Ukosefu wa Nidhamu Kwa Mfanyakazi

Ukosefu wa Nidhamu Kwa Mfanyakazi

luki2

Member
Joined
Oct 9, 2013
Posts
34
Reaction score
5
Mkuu tafadhali nisaidie katika hili. Anafanya kazi katika kampuni ya mtu binafsi. Mtu huyu amekua na tabia ya kukosa nidhamu kazini mara nyingi kazini anakuja amelewa.

Mwajiri amechukua hatua ya kumsimamisha na sio the first time alishasimama tena kama wiki mbili akarud kazini amemiss behave kwa mara nyingine tena ndo akasimamishwa.

Mhusika amesha kaa zaidi ya mwezi sasa na amekuja anadai mshahara wake na tayari anaenda mahakamani ni mkorofi sana.

Je kitu gan mwajiriwa anatakiwa kufanya/kuchukua hatua gani kwa mfanyakazi wa hivi?

Na je mfanyakazi ana haki ya kuendelea kulipwa mshahara wake?
 
Mbona hiyo kesi nyepesi tu. Kulewa kazini na ikithibitika linaweza kuwa ni kosa la kukufukuzisha kazi hasa kama umeshapewa onyo hapo kabla kama inavyoonekana ktk kesi hii.

Hata hivyo kwa muda wote ambao mfanyakazi amesimamishwa huku uchunguzi ukiendelea anapaswa kulipwa haki yake kama mfanyakazi hususani mshahara. Zama za kumsimamisha mtu bila mshahara zilishapita kitambo.
 
Kitaalamu mwenye kuthibisha kiwango cha mtu kua amelewa ni daktari,maana anaweza kukubana kisheria kwamba nithibitishie kua nilikua nimelewa.
 
Kitaalamu mwenye kuthibisha kiwango cha mtu kua amelewa ni daktari,maana anaweza kukubana kisheria kwamba nithibitishie kua nilikua nimelewa.

Ni kweli lkn vipo pia vipimo vinavyothibitisha hilo. Hata hivyo sheria ya kazi haihitaji uthibitisho beyond reasonable doubt, bali huegamia kwenye uwiano wa mizania (balance of probabilities) So siyo daktari tu anayeweza kuthibitisha ulevi wa mtu kwa kesi kama hii
 
Ok! Lakini ujue sheria za kazi hazikatazi kunywa bali zinakataza ulevi.
So mtaalamu pekee atajua volume ya kilevi na kinaweza kukaa muda gani kichwani.
 
Back
Top Bottom