. Kuandikishana brother inahitaji ubandidu flani hivi, especially anayekuja kukopa ni mshkaji wa karibu sana ambaye unajua kabisa ana kipato reasonable. Lesson learnt lakini.
 
That's the mistake they make "assuming we don't need the money that's why we gave them"
Nakumbuka a few years ago nilikua nimepanga Kinondoni mpangaji mwenzangu (kijana) ambae tulitokea kuzoeana alikua anadaiwa kodi hana pesa, akaja akaniomba nimkopeshe. Kwa moyo mweupe nikamwazima 500,000 na nukamuuliza lini itarudi akasema next month. Nikaona poa tu...keeping in mind hiyo pesa niliplan kununua mahitaji ya mdogo wangu na kumpa p.money ya while akifungua.
Jirani akalipa kodi mwezi ulofuata kapiga kimya nikapotezea, mwezi mwingine tena kimya... Ikabidi nimkumbushe akanipa viswahili akaniambia nimpe muda, bila hiyana nikakubali.
Uzuri nilisha msort dogo akaenda skuli bila shida.
Ila jirani alinikwaza for taking advantage of my kindness.... Siku nkamwabia uvumilivu umenishinda hiyo pesa utatoa bila kupenda.
Nikakaa a week tena harudishi ananiona fala....Siku 1 lunch time nikatoka Mikocheni (offcn) to Victoria (office kwake) kufika reception nikaomba kumuona....
Alishtuka vibaya, but I was composed nikamwambia nnashida na HR wako nataka nimpe haka ka agreement ketu akate pesa yangu tumalizane mi na wewe.
Aliogopa akasema usifike huko naomba tuongee jioni, nikamwambia maongezi sitaki niambie unanipa lini right now... akasema kesho.
Kabla hata ya kesho akaniingizia 500,000 ,na mazoea yakaishia hapo!!!!!
Alinipa funzo kubwa sana, saiv hata aje mtu anatambaa sina helaaaaaaaaaa. Bora zikae kwenye account niziangalie ila sio kuwapa ungrateful people.
Hiyo ndo dawa ya wajinga
 
Rafiki yangu mmoja nilimkopa Laki Sita May 2017. Alikuwa nje ya mji na mkewe akapata emergency, akihitaji hiyo pesa. Kwa kuthamini urafiki wetu, nilimtumia fasta, na elfu kumi juu ya ''kutolea''. Huyu hajalipa mpaka leo. Mwingine alikuwa staff member na akaomba nimkope Laki Nane kwa kuwa alikuwa na shida ya kutoa kagari kake kapya bandarini. Ilikuwa June mwaka jana. Hajalipa mpaka leo.

Jambo la ajabu sasa, naona kama urafiki wetu umetetereka pakubwa sana kwa wote wawili. Sio kwamba nawasumbua kwa kuwadai, la hasha. Naona mmoja yeye hata nikichat nae, ule ukaribu wetu wa zamani haupo tena. Sasa hivi simuoni kabisa WhatsApp na nimeambiwa kabadilisha namba. Huyu wa Laki nane zaidi ya mara mbili amepokea simu zangu na kusema ''nipo busy/meeting mkuu, ntakucheki baadae buddaaa...''. Hakunicheki mpaka kesho kutwa. Last time nilitaka kumpa mchongo wa kazi moja hivi lakini alivyoyeyusha, deal nimempa mwingine.

Anyway, kopa mtu fedha at your own risk. Kwa kuwa ninathamimi sana urafiki, mwaka huu sintomkopa fedha mtu au rafiki yangu yeyote. Kama ni fedha kidogo na nimesukumwa na shida ya mtu, nitatoa msaada bure na halitakuwa deni. As for the two gentlemen, nimeshawasamehe moyoni ila sitawaambia na itakaa iwatese tu.
I have a feeling wewe ndo unadaiwa na ndo unawakwepa wenzio. Mkuu walipe wenzio hali ya urafki wenu iwe sawa
 
No, ni msg tu za simu. Kuandikishana brother inahitaji ubandidu flani hivi, especially anayekuja kukopa ni mshkaji wa karibu sana ambaye unajua kabisa ana kipato reasonable. Lesson learnt lakini.
Ha ha haz
Ungemwambia tuandikishane angekimbia na pesa aningechukua
 
I have a feeling wewe ndo unadaiwa na ndo unawakwepa wenzio. Mkuu walipe wenzio hali ya urafki wenu iwe sawa
😀😀😀😀 mkuu kama una deni kalipe tu. Anayetoa hela yake kukukopa haimaanishi hana shida na hela hiyo
 
Mbona kila mtu kakopesha humu, ?? Me huwa nakopesha kuna jamaa kipindi wanazuia viroba alikamatwa navyo akaomba nimsaidie, toka march 2017 Sept 2017 hapokei, nikaamua kusamehe na kufuta number yake ilikuwa inanichefua,

Mwenyewe huwa nakopa na kurudisha sema kuna kaka yangu alinikopesha 150k nikamlipa 100k tu, nyingine nikajisahaulisha, last week kanikopesha tena ila naamini this time nitalipa yote.

Sijisifii kudhurumu ila huyu anajua maisha yangu so haina tatizo.
 
bora ya huyo aliyekudhulumu lakini amejali urafiki wenu
Yeah, huwa tunawasiliana karibia kila siku! But unadhani ikitokea akaniambia ana shida ya pesa nimkopeshe nitafanya hivyo?? Ameshapoteza uaminifu wake kwangu
 
Back
Top Bottom