Ukosefu wa maji: Watumia mkojo wa ng'ombe kujisafisha wakiwa hedhini

Halfu wanasema kutumia tambara za nguo kujistiri si salama wakati mimi naona hayo mapedi yana kemikali kibao,, tamba zikitumika ambazo ni safi mimi naona ni salama zaidi,, au wenzangu ninyi mnaonaje
Wewe huwa unatumia?
 
Changamoto ya upatikanaji wa maji katika Kijiji cha Oltepes kilichopo Kata ya Orbomba, wilayani Longido huwalazimu wasichana na wanawake wa eneo hilo kutumia siagi ya ng’ombe ili kudhibiti damu ya hedhi na mkojo wa ng’ombe kujisafisha.

Wanawake hao hulazimika kutumia siagi hiyo (mafuta ya ng’ombe) kujipaka maeneo ya sirini, sambamba na vipande vya nguo za zamani ili kuifanya damu hiyo isishike katika nguo zao.

Eneo hilo lenye wakazi wapatao 4,000, hutembea umbali wa kilomita tano kutafuta maji, lakini nyakati za kiangazi wanapolazimika kutumia mkojo wa ng’ombe hutembea mpaka kilomita 10 kutafuta tu maji ya kunywa na kupikia kwenye mabwawa.

Hiyo ni sehemu ya adha wanayoipata wakazi wa maeneo kadhaa wilayani humo, licha ya sera ya maji kuelekeza majisafi na salama yapatikane umbali usiozidi mita 400 kutoka makazi ya watu yalipo.

Elizabeth Olodo (40) ni miongoni mwa wanawake wanaopitia changamoto hiyo kijijini hapo. Katika maisha yake yote, amekuwa akitegemea nguo za zamani na siagi ya ng’ombe ili kudhibiti hedhi yake.

Ingawa ni njia isiyo salama na kawaida, hii imekuwa ni chaguo lake pekee katika eneo ambalo taulo za hedhi ni anasa.

Elizabeth hujipaka siagi hii sehemu za siri ili kuepuka madoa kwenye nguo zake. Wakati wa kiangazi, ambapo maji ni haba, anakutana na changamoto kubwa zaidi kukusanya mkojo wa ng'ombe na kuuweka kwenye ndoo.

Alafu unakuta kuna li kiongozi linaishi kwa ubadhirifu wa pesa ya umma. Huku watu wananawia mikojo
 
Ni bora kununua magoli
Ni bora kununua mashangingi
Ni bora kuhonga watu wahame vyama vya siasa
Ni bora kufanya ziara huku na kule
 
Na kuwanunulia mashehe land rovers..
Utafikiri huko misikitini na makanisani hawatoi sadaka
 
Mmh! Nimejikuta nawaza hivyo hayo maji wanayokunywa hao ng'ombe mpaka wanapata huo mkojo yanatoka wapi?
Maji anauokunywa ng'ombe huko machungani wewe unaweza kunywa au kufanyia matumizi mengine domestic?!
Jibu la swali lako lipo hapa.
 
Mimi nilifikiri Rais akiwa mwanamke haya hayatatokea!!!
Tanzania ni kubwa! Na mfumo wa maisha wa jamii za wafugaji ni mfumo wa maisha ya kuhamahama. Na hata wakiweka makazi yao hali ya mtawanyiko wa makazi yao huwa changamoto kwa sababu utakuta sehemu ambayo zingekaa kaya 20 katika vijiji vya kawaida inakaliwa na kaya moja katika vijiji vya wafugaji ili kila mmoja apate eneo la kuweka mifugo yake bila kuingiliana na mifugo ya jirani zake.
Kwahiyo katika mazingira kama hayo ni ndiyo kupata miundombinu ya maji ya kudumu.
 
Back
Top Bottom