Uchaguzi 2020 Ukosefu wa hela ya kupiga kampeni wageuka neema kwa vyama vikubwa nchini

Kule kwetu kuna watu wanalala kwenye nyumba zisizo na milango, hivyo huweka miti, michi/mitwangio na mipini ya majembe mlangoni kuzuia watu kuingia ndani wakati watu wamelala usiku. Sasa wana msemo wao unaosema kujifungia sana kwa kutumia miti hiyo malangoni ni kulala nje, wakiwa na maana kwamba kama ukiiweka miti mingi mno na mizito mlangoni inaweza kuelemeana yenyewe kwa yenyewe na kusababisha ianguke chini na kuondoa kizingiti kilichokusudiwa cha watu kuingia ndani.

Kuna watu walibuni vizingiti vingi sana kwa wapinzani kushinda uchaguzi vikiwemo vile vya kuzuia vyama kuungana na kushirikiana, kuzuia harakati za kisiasa kwa miaka 5, kuzuia vyama kupata pesa za kuendeshea uchaguzi, wabunge na wapinzani kuhama vyama, nk.

Matokeo yake leo hii inaonekana kuwa kuna vyama viwili tu vinavyoshiriki uchaguzi huu wa 2020. Hii imesababishwa na vikwazo vingi mno kwa vyama na kuwafanya wapiga kura wote wagawanyike kwenye vyama viwili tu vilivyohimili vikwazo vyote vilivyowekwa na wadau. Kwa maana nyingine vikwazo viiingi kwa vyama vimewarahisishia kazi wapiga kura kubaki na mzigo wa vyama 2 tu vya kupigia kura.

Mizengwe imevimaliza NCCR Mageuzi, CUF, UMD, TLP, NLD,... kwenye mbio za urais. Hata baba wa taifa aliwahi kutamani vibaki vyama 2 tu vikubwa vya siasa Tanzania. Unabii wake karibu utatokea kwa mapenzi ya Mungu.
 
Zito kala hela za Membe halafu anamchinjia baharini mchana kweupe! mwanasiasa yeyote sio wa kuamini.
Zitto Mungu anakuona.
Acha ramli porojo Zitto keshasema kwamba Membe yuko bize kuliandaa baraza la Mawaziri
 
Kabla hujatoa ujinga wako angalia kwaumakini pima unachotaka kukisema act sio kukosa pesa za kampeni balinimkakati wakuitoa ccm njiani act wamesapoti bara chadema wamesapoti visiwani hilondio unaitakukosa pesa zakampeni
 
Kabla hujatoa ujinga wako angalia kwaumakini pima unachotaka kukisema act sio kukosa pesa za kampeni balinimkakati wakuitoa ccm njiani act wamesapoti bara chadema wamesapoti visiwani hilondio unaitakukosa pesa zakampeni
Ndugu yangu Ni ukweli kabisa vyama vyote vya upinzani havina fedha ya kutosha kuendeshea uchaguzi huu. Serikali imehakikisha kuwa hata misaada kutoka kwa marafiki wa nje haiwafikii. Ndio maana hata Chadema inakinga kofia ili kuchangiwa na wananchi hela ya kunywa maji. Unaposema act iko liquid sikatai lakini kauli ya vyama ni hiyo. Ila kusudi langu kwenye huu Uzi Ni kuonyesha namna kila kwenye changamoto kunaibuka fursa hapopo kupitia changamoto hiyo.
 
Haya bana
 
Membe ndiye mwanasiasa mjinga na mpumbavu kuliko wote ambao waliwahi kuwa wana CCM.
Sio mjinga huyu, muda wowote anaweza kumiminiwa pesa na wasiojulikana ili aendelee na kampeni kwa manufaa ya chama Cha mapidozi
 
Sio mjinga huyu, muda wowote anaweza kumiminiwa pesa na wasiojulikana ili aendelee na kampeni kwa manufaa ya chama Cha mapidozi
Very poor argument. By the way, kama unaamini Membe anaweza kutumiwa na CCM, vipi unamwamini Lissu?
 
Nakupa 100% Mkuu, haya yoote uliyoorodhesha na mwisho hilo la Amsterdam umemaliza kila kitu. Huo ndiyo ukweli wenyewe na bado mengi yapo njiani. Hii ni sehemu ndogo tu.
 
Very poor argument. By the way, kama unaamini Membe anaweza kutumiwa na CCM, vipi unamwamini Lissu?
Daa! hakuna asiyekuwa na Bei, lakini Bei ya Lissu inaweza kuwa kubwa Sana kuliko ya mh membe kurudi CCM.
 
Daa! hakuna asiyekuwa na Bei, lakini Bei ya Lissu inaweza kuwa kubwa Sana kuliko ya mh membe kurudi CCM.
Unawezaje usiamini mbwembwe zote za Lissu tangu ajiunge Chadema, mara makesi kibao na hafungwi, mara eti risasi 16 akapona. Mara Ubeleji, mara kavuliwa ubunge, mara akirudi atakamatwa na hakukamatwa, mara mgombea urais wa Chadema. Unaweza kubisha hajanunuliwa na kuandaliwa bila mambulula yanayomshabikia kujua?
 
Hiyo Kali Sasa, yaani anunuliwe huku akubali kuchechemea kwa risasi
 
Wahi Mirembe!!
 
Humjui vizuri Lissu wewe....
 
Kuna kila muujiza mzuri kwa CHADEMA na mgombea wake Tundu Lissu, hata ikibidi mtu mkubwa "atoweke" ili andiko litimie itakuwa hivyo na dadili zote zipo.
Ameen and so shall be
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…