Ukopaji fedha na jinsi unavyoua Urafiki

Ukopaji fedha na jinsi unavyoua Urafiki

Rafiki yangu mmoja nilimkopa Laki Sita May 2017. Alikuwa nje ya mji na mkewe akapata emergency, akihitaji hiyo pesa. Kwa kuthamini urafiki wetu, nilimtumia fasta, na elfu kumi juu ya ''kutolea''. Huyu hajalipa mpaka leo. Mwingine alikuwa staff member na akaomba nimkope Laki Nane kwa kuwa alikuwa na shida ya kutoa kagari kake kapya bandarini. Ilikuwa June mwaka jana. Hajalipa mpaka leo.

Jambo la ajabu sasa, naona kama urafiki wetu umetetereka pakubwa sana kwa wote wawili. Sio kwamba nawasumbua kwa kuwadai, la hasha. Naona mmoja yeye hata nikichat nae, ule ukaribu wetu wa zamani haupo tena. Sasa hivi simuoni kabisa WhatsApp na nimeambiwa kabadilisha namba. Huyu wa Laki nane zaidi ya mara mbili amepokea simu zangu na kusema ''nipo busy/meeting mkuu, ntakucheki baadae buddaaa...''. Hakunicheki mpaka kesho kutwa. Last time nilitaka kumpa mchongo wa kazi moja hivi lakini alivyoyeyusha, deal nimempa mwingine.

Anyway, kopa mtu fedha at your own risk. Kwa kuwa ninathamimi sana urafiki, mwaka huu sintomkopa fedha mtu au rafiki yangu yeyote. Kama ni fedha kidogo na nimesukumwa na shida ya mtu, nitatoa msaada bure na halitakuwa deni. As for the two gentlemen, nimeshawasamehe moyoni ila sitawaambia na itakaa iwatese tu.
Pole mkuu, tatizo huwezi kuacha kusaidia, mwenzako nina kama laki nane na nusu ipo kwa mabest, na ni kama wewe, urafiki na undugu umepotea kabisa, mimi sifuti majina yao, nikichukuliwa siku za mwisho wangu watalipa kwa kudaiwa na familia yangu..
Ntaendelea kusaidia, na wewe pia uendelee, vyote hivi twaviacha hapa hapa dugu, kwanini visisaidie wengine, acha viwasumbuwe roho zao lakini moyoni kwako ulisaidia wakati unazo..
 
KUKOPA= maana yake wewe unapokea pesa toka kwa mtu na utamrejesea.


KUKOPESHA= Maana yake wewe unatoa pesa yako unampatia mtu na atakurudishia hiyo pesa.....


Naomba kukusahihisha matumizi ya hayo maneno mawili
 
Haki binadamu wabaya sana!huu uzi umezidi kunikumbusha machungu jaman wakopeshwaji ni wakatili mno.Nimetapeliwa pesa zangu za kutosha ila nimemwachia Mungu.Jaman msikopeshe mtu hasa enzi hivi za vyuma vyenye grisi mtakuja kujuta.
 
Haki binadamu wabaya sana!huu uzi umezidi kunikumbusha machungu jaman wakopeshwaji ni wakatili mno.Nimetapeliwa pesa zangu za kutosha ila nimemwachia Mungu.Jaman msikopeshe mtu hasa enzi hivi za vyuma vyenye grisi mtakuja kujuta.

Chartyyyyyy!!!!!!
You good my furendiiii!
 
Daa pole, ndugu kwa yaliyo kukuta sio ww pekee yako mm mwenyewe mwaka jana nimetoa msamaha kwa watu watatu ambao mmoja ni Rafiki pia ndugu alipatwa na shida baba mkwe wake alikuwa taaban nikawa nimempatia kiasi huwezi amini mpaka dak hii akiniona huwa anabadili njia ama kujificha[emoji16]
 
Haki binadamu wabaya sana!huu uzi umezidi kunikumbusha machungu jaman wakopeshwaji ni wakatili mno.Nimetapeliwa pesa zangu za kutosha ila nimemwachia Mungu.Jaman msikopeshe mtu hasa enzi hivi za vyuma vyenye grisi mtakuja kujuta.
halafu nilikuwa nakupigia simu juzi unikopeshe kwa vile ushasoma huu uzi nahisi hutanikopesha aiseee daaaah.
 
Back
Top Bottom