John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Ukraine imekubali kushiriki mazungumzo ya amani na Urusi, ambapo wajumbe wa pande zote mbili wamepanga kukutana katika eneo la mpaka kati ya Belarus na Ukraine.
Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa ofisi ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, inaelezwa kuwa hakuna masharti yoyote yaliyowekwa katika mazungumzo hayo ya mpakani yanayotarajiwa kufanyika leo Jumatatu Februari 28, 2022.
Awali, Zelensky alikataa kukutana na wajumbe wa Urusi katika eneo lililoainishwa na Serikali ya Urusi kwa madai kwamba taifa hilo kwa sehemu fulani lilipanga uvamizi wake nchini Belarus.
Tangazo hilo limetolewa katika kipindi kifupi baada ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin kuamuru kuwekwa katika hali ya tahadhari kwa silaha za kujikinga katika pasipo kuzitaja silaha za nyuklia.
Akitoa tangazo hilo Rais Putin amesema viongozi wa nchi zinazoongoza Umoja wa Kujihami NATO, wanaruhusu kauli za uchochezi dhidi ya taifa lao, kwa hivyo amewaamuru Waziri wa Ulinzi na mkuu wa majeshi kuliweka jeshi katika mfumo maalumu wa tahadhari.