Ukraine yaishutumu Urusi kwa wizi wa nafaka

Ukraine yaishutumu Urusi kwa wizi wa nafaka

Hapo Russia anachukua siyo kuiba,Nkishakutandika nakusachi kama una chochote nachukua na Viatu nakuvua.Russia kachukua.
 
Hapo Russia anachukua siyo kuiba,Nkishakutandika nakusachi kama una chochote nachukua na Viatu nakuvua.Russia kachukua.
Anaiba Vitani, tena Nafaka, inawezekana ameanza kupungikiwa chakula
 
Hali inazidi kuwa mbaya kwa Putin katika vita hii, hivi sasa Urusi inaiba nafaka za Ukraine na kuziuza.

Hii siyo picha nzuri kwa nchi inayojinasibu inakila kitu na inajitosheleza kuiba nafaka za nchi ndogo kama Ukraine ukilinganisha na uwezo wake. Tena inaiba Vitani.

_______________________________________

Ukraine inasema kwamba 'wezi wa Urusi' wanaiba nafaka yao na kuiuza ughaibuni

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba, anadai kwamba "wezi wa Urusi" wanaiba nafaka ya Ukraine ili kuziuza nje ya nchi, akisema nafaka inapakiwa kwenye meli, ambazo zitapitia Bosphorus – mkondo mwembamba ambao unagawanya pande za Ulaya na bara Asia – ili kuuzwa nje ..

"Ninatoa wito kwa majimbo yote kuwa macho na kukataa mapendekezo yoyote kama hayo. Msinunue vilivyoibiwa. Msiwe washiriki wa uhalifu wa Urusi," Kuleba alisema kwenye Twitter.

BBC haijathibitisha madai hayo. Urusi mnamo Jumanne ilipuuza picha za "bandia" zinazoonyesha meli zikiwa zimejaa nafaka huko Crimea.

Wakati huohuo Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, aliishutumu Urusi kwa kutumia chakula kama silaha katika vita vya Ukraine, akiongeza kuwa ilikuwa ikitwaa nafaka na kuzijaza katika meli kwenye maeneo inayoyadhibiti.

Alisema madhara tayari yanaonekana katika kuongezeka kwa bei ya chakula, mbolea na nishati duniani - na kusababisha mateso zaidi kwa wale wanaohitaji zaidi.

Chanzo BBC.
View attachment 2237156

Hivi Urusi ndo tuseme inaiba leo? Wakati mali za Urusi na raia wa Urusi zimeibiwa na mataifa ya Magharibi na Marekani kwa mabilioni mbona hatukusikia wakiitwa wezi?

Ujinga sipendi.
 
🤣🤣🤣🤣
p_6850101117491867383248_1_5aa3b8774a81614604dd42617df7bc76.jpg
 
Wale tu wanaowaza kwa kutumia wowowo zao ndio wataamini hii propaganda
 
Halaf pia vita ni vita wajomba wakati unapigana na opponent wako anaweza kupasua sahani yako, kuchana shati yako, kupiga mateke paka wako, ilimradi yupo kwenye mapigano

Hiyu Ukraine haishiwi milio, mara nimepigwa ngumi ya jicho, mara jamaa kaning'ata, mara wanakuja watatu.....

Tulia baba hoyo ndio vita na usituambie sisi mana sisi ni watazamaji tu bwashee
 
Ha ha ha ....nmecheka kwa sauti[emoji4]
 
Back
Top Bottom