kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #21
Kule kwetu kuna watu wanalala kwenye nyumba zisizo na milango, hivyo huweka miti, michi/mitwangio na mipini ya majembe mlangoni kuzuia watu kuingia ndani wakati watu wamelala usiku. Sasa wana msemo wao unaosema kujifungia sana kwa kutumia miti hiyo malangoni ni kulala nje, wakiwa na maana kwamba kama ukiiweka miti mingi mno na mizito mlangoni inaweza kuelemeana yenyewe kwa yenyewe na kusababisha ianguke chini na kuondoa kizingiti kilichokusudiwa cha watu kuingia ndani.
Kuna watu walibuni vizingiti vingi sana kwa wapinzani kushinda uchaguzi vikiwemo vile vya kuzuia vyama kuungana na kushirikiana, kuzuia harakati za kisiasa kwa miaka 5, kuzuia vyama kupata pesa za kuendeshea uchaguzi, wabunge na wapinzani kuhama vyama, nk.
Matokeo yake leo hii inaonekana kuwa kuna vyama viwili tu vinavyoshiriki uchaguzi huu wa 2020. Hii imesababishwa na vikwazo vingi mno kwa vyama na kuwafanya wapiga kura wote wagawanyike kwenye vyama viwili tu vilivyohimili vikwazo vyote vilivyowekwa na wadau. Kwa maana nyingine vikwazo viiingi kwa vyama vimewarahisishia kazi wapiga kura kubaki na mzigo wa vyama 2 tu vya kupigia kura.
Mizengwe imevimaliza NCCR Mageuzi, CUF, UMD, TLP, NLD,... kwenye mbio za urais. Hata baba wa taifa aliwahi kutamani vibaki vyama 2 tu vikubwa vya siasa Tanzania. Unabii wake karibu utatokea kwa mapenzi ya Mungu.