Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Ukiondoa ushabiki wa Marekani na vyombo vyake vya habari wanaowachochea waukraine wapigane kwa niaba yao lakini ukweli unaopatikana katika matamshi ya waukreni wenyewe kuanzia raisi Zelensky mpaka mameya wa miji mbali mbali ni kwamba vita baina yao na Urusi vimeshawarudisha nyuma sana.Kwanza Zelensky ameomba misaada kwa lugha kali mpaka koo limemkauka ameamua kukaaa kimya.Kwa upande wa msemaji wa kijeshi jana alikiri kwambaa viwanda vyote vya kijeshi vimeshabomolewa na makombora ya Urusi.Kwa upande wa meya wa Mariupol amesema mitaa mingi ya jiji hilo la bandari sasa inashikiliwa na majeshi ya Urusi.
Mpya ya leo ni kuwa baada ya kuhisi ahuweni ya vita baada ya kauli ya mbinu za kivita ya urusi kurudisha nyuma jeshi lake,leo meya wa mji mkuu wa Kiyv amesema mapigano ni makali mno kuzunguka jiji hilo kutokea magharibi na mashariki.Hii ni dalili kuwa Urusu ukiondoa propaganda za NATO amedhamiria kutokurudi nyuma kabla ya kuiteka Ukraine yote.