Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Nazungumzia kwa uzoefu wa mitaani, kwenye jamii, mitandaoni na kama mzazi na mlezi
Mitaani na kwenye jamii usasa ndio umeshika hatamu si kwa wazazi/walezi wala watoto wenyewe
Wazazi na walezi kutokana na utandawazi na harakati za maisha hatuna muda wa kukaa na watoto wetu na kuwafunza mambo ya msingi kutoka kwenye vinywa vyetu
Tumewaachia walimu wa shule, madrasa Sunday school na mafundisho watufanyie hizo kazi
Hata pale tunapopata nafasi finyu tutawapa maonyo ya ukali na vitisho kuhusu ulawit, usagaji na mambo ya mahusiano
Hatuna muda wa kuwafunza nini maana ya kuwa mwanaume ama mwanamke halisi
Hatuna muda wa kuwafunza na kuwajengea uwezo wa kujitambua binafsi na dhima yao yakuwa kama walivyo kijinsia
Hatuna muda wa kuwaambia ABC za makuzi kutoka utotoni na kuingia ukubwani
Dhima ya kujitunza kimwili na kiakili
Dhima ya usafi wa kimwili na kiroho
Dhima ya namna ya kuoga na kujisafisha
Hata namna ya kujitunza nywele za aina zote kucha, usafi wa kinywa nk
Hao tunaowaachia watusaidie pamoja na kujitahidi sana lakini kuna kazi ya ziada inatuhudu
Unapoona jukwaani zimejaa mada za malalamiko kwa jinsia kinzani, ama kutaka ushauri wa mambo ya kijinga kabisa unaweza kuona ombwe la maarifa walilonalo watoto wetu