Ukosefu wa huduma ya mtandao (Internet service) umekosesha nchi mapato makubwa ya ndani na nje

Kubwjing

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2025
Posts
3,289
Reaction score
5,964
Wasalaam Aleykhum,

Hatimaye nimefika nyumbani Zanzibar salama majira ya jana jioni na kuswali Isha nyumbani

Mie ni Muislam ninayeogopa Unafik kuliko Shirki (japo dhambi zote mbaya sana mbele ya Allah (S.A.W)

Nimeumizwa na vifo nilivyoshughudia huko bara kwasababu kikazi mi n maranyingi nakuwa bara huko. Nimeona watoto wa miaka wallah haizidi 15 wakifa kwa kupigwa risasi

Kingine katika kazi zetu za Utalii twategemea mtandao kwa asilimia 90 mpaka 95, tulikosa huduma hiyo ya Internet kwa siku zipatazo nne na kuathiri sana upokeaji na uelekezaji wa Wageni kuanzia mapokezi

Wageni wengi sana wameenda nchi jirani ya Kenya kupitia Mombasa na wengine kupanda ndege na kushukia Nairobi- Kenya, tena Wanaisema vibaya sana Nchi yetu hii mpaka watukana kabisa

Wageni hawahusiani kabisa na SIASA wala MAANDAMANO, sasa kwa vipi wanakosa huduma muhimu sana ya Internet?

Kwa vipi watawasiliana na Ndugu zao huko walikotoka pasipo Internet?

Tuwe wakweli Huduma ya Internet kuzuiwa kumesababisha kukosa fedha nyingi katika Mzunguko wa ndani na Fedha za kutoka nje ya nchi

Wallah kwa hili Serikali ilifahamu vyema
 
No data no right to speak.
Kuna nchi inaacha internet itumike kuleta vurugu?
Hao Wageni wa Kizungu wangetumia Internet kuleta vurugu ili wapate nini?
 
No data no right to speak.
Kuna nchi inaacha internet itumike kuleta vurugu?
Ungeongea hivyo mbele ya Wageni waliobook hotels na full accomodation na kulipia before huduma zote ndio ungepokea matusi ya mama yako mzazi mpaka Bibi zako

Wafikiri wenzetu wanapenda ujinga ujinga kwenye mambo yao?
 
Ni sehemu ndogo sana maana hayo yanahusu pesa. Pesa za Tanzania kupatikana na kupotea ni ishu ya kawaida sana na raia wakishajua kuhusu hilo na mifano iko mingi pia na tukisema tuitaje haitaisha.

Ishu kubwa kuliko zote kwa sasa wala si fedha, ni ishu ya uhai. Damu ni nyingi na kama kweli damu inabeba laana basi hili ndo la kutubu kwa Mungu. Damu ina shida sana.
 
Wasalaam Aleykhum,

Hatimaye nimefika nyumbani Zanzibar salama majira ya jana jioni na kuswali Isha nyumbani

Mie ni Muislam ninayeogopa Unafik kuliko Shirki (japo dhambi zote mbaya sana mbele ya Allah (S.A.W)

Nimeumizwa na vifo nilivyoshughudia huko bara kwasababu kikazi mi n maranyingi nakuwa bara huko. Nimeona watoto wa miaka wallah haizidi 15 wakifa kwa kupigwa risasi

Kingine katika kazi zetu za Utalii twategemea mtandao kwa asilimia 90 mpaka 95, tulikosa huduma hiyo ya Internet kwa siku zipatazo nne na kuathiri sana upokeaji na uelekezaji wa Wageni kuanzia mapokezi

Wageni wengi sana wameenda nchi jirani ya Kenya kupitia Mombasa na wengine kupanda ndege na kushukia Nairobi- Kenya, tena Wanaisema vibaya sana Nchi yetu hii mpaka watukana kabisa

Wageni hawahusiani kabisa na SIASA wala MAANDAMANO, sasa kwa vipi wanakosa huduma muhimu sana ya Internet?

Kwa vipi wanawasiliana na Ndugu zao huko walikotoka?

Tuwe wakweli Huduma ya Internet kuzuiwa kumesababisha kukosa fedha nyingi katika Mzunguko wa ndani na Fedha za kutoka nje ya nchi

Wallah kwa hili Serikali ilifahamu vyema
Wasalaam alaykum ndiyo nini muislam usiyependa unafki?
 
Mapato yanini ikiwa hayo mapato wanaiba wanajengea madem.zao majumba wananunua majumba wanahonga askari waue ndugu zetu mapato yanini sasa ikiwa hayo mapato ndio change cha chuki mpaka tunafikia hatua ya kuwana
 
No data no right to speak.
Kuna nchi inaacha internet itumike kuleta vurugu?
Kwa hiyo na yale matokeo kutoka kwenye vituo vya kura mliyapata kwa kutumia njia gani! Mlitumia njia ya simu, au mlitumia magari kusafirisha fomu za matokeo mpaka kwa Mwenyekiti wenu wa tume kule Dodoma?

Halafu kama internet ilitumika kuleta vurugu, mbona hayo maandamano hayakuishia siku ile ile ya tarehe 29 mlipozima? Halafu huo msemo unasema hivi; no research, no right to speak! Na siyo no data no right to speak!!

NB:- kama huna akili timamu usinihangaishe kuyajibu haya maswali yangu.
 
Walivyo hawana akili wataishia kuchapisha pesa
 
Back
Top Bottom