Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Changamoto ya upatikanaji wa maji katika Kijiji cha Oltepes kilichopo Kata ya Orbomba, wilayani Longido huwalazimu wasichana na wanawake wa eneo hilo kutumia siagi ya ng’ombe ili kudhibiti damu ya hedhi na mkojo wa ng’ombe kujisafisha.
Wanawake hao hulazimika kutumia siagi hiyo (mafuta ya ng’ombe) kujipaka maeneo ya sirini, sambamba na vipande vya nguo za zamani ili kuifanya damu hiyo isishike katika nguo zao.
Eneo hilo lenye wakazi wapatao 4,000, hutembea umbali wa kilomita tano kutafuta maji, lakini nyakati za kiangazi wanapolazimika kutumia mkojo wa ng’ombe hutembea mpaka kilomita 10 kutafuta tu maji ya kunywa na kupikia kwenye mabwawa.
Hiyo ni sehemu ya adha wanayoipata wakazi wa maeneo kadhaa wilayani humo, licha ya sera ya maji kuelekeza majisafi na salama yapatikane umbali usiozidi mita 400 kutoka makazi ya watu yalipo.
Elizabeth Olodo (40) ni miongoni mwa wanawake wanaopitia changamoto hiyo kijijini hapo. Katika maisha yake yote, amekuwa akitegemea nguo za zamani na siagi ya ng’ombe ili kudhibiti hedhi yake.
Ingawa ni njia isiyo salama na kawaida, hii imekuwa ni chaguo lake pekee katika eneo ambalo taulo za hedhi ni anasa.
Elizabeth hujipaka siagi hii sehemu za siri ili kuepuka madoa kwenye nguo zake. Wakati wa kiangazi, ambapo maji ni haba, anakutana na changamoto kubwa zaidi kukusanya mkojo wa ng'ombe na kuuweka kwenye ndoo.